Habari za mda huu watu wa nguvu !
Naomba kutoa elimu kidogo kuelewesha kuhusu jambo fulani, kuna uzi hapa nimeona jamaa anadai shekhe anakataza watu wasifuturu na makafiri.
kwanza tuelewe maana ya kafiri ni nn!? kufunga na kufuturu ni kwa kina nani waliokusudiwa!?
kafiri ni neno la kiarabu la linaloandikwa ''kafir'' yaani asiyeamini , kingereza infidel au nonbeliever.....Ukiangalia aya ya kufunga ilikuja kwa wanaoamini tu basi wala sio makafir ,ina maana kafiri (nonbeliever) haruhusiwi kufunga hata kufuturu ,maana kufuturu ni maalum kwa wanaofungatu ,mwingine atakula tu ila sio kufuturu yaani kama haujafunga unachokula sio futari .
Ayah ya funga Surah Al Baqara, ayah
183
''Enyi mlioamini,Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu'' Neno nililopigia mstari ndio point yangu, kwamba walioamini tu ina maana kama huamini huwezi kufunga kwa mujibu wa sheria za kiislamu.
KUFUTURU ni nin?
Kufuturu ni chakula au kinywaji ambacho mtu aliyefunga anakula au kunywa baada ya siku kuisha ,kufikia ukomo wa kufunga kisheria kuanzia alfajiri linapochomoza jua mpaka jioni linapozama jua...Chochot iwe kinywaji au chakula anachokula alaiyefunga ndio kufuturu .
kile unachokula awali ndi kufuturu na kufungua pale kama ulikunywa maji ,tunda ,chakula chochote pale ndio umefuturu na sio vyakula kibao. kwa misingi hii ambaye haamini (kafir) hawezi kufuturu kisheria kwamba hana uwezo wa kufunga kisheria ,haiwezekani mtu asiyeamini akafunga hata uje kijamii isipokuwa wale ambao hawaruhusiwi kufunga kisheria kama ;
- Wagojwa
- Kichaa (mwendawazimu)
- Msafiri(mtu aliye kweny safari)
- Wazee
- Wanawake waliopo kweny hedhi/damu ya uzazi
- Wanawake weny mimba na wanaonyonyesha
Licha ya hao kuwa na udhuru wa kutokufunga kisheria ,wapo ambao watalipia ila wenye hali za kudumu kama wazee wao ni ''exceptional'' kweny kufunga.
Sambamba na hili , kweny kufuturu hao hawawezi kufuturu bali kama wakila pamoja na waliofunga ,wanakula kawaida kama kila siku ila sio futari kwa vile kufutur ni wa waliofunga tu.!!
NB: UZI HUU NI MAHSUSI KWA AJILI YA KUELIMISHA WALA SIO MALUMBANO , NIWATAKIENI KWARESMA NA RAMADHANI NJEMA 🤲