Ramadhan Special Thread

Hlf ple ulipopata ajali sio maeneo yale ya scaba scuba?
 
Waalaykum Salaam Warahmatullaah Wabarakaatuh
 
Kama mnaishi karibu bora mtoto awe anakuja kukuletea maana itakupa amani zaidi kuliko kwenda hapo.
 
Sawa mwalimu shukran
 
Waaleykum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,
Rafiki yupo sahihi na wala usijisikie vibaya kwenda kupata iftar kwake, hiyo ni sadaka nzuri kwa hiyo familia,

Umesahau kua tumeambiwa tuftari nje na kila Muislam apitae aweze kupata iftar? Huu ni mwezi wa kuchuma usiwanyime wenzio rizki.
 
[emoji617]JE INAFAA KUFUNGA BILA YA KULA DAKU[emoji780]


❪[emoji411]❫ السُّــــ☟ـــؤَال : ﻫﻞ ﻳﺠﻮﺯ اﻟﺼﻴﺎﻡ ﺑﺪﻭﻥ ﺳﺤﻮﺭ؟ ﻭﺟﺰاﻛﻢ اﻟﻠﻪ ﺧﻴﺮا.


[emoji404]Swali: je inafaa kufunga bila ya kula daku? Allah awalipe kheri


❪[emoji411]❫ الجَـــ☟ـــوَاب : اﻟﻤﺸﺮﻭﻉ ﻟﻠﺼﺎﺋﻢ ﺃﻥ ﻳﺘﺴﺤﺮ ﻗﺒﻞ ﻃﻠﻮﻉ اﻟﻔﺠﺮ؛ ﻟﻤﺎ ﻓﻲ ﺫﻟﻚ ﻣﻦ اﻟﺘﻘﻮﻱ ﻋﻠﻰ اﻟﺼﻴﺎﻡ،


[emoji3514]Jawabu: jambo lililo wekewa sharia kwa mfungaji ni kula daku kabla ya kuchomoza kwa Al-fajiri kwa yale yaliyo kuwepo ndani yake katika uchamungu juu ya funga


ﻭﻗﺪ ﺣﺚ اﻟﻨﺒﻲ ﺻﻠﻰ اﻟﻠﻪ ﻋﻠﻴﻪ ﻭﺳﻠﻢ ﻋﻠﻰ ﺫﻟﻚ، ﻭﺑﻴﻦ ﺃﻥ ﻓﻲ اﻟﺴﺤﻮﺭ ﺑﺮﻛﺔ، ﻟﻜﻦ ﻟﻮ ﺻﺎﻡ اﻹﻧﺴﺎﻥ ﺑﺪﻭﻥ ﺳﺤﻮﺭ ﻓﺈﻥ ﺻﻴﺎﻣﻪ ﺻﺤﻴﺢ.


Kwa hakika amehimiza mtume (swallah llahu alayhi wasallam) juu ya kula daku, na akabainisha hakika ya kula daku kuna barka, lakini lau angefunga mtu bila ya kula daku basi hakika ya funga yake ni sahihi."


Fatwa ya lajnah ya kudumu


❪[emoji432]❫ المصْــــدَرُ: ❪فَتــَاوى اللجنَةِ الدَّائمَ, اﻟﻔﺘﻮﻯ ﺭﻗﻢ (14093❫.


══════ ❁✿❁ ══════

[emoji429] [emoji3578] Abou hudaa Al-jaziiriyyi حفظــــــــــه اللــــــــــه تعالــــــــــى ورعــــــــــاه[emoji433]

[emoji432]═══ AL-HUDAA DURUUSU ONLINE ═══[emoji432]




*[emoji668]Ili kupata faida zaidi ungana nasi katika channel

VUNA THAWABU KWA KUSAMBAZA KWA WENGINE[emoji108]

[emoji441]Kua muadilifu us'badili chochote[emoji95]
 
Je Na Wewe Unaepuka Kula Daku Ili Uonekane Mkakamavu kama John Cena?

Kuna watu hawapendi kabisa kula daku. Tena wengine wanajinadi kabisa hadharani kuwa mambo ya kuamka amka usiku mwingi kisa kula daku wao hawataki "tabu" hizo.

Kutokula daku kwa sababu ya kujiona unaweza kufunga bila kula daku au kwa sababu unajiona hauwez mambo ya kuamka amka usiku ili ule daku ni makosa kwa sababu mbili hizi:

(1)Kwanza mtume katuambia daku ina baraka. kwa hio mtu asiekula daku anakataa baraka.

(2)Mtume katuambia tofauti kati ya funga ya waislamu na wasiokuwa waislamu ni daku. Je muislamu anayefunga anataka funga yake isiwe tofauti na ya wale wasiokuwa waislamu?

Sababu nyingine nakupa bonus:
(3)Daku sio chakula cha saa nne, tano au sita usiku. Kutoka ktk sunna ya mtume tunaona daku inatakiwa kuliwa usiku wa mwisho haswa kati ya saa tisa usiku na saa kumi na moja alfajir ili mradi kabla ya wakati wa Alfajir haujaingia. Kuna wale wanaoona kula muda huo hawajazoea na hawataki hivyo wanakula saa nne au tano na wanajihesabu washapata daku. wengine hawali kabisa sababu wanadai hawawez kuamka usiku mwingi kula.
Wote hawa hawataki kutambua kwanza baraka za daku kama zilivyotajwa juu na pia wanapenda kuzipuuza fadhila kubwa ya mwezi wa Ramadhan ya kuamka usiku sana angalau kupata rakaa mbili za qiyam layl. Maana kama wasingetaka kuzipuuza basi hata kama wangeshindwa kuamka kula daku basi wangeamka kwa qiyaam layl. Na kama wangeamka kwa qiyam layl basi ndo tayar muda wa kula daku ndio huo huo.

NB: wale wanaosahau kula daku kwa bahati mbaya, kama kwa sababu ya kupitiliza au hali ya afya au ya kiuchumi hawahusiani na makosa haya. Hii inawahusu wasiotaka kula kwa makusudi tu kwa kuona daku si jambo la umuhimu.

Daku hata ya maji na tende au hata maji tu pekee ni bora kuliko kutotia chochote tumboni kwa kupuuza umuhimu wa daku.

Kutotaka kula daku kwa kujiona wewe ni kama John Cena, una NGUVU za kuweza kufunga bila kula daku ni ujinga. Kwa waislamu kufunga saumu sio mashindano ya nani anaweza kukaa na njaa muda mrefu zaidi. Bali ni nani anaweza kufanya ibada nyingi zaidi kwa unyenyekevu na uchaMungu na kujizuia na yaliyokatazwa na kukimbilia yaliyopendekezwa na mwisho kabisa ni kwa kufuata maelekezo ya mtume ya jinsi ya kufanya ibada hizo. Mfano ibada ya saum mtume kaelekeza watu wale daku.

Wabillahi Tawfiq.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…