Ramadhan Special Thread

Allahuma Aamin
 
Hakika Allah (swt) amewaekea wazi njia ya haki na akaiangaza ima ushikamane na maovu au ushikamane na mema, chukueni zawadi kutoka katika masiku yenye kumalizika kwa ajili ya masiku yasiokwisha, kwani nyinyi ni kama wasafiri waliosimama hawajui muda gani wataamrishwa kutembea, anafanya nini duniani yule alieumbwa kwa ajili ya akhera, anaifanyia nini mali yule ambae anajua muda mfupi atanyanganywa.(Imam Ally a.s katika Nahjulbalagh hutba no 157)
 
Jana magharibi ilinikuta Sinza, basi swala na futari hadi narudi kwangu Kigamboni inakaribia saa nne usiku. Hivyo nimegundua ile futari ninayowaalika itakuwa mzigo(takliifu) kwa wengi. Hivyo nimeiondoa na nashauri kwa mwenye wasaa tuandae kwa mitaa yetu, Futari isichukue muda mwingi ili tuwahi ibada zingine
 
URADI NI NINI ?
 
ENYI WANAWAKE SOMENI UJUMBE HUU,NA MUMCHE ALLAH, MAASWI YATAKAYOWATIA WANAWAKE MOTONI NI HAYA HAPA:

Bibi Aishah (Radhiallahu Anha) alimuuliza bwana Mtume (S.A.W) je kuna mtu yoyote miongoni mwa wafuasi wako atayeingiaJannah bila hesabu. Ndio akajibu Mtume (S. A. W ) mtu ambaye daima analia kwa dhambi zake
Siku moja Bibi Fatma Radhi Allah An-ha alikwenda
kwa Mtume (S.W.W) akamkuta analia sana
Bibi Fatma akamuliza nini kinachokuliza ya Rasulla
Allah ??

Akajibu:

Jinsi nilivowaona Wanawake wakipewa adhabu mbali
mbali Motoni
Bibi Fatma akamuliza:
Ni Adhabu gani hizo ya Rasulla Allah ??
Mtume Muhammad (S.A.W) akajibu:-

1. Mwanamke katundikwa kwa nywele zake na huku
ubongo wake na mikono yake inatolewa kwa
nyuma ya mgongo wake na huku anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI MWANAMKE ANAETEMBEA KICHWA WAZI.

2. Mwanamke kafungwa mikono yake na miguu
yake juu ya utosi wake huku kaachiwa Joka na Nge
wakimdona.

HUYU NI MWANAMKE ANAETOKA BILA RUHUSA YA MUMEWE.

3. Katundikwa kwa ulimi wake umevutwa hadi
dhiraa 70 na anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI YULE ALIYEMUUDHI MUMEWE HADI AKAKASIRIKA.

4. Anakula mwili wake na huku kila akila nyama inajirud upya na huku anamiminiwa moto wa lami.

HUYU NI YULE ALIYEKUWA ANAJIPAMBA NA ANADHIHIRISHA PAMBO LAKE.

5. Anakata mwili wake kwa Mikasi ya moto km
anaekata kitambaa.

HUYU NI MWANAMKE ALIYEKUWA AKIPENDA KUTEMBEA HUKU AMEVAA NGUO ZA KUBANA ZINAZO ONESHA FIGER YA MWILI WAKE.

6. Mwengine uso wake mweusi sana huku anakula
tumbo lake na mikono yake.

HUYU NI YULE ALIYEKUWA ANAFITINISHA.

7. Na wengine wametiwa ndani ya masanduku ya Moto na Nge wakiwatafuna miili yao.

HAWA NI WANAWAKE WANAOWABANDIKA WAUME ZAO WATOTO WASIO KUWA WAO.

EWE MWANAMKE JIEPUSHE NA ADHABU HIZO KWA
HAKIKA NI ADHABU KALI.

Share na rafiki zako ili mawaidha yawafikie wengi....

HAKIKA UKUMBUSHO UTAWAFAA WENYE KUAMINI
 
TUOGOPE KUSENGENYA JAMANI MUNGU HAPENDI

Ndugu zangu katika imani, hakuna jambo jipya katika dini yetu hii kila kitu kilishawekwa wazi
ila ni vizuri tukumbushane kila wakati na tusichoke kwa hilo kwani :
''Hakuwa binnadamu isipokuwa ni kiumbe mwenye kusahau sahau''

Kusengenya ni miongoni mwa mambo yaliokatazwa sana na M/Mungu kiasi kwamba Amekufananisha na kula nyama ya maiti,na hii ni miongoni mwa madhambi ambayo tunayafanya kila siku kwa kujua ama kutokujua,basi nakukumbusha tena ndugu yangu tuwe makini na ndimi zetu

Kusengenya ni kumtaja mtu kwa jambo asilolipenda. Mtume mtukufu (s.a.w.) anasema: “Kusengenya ni kumtaja ndugu yako kwa jambo analolichukia. Ikiwa jambo hilo analo huko ni kusengenya na ikiwa hana basi utakuwa unasema uongo.”.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemfananisha mwenye kusengenywa na maiti kwa vile anakuwa hayupo na akaifananisha heshima yake na nyama yake na kumtaja kwa uovu ndiyo kama unakula nyama yake. hivyo kama tunaona kinyaa kula nyama ya maiti basi pia tuone kinyaa kumsengenya asiyekuwepo.

Na Mwenyezi Mungu hasamehi kusengenya mpaka asamehe aliyesengenywa
Basi ikiwa umemsengenya mtu na mauti yakakuta bila kumuomba msamaha basi ujue utakuwa na deni siku ya kiyama na viungo vyako vitakuwa shahidi siku hiyo

Na kwenye kusengenya yule anayesengenya na msikilizaji wote wana dhambi
Nawausia na kujiusia nafsi yangu tukae mbali na maasi na tuikumbuke siku ya malipo

''Yeyote yule anaefanya wema mfano wa uzito wa sisimizi siku hiyo atauona wema wake
na yeyote yule anaefanya uovu mfano wa uzito wa sisimizi siku hiyo atauona uovu wake'

 
Hivi vilema wote ni waislam kwel

Hapana, sidhani kama ni kweli vilema wote ni waislam aidha kama wataka kufaham zaidi ni vyema ukaenda kwa Kakobe au wachungaji wowote wanaowaombea vilema na viwete wakasimama uwaulize kuwa je, wale ni waislam watakupa jibu sahihi kama vilema wote ni waislam au laa.

Shukran laka jaziylah. Marhabanbik.
 
mie nimeshindwa hata kumuelewa
 
Bihusnil khaatimah ya Allah!! Astaghfirullah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…