Raisi Samia, utatembelea bucha zote lakini maini ni yale yale!

Sintashangaa kwamba katika maraisi wote wa Tanzania, Raisi Samia atakuwa anashikilia rekodi ya kuteua na kutumbua, na kama bado hashikilii hiyo rekodi, basi ataishikilia hivi punde, na huenda ikawa ni rekodi ya raisi aliyeteua na kutumbua kwa kiwango cha juu zaidi duniani!

Nataka nikueleze wazi Raisi Samia kwamba huwezi kutoa samaki mzuri katika kapu lenye kutoa harufu ya samaki waliovunda. Hawa waeule wako, utawajaribu kila mahali, na mwishowe bado utaona wanapwaya katika nafasi unazowapa.

Sasa ninavyoona hapa una matatizo makubwa mawili katika kuteua kwako; kwanza unateua watu wale wale waliopwaya katika nafasi fulani, ukiwa na matumaini kwamba wataweza katika nafasi nyingine. Hilo halitatokea kamwe. Maini yataendelea kuwa maini katika bucha zote.

Pili ni kwamba, nimeona katika uteuzi wako uko sensitive sana katika dini ya mtu unaemteua. Ni rahisi kuona mara nyingi unaanza na sifa ya udini, kwamba nafasi hii nataka ichukuliwe na mwislamu/mkristo, halafu ndio unatafuta mtu wa kuijaza. Unajaribu ku-balance udini katika wateule wako. That is a very wrong approach, lakini naelewa kwa nini unafanya hivyo.

Ushauri wangu kwako, na nakuhakikishia ukifuata ushauri huu utafanikiwa sana, kubali kuingiza watu wa upinzani au hata watu wasio na vyama vya siasa katika teuzi zako. Kumbuka hilo linafanyika sasa kule Zanzibar bila matatizo, lilifanyika Kenya likafanikiwa na sasa wanalifanya tena, na pia sasa linafanyika South Africa na kwingineko.

Achana na conservatives katika CCM wanaokuambia huwezi kuwaweka watu wa upinzani kwenye baraza lako la mawaziri, au teuzi zako za mabalozi nk. Na unapaswa kuteua watu hao bila kuwataka wajiunge na CCM. Wateue na waambie waendelee kuwa na vyama vyao kisiasa na kuwajibika kwako kikazi. Teua Watanzania wanaoweza kazi, sio vyama vyao vya siasa. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa, kumbuka hilo.

Kwa mfano, umeona kwamba tuna matatizo makubwa katika utendaji wa jeshi la polisi, hadi wamefikia kiwango cha wao kuwa wahalifu sasa, kwa sababu wanaichukulia CCM for granted. Mimi ningekushauri kwamba wizara ambazo zinakuletea lawama sana kama raisi, kama Mambo ya Ndani na Maliasili na Utalii, wape watu wa Upinzani waziongoze. Mwaka 1994, Mandela wa ANC alipokuwa Raisi wa South Africa, alimpa Buthelezi wa Inkatha Freedom Party kuongoza wizara ya Mambo ya Ndani kwa sababu ilionekana kuwa wizara yenye matatizo sana, ambayo yalihusishwa na Inkatha Party ya Buthelezi. Sasa kama wananchi wana malalamiko sana na Polisi na Uhamiaji, wape Wapinzani waongoze Wizara hiyo. Mteue Mbowe, Tundu Lissu au Lema awe waziri wa mambo ya ndani, mwache yeye aliunde upya jeshi la polisi - si itakuwa kwa faida ya Watanzania, pamoja na CCM?

Pia, acha kufikiria dini kabla ya kutafuta mtu wa kujaza nafasi fulani. Kuna wakati Nyerere aliulizwa swali, hivi katika baraza lako la mawaziri kuna waislamu wangapi na Wakristo wangapi, akashangaa, na kusema hajui, na hajawahi hata kufikiria kama huyu ni mkristo au muislamu anapofanya uteuzi. Najua wewe ni tofauti na Nyerere, unafikiria suala la udini unapofanya uteuzi, na huenda hata unajua idadi ya mawaziri wakristo na waislamu katika baraza lako. Achana mtazamo huo kabisa. Sio tatizo kuwa na mawaziri wengi wakristo au waislamu - ili mradi ni watu makini, wachapa kazi na wazalendo wa kweli walioteuliwa.
Maini kweli ni yale yale lakini hata mabwana Afya huwa wanatembelea machinjioni kupima maini yenye kugundulika na vimelea vya maradhi huwa yanachomwa moto !
 
Raisi Samia, nilikuambia utatembelea bucha zote, maini ni yale yale, naona bado hujanielewa!
 
Hadi sasa ndio anashikilia hiyo rekodi. Ana miaka 3 ila kila taasisi ina wakurugenzi 4 ama 5. Kila wizara una mawaziri 3 am 4, kila halmashauri ina wakuu wa wilaya 3 ama 3, wakurugenzi, ras ama das, rc na wote wanaoteuliwa.
Naona mtu wetu kaamua kununua maini bucha nyingine tena, akitarajia safari yatakuwa tofauti!
 
SSH ana shida hapendi watu wampite umaarafu, wachapakazi kama Lukuvi, Slaa, Kalemani, Majaliwa, Kabudi, Polepole, Bashiru hawa walikuwa watendaji wazuri angewatumia vizuri wangemsaidia sana na kuepuka matatizo mengi na mikataba mibovu
Safari hii kapitiliza. Kumweka Kabudi utamaduni nadhani ni kupita kiasi! Kabudi anapaswa ajitambue sasa, atambue maisha sio lazima uwe waziri!
 
Sintashangaa kwamba katika maraisi wote wa Tanzania, Raisi Samia atakuwa anashikilia rekodi ya kuteua na kutumbua, na kama bado hashikilii hiyo rekodi, basi ataishikilia hivi punde, na huenda ikawa ni rekodi ya raisi aliyeteua na kutumbua kwa kiwango cha juu zaidi duniani!

Nataka nikueleze wazi Raisi Samia kwamba huwezi kutoa samaki mzuri katika kapu lenye kutoa harufu ya samaki waliovunda. Hawa waeule wako, utawajaribu kila mahali, na mwishowe bado utaona wanapwaya katika nafasi unazowapa.

Sasa ninavyoona hapa una matatizo makubwa mawili katika kuteua kwako; kwanza unateua watu wale wale waliopwaya katika nafasi fulani, ukiwa na matumaini kwamba wataweza katika nafasi nyingine. Hilo halitatokea kamwe. Maini yataendelea kuwa maini katika bucha zote.

Pili ni kwamba, nimeona katika uteuzi wako uko sensitive sana katika dini ya mtu unaemteua. Ni rahisi kuona mara nyingi unaanza na sifa ya udini, kwamba nafasi hii nataka ichukuliwe na mwislamu/mkristo, halafu ndio unatafuta mtu wa kuijaza. Unajaribu ku-balance udini katika wateule wako. That is a very wrong approach, lakini naelewa kwa nini unafanya hivyo.

Ushauri wangu kwako, na nakuhakikishia ukifuata ushauri huu utafanikiwa sana, kubali kuingiza watu wa upinzani au hata watu wasio na vyama vya siasa katika teuzi zako. Kumbuka hilo linafanyika sasa kule Zanzibar bila matatizo, lilifanyika Kenya likafanikiwa na sasa wanalifanya tena, na pia sasa linafanyika South Africa na kwingineko.

Achana na conservatives katika CCM wanaokuambia huwezi kuwaweka watu wa upinzani kwenye baraza lako la mawaziri, au teuzi zako za mawaziri, mabalozi nk. Na unapaswa kuteua watu hao bila kuwataka wajiunge na CCM. Wateue na waambie waendelee kuwa na vyama vyao kisiasa na kuwajibika kwako kikazi. Teua Watanzania wanaoweza kazi, sio vyama vyao vya siasa. Tanzania ni kubwa kuliko vyama vya siasa, kumbuka hilo.

Kwa mfano, umeona kwamba tuna matatizo makubwa katika utendaji wa jeshi la polisi, hadi wamefikia kiwango cha wao kuwa wahalifu sasa, kwa sababu wanaichukulia CCM for granted. Mimi ningekushauri kwamba wizara ambazo zinakuletea lawama sana kama raisi, kama Mambo ya Ndani na Maliasili na Utalii, wape watu wa Upinzani waziongoze. Mwaka 1994, Mandela wa ANC alipokuwa Raisi wa South Africa, alimpa Buthelezi wa Inkatha Freedom Party kuongoza wizara ya Mambo ya Ndani kwa sababu ilionekana kuwa wizara yenye matatizo sana, ambayo yalihusishwa na Inkatha Party ya Buthelezi. Sasa kama wananchi wana malalamiko sana na Polisi na Uhamiaji, wape Wapinzani waongoze Wizara hiyo. Mteue Mbowe, Tundu Lissu au Lema awe waziri wa mambo ya ndani, mwache yeye aliunde upya jeshi la polisi - si itakuwa kwa faida ya Watanzania, pamoja na CCM?

Pia, acha kufikiria dini kabla ya kutafuta mtu wa kujaza nafasi fulani. Kuna wakati Nyerere aliulizwa swali, hivi katika baraza lako la mawaziri kuna waislamu wangapi na Wakristo wangapi, akashangaa, na kusema hajui, na hajawahi hata kufikiria kama huyu ni mkristo au muislamu anapofanya uteuzi. Najua wewe ni tofauti na Nyerere, unafikiria suala la udini unapofanya uteuzi, na huenda hata unajua idadi ya mawaziri wakristo na waislamu katika baraza lako. Achana mtazamo huo kabisa. Sio tatizo kuwa na mawaziri wengi wakristo au waislamu - ili mradi ni watu makini, wachapa kazi na wazalendo wa kweli walioteuliwa.
Sasa wewe unataka mpasuko ndani ya CCM utokee kwake maana katika vitu ambavyo atakuwa kaenda wrong ndani ya chama ni kufanya teuzi hizo kuwapa wapinzani tena ambao hawajaungama kwa CCM
 
Kule Zanzibar wanafanya. Kuteua wapinzani wawili au watatu sio mbaya, na ni namna ya kukubali yaishe. Nilitoa mfano wa Mandela na Buthelezi kule bondeni. ANC na Inkatha Freedom Party, IFP, walikuwa na uadui mkubwa sana, waliuana vibaya. Lakini Mandela alipendekeza kwa ANC wampe Buthelezi uwaziri wa mambo ya ndani. Alipingwa na kuzomewa, lakini hatimae watu waliona lojiki yake.
 
HUYO MWANAMKE HAFAI KUWA RAIS WA NCHI LEO NDIO NIMEAMINI.

MAMA ABDUL JINGA KABISA.
 
Kule Zanzibar wanafanya. Kuteua wapinzani wawili au watatu sio mbaya, na ni namna ya kukubali yaishe. Nilitoa mfano wa Mandela na Buthelezi kule bondeni. ANC na Inkatha Freedom Party, IFP, walikuwa na uadui mkubwa sana, waliuana vibaya. Lakini Mandela alipendekeza kwa ANC wampe Buthelezi uwaziri wa mambo ya ndani. Alipingwa na kuzomewa, lakini hatimae watu waliona lojiki yake.
Kule walikiamsha wakati wa maalim seifu sharifu hamadi walipata mpaka wakimbizi kwaiyo kuna selekali ya umoja wa kitaifa huku kiongozi yoyote wa juu akifanya hicho kitu ataonekana hafai ndani ya CCM
 
Nadhani tutumie tu busara ya Mandela. Kwa mfano, kama Chadema wanasema Polisi wanafanya uzembe kukamata wasiojulikana, na kama kweli serikali haihusiki na utekaji, basi wape Chadema waongoze wizara ya mambo ya ndani, na kama raisi muagize waziri wa Chadema kwamba anataka sisisikie tena mambo ya utekaji ndani ya miazi mitatu ijayo!

Sangara hukaangwa kwa mafuta yake mwenyewe!
 
Nafikiri mkuu hapa jambo la muhimu tupate katiba mpya ndio itakuwa suluhisho la magonjwa yote hayo unayoyazungumza
 
Katiba mpya ni mpango wa muda mrefu, in the meantime kuna issue zinataka solution za haraka
 
Back
Top Bottom