Ramadhan Special Thread

ikiwa kama ndiyo kwanza unaingia katika huu uzi usisite kufungua na kuperuzi kuanzia page ya 1 kuna mambo mengi yenye faida yamo humu kuhusu mfungo wa ramadhani, ikiwa wayafahamu si vibaya ukajikumbusha, na mengine ya kheri yataletwa insha Allah kwani Mtume (s.a.w) anasema ''elimu ni mali ya muumini popote utakapoiona ufanye pupa kuichukua''

shukrani nyingi sana ziende kwa Hance Mtanashati kwa kulileta jambo hili la kheri Nyoka_mzee ukhuty everhurt SDG Abdul edwayne Dizkiz sungita cleverer Mndengestani mjingamimi emmyta Super women 2 alibakari Hashim bin Faustin dullynho arch67 dimaa Kanye2016 CleverKING Dr Simba uroto Arabian queen babu na mjukuu lucley Ibney momentoftruth Mwanakanenge mansakankanmusa leprincess shiite kikuna Kilemakyaaro THOMAS SANKARA forumyangu Joninho shaban mwiga byongo thatsit @wrong turn [USER=63847]mkomatembo jr boy lamalu Patience123 Kulupura mimisiowewe Khalidoun miseryman Rabii90 Angel Nylon Kadhi Mkuu 1 nasmapesa Omar Lugendo Mzigua wa kuchovya Bacyclerbacy Madam Mwajuma ISIS Mbulu nanawoo As Salafiyyu91 Alkanjir kichunjuu kichunjuu
Adharusi ngakotecture Mwifwa darcity [USER=62657]msabillah noiselessly hunter Chiwaso Mahmood [USER=187015]hyusuph khaliciouz MANI structuralist Pohamba shashashaa muhhidinramadhan Abdulwahid Polite kivyako IBRAHIM KAUKI Baraghash Ghazwat Khamisiya hosh kosh Tetty 2kimo Mwanamageuko [USER=313720]kezacute Big Dy ZAGANZA Abuu Saad Eliamini Saguda47 Nzory Mussa Penelope Latifah Ayoub MziziMkavu the horticulturist Maalim Shewedy kwinyo samira cute samira said
na wengineo wote tuendelee kuwa pamoja hapa kwani dini ni nasaha
'' ...na saidianeni katika wema na uchamungu wala msisaidiane katika dhambi na uadui...(Q.5:2)
ALLAH KWA BARAKA YA RAMADHANI HII PENYE UZITO ATUJALIE TAHFIF, ATULIPE YALIYO YA KHERI DUNIANI NA AKHERA (AMEEN)[/USER][/USER][/USER][/USER]
 
Na mie pia nipo mkuu..siachi hata kurasa moja
 
Asante mkuu
Labla nijazie tu kido KIBABA KIMOJA=600gram

★Pili kuhusu mama mja mzito Kama atashauriwa dactari kutokana na Afya yake ,huyu ataruhusiwa kula mchana wa ramadhani asiwe tena anakaa nje ndio anakula akae ndani na atalipa baada ya kuisha ramadhani.
Mama mjamzito akiwa hakufunga labla kwa kuhufia afya ya mtoto wake ,huyu atalipa kufunga na pia hatawarisha masikini yaani atatoa kibaba kimoja =600gm, kwahio huyu atafanya yote mawili kwa pamoja.

★Kwa wale wanaodaiwa jamani mulipe kabla mwezi ujaanza
Kwa wale dada zetu mkiwa ktk siku zenu sio tena kwakua mmeruhusiwa kula basi tena unakaa nje unapigilia msosi jifiche sio tena kilamtu ajue upo katika sikuzako.
★Kuna wengine hasa mama zetu utawakuta wapo ktk mwezi lakini hali mchana hii hairuhusiwi utakuwa unakiuka amri ya ALLAH SUB HANA WA'ALA unajishindisha na njaa pasi na sababu.Muhimu kujihifazi wakati wa kula sio tena kila mtu akuone tuwe wasiri katika kula mchana wa ramadhani.
 
Jazaaka llahu lkhayr
 
NI JUU YA NANI INAMPASA SWAUM YA RAMADHAN??








JAWABU:




Ni wajibu kufunga ramadhani kwa kila Muislam Mukallaf kwa wanaume na wanawake, na inapendeza kwa aliyefikia umri wa miaka saba na kuendelea na akaiweza kuifunga wanaume na wanawake.

Na itawapasa Mawalii wa vijana hao wawaamrishe kufunga wakiwa na uwezo kama vile wanavyowaamrisha swala.

na asili ya jambo hili ni kauli ya Allaah-'azza wajalla- :

"Enyi ambao mmeamini imefaradhishiwa juu yenu swaum kama ilivyofaradhishwa kwa waliotangulia kabla yenu ili mpate kumcha. Ni siku chache za kuhesabika, basi yeyote miongoni mwenu atakayekuwa mgonjwa au kuwa safarini basi ni hesabu za deni atakazolipa siku nyingine" al-baqarah 183-184.

mpaka aliposema:

"Mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imeshushwa Qur'an, Uongofu kwaajili ya watu na ubainisho unaotokamana Uongofu na ni kitenganishi (kinachotenganisha baina ya haki na batili). Basi yeyote ambaye ataingiliwa na mwezi basi aufunge, na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi ni hesabu za deni atakazozifunga siku nyingine" al-baqarah 185.


na kauli ya Mtume (swalla Llaahu 'alayhi wasallam):

"Umejengwa Uislam juu ya nguzo tano:

• kushahadia kwamba hakuna mola apasayekuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.

• kusimamisha swala.

• kutoa zaka.

• kufunga Ramadhan.

• kuhiji kwenye nyumba ya Allaah." imeafikiwa juu ya usahihi wake kutoka katika hadhithi ya Ibn 'Umar (Allaah awaridhie).
 
MFUNGO UNAANZA LINI NA MIMI NIJITAHIDI KUFUNGA,,
NAWATAKIA MFUNGO MWEMA

SWALI;KWA MUME NA MKE WANOISHI PAMOJA BILA NDOA KWENYE MFUNGO HAPO INAKUAJE
Hawaruhusiwi kushiriki tendo la ndoa mchana ,wanaruhusiwa jioni baada ya kufungulia.
 
MFUNGO UNAANZA LINI NA MIMI NIJITAHIDI KUFUNGA,,
NAWATAKIA MFUNGO MWEMA

SWALI;KWA MUME NA MKE WANOISHI PAMOJA BILA NDOA KWENYE MFUNGO HAPO INAKUAJE
Hamna mme na mke bila ndoa katika Uislam, hao ni mahawara na wanafanya zinaa, zinaa ni uchafu ktk Uislam, km alivyosema Allah fil Qur'anil kariim kwamba;
"Na msiikurubie zinaa hakika zinaa ni uchafu na ni dhambi kubwa"
Ili ufunge unatakiwa kuwa tohara, na hao watu wawili hawako tohara inaamaana hawana funga wanashinda na njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…