Rais yeyote yule ana Majukumu mazito sana wananchi tuungane kuwaombea marais wetu

Rais yeyote yule ana Majukumu mazito sana wananchi tuungane kuwaombea marais wetu

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Raisi ni cheo kikubwa sana kinachotawala nchi yeyote duniani hapa

Majukumu ya Raisi ni mazito sana kwasababu anatawala nchi yote kwa ujumla na kuhakikisha kila jambo linakwenda kwa usahihi kama katiba inavyo ongoza.

Inapotokea Raisi ametingwa basi wananchi wakati mwingine wajaribu kuelewa kwamba Raisi ni binadamu kama wao.

Ukweli ni kwamba hakuna Raisi yeyote hapa duniani ataacha kulaumiwa hii ni kwasababu anaongoza watu wa aina mbili:

(1) Watu wanaotoka ngome ya Mungu
(2) Watu wanaotoka ngome ya Shetani

Kulingana na upinzani huu malalamiko hayatakosekana kamwe

Hali kadhalika tukirejelea hotuba za Baba wa Taifa Mwl Nyerere amekuwa mstari wa mbele kupinga udini na ukabila kwasababu tayari huu ni upinzani ili kujenga Taifa njia pekee ni kuunganisha wananchi kuwa wamoja.

Hivyobasi, tuwaombee maraisi wetu waweze kuunganisha wananchi na kuwa familia moja yenye upendo na amani kazi ambayo ni ngumu sana wakati mwingine inaweza kugharimu maisha.

Kuwa jamii moja hii ndio njia pekee ya kujenga Taifa.

SeekPng.com_king-chair-png_427005.png
 
Unaachana kuombea familia yako iondokane na ufukara unaenda kumuombea mtu ambaye ana kila aina ya ulinzi hapa duniani isipokuwa wa roho mtakatifu, rubbish siwezi fanya huo upuuzi
Raisi akiongoza vizuri wewe na familia yako mtaweza kukamilisha malengo kwasababu fedha zinamilikiwa na dola,
 
Unaachana kuombea familia yako iondokane na ufukara unaenda kumuombea mtu ambaye ana kila aina ya ulinzi hapa duniani isipokuwa wa roho mtakatifu, rubbish siwezi fanya huo upuuzi
Hicho kiti kinabeba mustakabali mkubwa sana wa wewe na familia yako, usiangalie nani amekikalia, ombea mtu aliyekatilia hicho kiti waombaji wanajua nini nasema.
 
hivi unawezaje kuwaombea hawa maraisi ya kiafrika ilihali ni waizi wanaowaibia wananchi?
Wakati mwingine wanafanya hivyo kwasababu tofauti , Raisi anaongoza watu wa aina mbili, wanaotoka ngome ya Mungu na ngome ya Shetani, ndio maana haya yanatokea
 
Raisi ni cheo kikubwa sana kinachotawala nchi yeyote duniani hapa

Majukumu ya Raisi ni mazito sana kwasababu anatawala nchi yote kwa ujumla na kuhakikisha kila jambo linakwenda kwa usahihi kama katiba inavyo ongoza...
Marais huwa wanaweza kuwa na dhamira njema kabisa Kwa nchi na wananchi Kwa ujumla,tatizo huwa ni washauri wenye Nia ovu ndio huwafanya Marais waonekane wabaya.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Raisi ni cheo kikubwa sana kinachotawala nchi yeyote duniani hapa

Majukumu ya Raisi ni mazito sana kwasababu anatawala nchi yote kwa ujumla na kuhakikisha kila jambo linakwenda kwa usahihi kama katiba inavyo ongoza...
Peleka njaa zako huko. Unadhani Mungu ni mnafiki wa kusikiliza maombi ya kinafiki kutoka kwa watu waovu? Eti tumuombee.
 
Hicho kiti kinabeba mustakabali mkubwa sana wa wewe na familia yako, usiangalie nani amekikalia, ombea mtu aliyekatilia hicho kiti waombaji wanajua nini nasema.
Kwa hiyo issue siyo kuongoz kwa kufuata katiba, sheria na taratibu isipokuwa ni kwa maombi? mimi sina huo muda wa kuombea mtu ambaye hanihusu nikaacha familia yangu ambayo itanisaidia hata nikipata matatizo, kufa leo uone kama atafika hata kwenye msiba wako pamoja na maombi yako.
 
Tunaheshimu mawazo yako, Je Raisi akadhoofisha mzunguko wa fedha tutaweza kujikimu?
 
Back
Top Bottom