SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Hivi karibuni, Simba wametoa poster moja ya "Kwa Mkapa Hatoki Mtu" ikiambatana na picha ya Moses Phiri akiwa vitani akiwa amezungukwa na moto.
Mimi sijawahi kupenda hizi graphics toka enzi zile zinaanza kutumika ila nilijua kuna mambo ukiyasema nchi hii unaweza kupigwa mawe ingawa unaweza kuwa sahihi.
Siku ya jana Raja Casablanca wametoa clip moja wakitumia graphics hiyo kwa nyuma na mbele kuna jamaa mwenye rangi ya kijani amewekwa akipayuka maneno "Kunta Kinte now we're coming!", kwa tafsiri isiyo rasmi "Kunta Kinte, tunakuja kwa ajili yako!".
Nimeambatanisha clip hiyo.
Nitawaachia wenyewe mtafute Kunta Kinte ni nani ila nitakwambia kwa nini yule mtu ni wa kijani. Yule mpayukaji ni wa kijani kutaka kuonyesha kuwa graphics za Simba ni cheap na za kizamani, kwamba hazijafanywa vizuri.
Baada ya kuona kejeli yao kama haikueleweka maana nimesoma majibu ya wengi sikuona kama kuna aliyekuwa ameelewa walichomaanisha, wao wakatengeneza poster yao kali kishenzi, ikionyesha TAI mkubwa zaidi ya Mlima Kilimanjaro halafu wakaambatanisha maneno "Coming for the Serengeti", kwa tafsiri yangu "Tunakuja kupambana na au kuchukua Serengeti nzima" wakiwa na maana hawaji tu kupambana na Simba ila na wanyama wote wa mwituni! Nadhani hapa pia wengi hawakuelewa point yao.
Simba kweli wako mbali. Wameshaachana na wala mihogo sasa wanajenga utani wa jadi na timu kubwa kubwa huko duniani. Hizi ni kejeli tu kama ambavyo huwa tunatambiana Yanga na Simba na kukandia mazuri ya mwenzako kwa sababu pamoja na mimi kutozipenda ila graphics zile za Simba siyo mbaya kihivyoo.