Raja Casablanca wakejeli graphics za Simba

Raja Casablanca wakejeli graphics za Simba

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Hivi karibuni, Simba wametoa poster moja ya "Kwa Mkapa Hatoki Mtu" ikiambatana na picha ya Moses Phiri akiwa vitani akiwa amezungukwa na moto.
20230214_100119.jpg

Mimi sijawahi kupenda hizi graphics toka enzi zile zinaanza kutumika ila nilijua kuna mambo ukiyasema nchi hii unaweza kupigwa mawe ingawa unaweza kuwa sahihi.

Siku ya jana Raja Casablanca wametoa clip moja wakitumia graphics hiyo kwa nyuma na mbele kuna jamaa mwenye rangi ya kijani amewekwa akipayuka maneno "Kunta Kinte now we're coming!", kwa tafsiri isiyo rasmi "Kunta Kinte, tunakuja kwa ajili yako!".

Nimeambatanisha clip hiyo.

Nitawaachia wenyewe mtafute Kunta Kinte ni nani ila nitakwambia kwa nini yule mtu ni wa kijani. Yule mpayukaji ni wa kijani kutaka kuonyesha kuwa graphics za Simba ni cheap na za kizamani, kwamba hazijafanywa vizuri.

Baada ya kuona kejeli yao kama haikueleweka maana nimesoma majibu ya wengi sikuona kama kuna aliyekuwa ameelewa walichomaanisha, wao wakatengeneza poster yao kali kishenzi, ikionyesha TAI mkubwa zaidi ya Mlima Kilimanjaro halafu wakaambatanisha maneno "Coming for the Serengeti", kwa tafsiri yangu "Tunakuja kupambana na au kuchukua Serengeti nzima" wakiwa na maana hawaji tu kupambana na Simba ila na wanyama wote wa mwituni! Nadhani hapa pia wengi hawakuelewa point yao.

20230214_095915.jpg

Simba kweli wako mbali. Wameshaachana na wala mihogo sasa wanajenga utani wa jadi na timu kubwa kubwa huko duniani. Hizi ni kejeli tu kama ambavyo huwa tunatambiana Yanga na Simba na kukandia mazuri ya mwenzako kwa sababu pamoja na mimi kutozipenda ila graphics zile za Simba siyo mbaya kihivyoo.

Anasema 'Kunta Kinte nao wakome nao wakooome pay play low lost forever nao wakooome....' 😂😂😂
 
Kuna kingine huyo jamaa amesema. Amesema "Pepe's long lost brother, now we are coming!". Nimekutana na maana hii ya "Pepe's little brother". Mwenye uelewa wa reference hii atujuze nisije nikasema kituko.

20230214_211528.jpg
 
View attachment 2517675
Bother yourself hajasema hivyo mimi sijasikia Pepe wala Chili kwenye hio clip... Don't exaggerate
 
Mboni Posta yao ni nzuri sana wanatutangazia utalii wa nje & ndani, shida ipo wapi? Mimi sijaona ubaya wowote wakitaka hata Kituro tutawapeleka
Poster yao kali saaana ila sijaelewa hiyo mistari ya kushoto ina maana gani. Ndiyo maana nasema ni kejeli tu kuonyesha "hivi ndiyo jinsi ya kutengeneza poster sasa"
 
Poster yao kali saaana ila sijaelewa hiyo mistari ya kushoto ina maana gani. Ndiyo maana nasema ni kejeli tu kuonyesha "hivi ndiyo jinsi ya kutengeneza poster sasa"
Hio Posta yao ni dunia nyingine hii ya Simba ni ya local designer tu sio professional designer ndio maana unaona utofauti ulivyo,
 
Hapana msikilize kwa umakini huyo anaongea kiswahili ili Simba wamuelewe, ameongea kiswahili kwenye hio clip
Mbona na wewe umenukuhu maneno ya kiingereza pia "pay play low lost forever"?
 
Mbona na wewe umenukuhu maneno ya kiingereza pia "pay play low lost forever"?
Ndio hilo anetaja kati pale.. Ila anasema Kunta Kinte nao wakome (km walivyopigwa wale 5 basi na Simba wakome)
 
Hayo maneno ya kiingereza mzee umetuingiza chaka kabisa
Sikiliza tena au kingereza kigumu mzee una matatizo ya masikio?

'Kunta Kinte nao wakome nao wakome [pay] [play low] [lost forever] nao wakomeee...'

Fungua hio code

Sikiliza tena kwa umakini, kuna watu mna matatizo ya masikio ndio tatizo
 
Sikiliza tena au kingereza kigumu mzee una matatizo ya masikio?

'Kunta Kinte nao wakome nao wakome pay play low lost forever nao wakomeee...'

Sikiliza tena kwa umakini, kuna watu mna matatizo ya masikio ndio tatizo
Sasa wewe kwa mtazamo wako "pay play low lost forever" ina maana gani?
 
Back
Top Bottom