Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Sintashangaa kwamba katika maraisi wote wa Tanzania, Raisi Samia atakuwa anashikilia rekodi ya kuteua na kutumbua, na kama bado hashikilii hiyo rekodi, basi ataishikilia hivi punde, na huenda ikawa ni rekodi ya raisi aliyeteua na kutumbua kwa kiwango cha juu zaidi duniani!
Nataka nikueleze wazi Raisi Samia kwamba huwezi kutoa samaki mzuri katika kapu lenye kutoa harufu ya samaki waliovunda. Hawa waeule wako, utawajaribu kila mahali, na mwishowe bado utaona wanapwaya katika nafasi unazowapa.
Sasa ninavyoona hapa una matatizo makubwa mawili katika kuteua kwako; kwanza unateua watu wale wale waliopwaya katika nafasi fulani, ukiwa na matumaini kwamba wataweza katika nafasi nyingine. Hilo halitatokea kamwe. Maini yataendelea kuwa maini katika bucha zote.
Pili ni kwamba, nimeona katika uteuzi wako uko sensitive sana katika dini ya mtu unaemteua. Ni rahisi kuona mara nyingi unaanza na sifa ya udini, kwamba nafasi hii nataka ichukuliwe na mwislamu/mkristo, halafu ndio unatafuta mtu wa kuijaza. Unajaribu ku-balance udini katika wateule wako. That is a very wrong approach, lakini naelewa kwa nini unafanya hivyo.
Ushauri wangu kwako, na nakuhakikishia ukifuata ushauri huu utafanikiwa sana, kubali kuingiza watu wa upinzani au hata watu wasio na vyama vya siasa katika teuzi zako. Kumbuka hilo linafanyika sasa kule Zanzibar bila matatizo, lilifanyika Kenya likafanikiwa na sasa wanalifanya tena, na pia sasa linafanyika South Africa na kwingineko.
Achana na conservatives katika CCM wanaokuambia huwezi kuwaweka watu wa upinzani kwenye baraza lako la mawaziri, au teuzi zako za mawaziri, mabalozi nk. Na unapaswa kuteua watu hao bila kuwataka wajiunge na CCM. Wateue na waambie waendelee kuwa na vyama vyao kisiasa na kuwajibika kwako kikazi. Teua Watanzania wanaoweza kazi, sio vyama vyao vya siasa. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa, kumbuka hilo.
Kwa mfano, umeona kwamba tuna matatizo makubwa katika utendaji wa jeshi la polisi, hadi wamefikia kiwango cha wao kuwa wahalifu sasa, kwa sababu wanaichukulia CCM for granted. Mimi ningekushauri kwamba wizara ambazo zinakuletea lawama sana kama raisi, kama Mambo ya Ndani na Maliasili na Utalii, wape watu wa Upinzani waziongoze. Mwaka 1994, Mandela wa ANC alipokuwa Raisi wa South Africa, alimpa Buthelezi wa Inkatha Freedom Party kuongoza wizara ya Mambo ya Ndani kwa sababu ilionekana kuwa wizara yenye matatizo sana, ambayo yalihusishwa na Inkatha Party ya Buthelezi. Sasa kama wananchi wana malalamiko sana na Polisi na Uhamiaji, wape Wapinzani waongoze Wizara hiyo. Mteue Mbowe, Tundu Lissu au Lema awe waziri wa mambo ya ndani, mwache yeye aliunde upya jeshi la polisi - si itakuwa kwa faida ya Watanzania, pamoja na CCM?
Pia, acha kufikiria dini kabla ya kutafuta mtu wa kujaza nafasi fulani. Kuna wakati Nyerere aliulizwa swali, hivi katika baraza lako la mawaziri kuna waislamu wangapi na Wakristo wangapi, akashangaa, na kusema hajui, na hajawahi hata kufikiria kama huyu ni mkristo au muislamu anapofanya uteuzi. Najua wewe ni tofauti na Nyerere, unafikiria suala la udini unapofanya uteuzi, na huenda hata unajua idadi ya mawaziri wakristo na waislamu katika baraza lako. Achana mtazamo huo kabisa. Sio tatizo kuwa na mawaziri wengi wakristo au waislamu - ili mradi ni watu makini, wachapa kazi na wazalendo wa kweli walioteuliwa.