Ramadhan Special Thread

Ukiangalia mwisho wa aya hapo neno KARIYM limetanguliwa na neno KITABU(jina)kwa maana ya hapo utafasiri kwamba kitabu ni MTENDA (فاعل)?

Hapo Kitabu anakuwa (نائب فاعل ) na huyo (كريم) anakuwa ni (صفة). Ndio maana ukiisoma aya inakuwa imeishia hapo,na inakuwa aya hiyo ya 29 ni habari wa (ان) kwa aya inayofata ya 30.

Sababu naona unababatiza maana,naomba uniambie ni wakati gani viwili hivyo vinakiwa (مفعول) ?

Hapo kuna sehemu ndogo sana umechemka,kuna vitu viwili unatakiwa utofautishe kati ya فعل متعدي na فعل الازم sijui kama umeona hilo.

Hivi ni kweli tamko (كتاب كريم) ni sawa na tamko (رمضان كريم) tamko la pili linaingia kwenye فعل متعدي kama vile ilivyo kwa mfano huu (رجل كريم و مكرم) kwa maana linahitaji kitu kukamilisha maana iliyo kusudiwa na sentensi (رمضان كريم) hapo Ramadhaan anakuwa ni كريم kwa nafsi yake mwenyewe wakati ukarimu ni wa Allah,mtume au waumini.

Nipo ....
 

كريم inageukaje hapo kuwa mtendwa wakati tamko hilo ni sifa ya كتاب ? Kitabu hapo ni نائب فاعل .

Hichi kiarabu unachokiandika hapa na kukibabadua ni kiarabu cha wapi ?

Au ushawahi kusoma kitabu chochote cha "اعراب القرآن " ukaona wameelezea kama unavyoelezea hapo ?
 
Katika hizo aya ulizonukuu tamko كريم limesimama kama sifa ya hivyo vilivyozungumziwa.

Soma vitabu vinavyoelezea Irabu ya Qur'aan utaona na kupata faida.
 
NAJIBU MASWALI YOTE YANAYOHUSU SWAUM YA RAMADHAN NA IBADA ZOTE ZINAZOAMBATANA NAZO...KABLA NA BAADA YA RAMADHAN...KARIBUNI...
Naomba kuuliza inakuwaje mnasema mnafunga, wakati usiku mnakula Mara mbili ile kufturu na daku ,

Je huko sio kubadili ratiba ya chakula, badala ya mchana mnaipeleka usiku?
 
Mkuu ebu kuwa siriaz kwanza..

Kwani نائب الفاعل sio مفعول به?

naibu wa mtendaj sio mtendwaji?
Hata kama utasema ni naibu wa mtenda bado haipingi kusema kwamba huyo ni mtendwa.

Bali anaitwa nibu wa mtenda kwa kule kupata kwake raf'u مرفوع

Mfano katika aya..

قتل أصحاب الأخدود

[ AL - BURUUJ - 4 ]
Wameangamizwa watu wa makhandaki

Ukiangalia katika aya neno الأخدود limekuwa مرفوع (lina dhwamma)wakati hao ni watendwaji ambao walitakiwa wawe na nasbu yaani wawe منصوب (wapate fat'ha mwishoni).

Lakini hapo wamekuwa na dhwamma kwa sababu فاعل مجهوووووور (mtenda hafahamiki) hivyo wao wanakuwa ni wasaidizi wa mtendaji wanakaa badala ya mtendaji.

Lakini sasa hao watu wa makhandani kiuhalisia unawatoa katika kutendwa ati kwa kuwa wamekuwa ni نئب الفاعل (wasaidizi wa mtendaji)?

Sasa kitu kuwa naibu faail hakimtoi kwamba ati hajatendwa,katendwa lakini mtendaji haafahamiki na kawaida ya mtendaji anapata dhwamma mwishoni lakini kwa kuwa hayupo basi anapata dhwamma aliyemtenda.

Sasa sijui unachokipinga wewe kupitia nibu faail juu ya neno kariym ni kipi hapo mkuu zurrrrrrrri
 
Akhuy

Hii mada si bora kuendelea nayo

Tulete faida za Funga kwa watu
Ni lipi la kufanya na lipi la kuwacha

Lau tutafungua mlango wa kuminyana kielimu,halafu wanaoelewa ni wachache,tutakuwa watu wa ajabu sana

Siona kama kuna haja na hili kwasasa

Shukran
Allah akubaarik sana popote ulipo
 
Naomba kuuliza inakuwaje mnasema mnafunga, wakati usiku mnakula Mara mbili ile kufturu na daku ,

Je huko sio kubadili ratiba ya chakula, badala ya mchana mnaipeleka usiku?
Kwa kawaida nyakati za mchana ndio nyakati haswaa za kupata chakula.yaani milo mikubwa yote hulika nyakati za mchana(asbuhi na mchana)na mmoja jioni.

Au wewe ulihisi funga ni jambo zito saaanaaaaaa kwamba tunakaa masaa24 na njaa?

Sasa huko kungekuwa ni kutiliwa ugumu.
Ukisema tunabadili ratiba huwenda ukawa sahihi lakini ndo hiyo tunaita funga kwa sababu unajizuia kwa muda ambao usile na unakula kwa muda ambao umeruhusiwa.

Au wewe utata wako uko wapi?
 
Nam akhy sikuwa na lengo la kuendelea nalo lakini kuna bwana mkubwa zurri ambae anakataza mambo pasi na kuwa na vikatazio madhubuti.

Na watu wanataka ukiwakataza jambo uwe na hoja madhubuti za kukataza hasa sisi waislamu wa kawaida sio kkubabaisha tu,inakuwa hatuelewi kwa kweli.ndio maana na mimi nikaandika hayo.
 
Shukran Akhuy

Nataraji ameelewa
 
Utashangaa wengi ya wanaofunga Ramadhani ni wauza unga, kuna connection gani hapa?
Hakuna connection.

Kwa sababu funga ni wajibu kwa kila muislamu.
Hata kama unauza unga haina maana uwajibu huo umeondoka.
Utatakiwa kufunga na dhambi za kuuza unga unapata.

Ukiacha kufunga unapata dhambi ya kuacha wajibu na huku ukiuza unga unapata dhambi ya kuuza unga.

Hivyo ukifunga unapunguza dhambi unabakiwa na dhambi moja ya kuuza unga.

Hakuna connection kama muuza unga anafunga hatuwezi kumkataza kufunga ati kwa kuwa anauza unga,bali ataambiwa afunge na aendelee lakini aache kuuza unga.
 

Ni kweli نائب فاعل ni مفعول به . Kama ilivyoelezwa hapa :

يقع نائب الفاعل بعد الفعل غير المعروف فاعله، ويصبح المفعول به هو الذي يقوم مقام الفاعل ويسمى نائب الفاعل، والفعل المبني للمجهول إذا كان فعل ماضٍ يكون أوله مضموماً والحرف ما قبل الأخير مكسوراً، وإذا كان مضارعاً يُضمّ أوله ويُحرّك الحرف ما قبل الأخير بالفتحة، ومثال بسيط على ذلك: الجملة الأولى :كَسرَتْ ربابٌ القلمَ.( مبني للمعلوم).


Hapa nakiri nilipitiwa. Ila hili bado haliruhusu au kufanya رمضان كريم kusihi,japokuwa msemo kilugha uko sawa,ila unaonyesha ya kuwa رمضان yenyewe ndio ina sifa ya كريم jambo ambalo si sahihi,kwani kwani sifa ya ukarimu haiwezi kuwa kwa mwezi bali sifa ya ukarimu unaikuta kwa Allah,Mtume na waumini.
 

 
Nimekutolea aya ambazo zimetumia neno kariym nazinukuu tena..

فالذين آمنوا وعملوا الصالحات لهم مغفرة ورزق كريم

[ AL -HAJJ - 50 ]
Basi walio amini na wakatenda mema watapata maghfira na riziki za ukarimu.

Mwisho wa aya kuna neno kariymu na limetanguliwa na jina la rizqi.hapo aya imehusisha rizqi na ukarimu.

Sasa hapo mbona imetajwa rizqi ambayo ni kariym je rizki mbona sio Allah,wala mtume wala waumini na imepewa sifa ya ukarimu?

إنه لقرآن كريم

[ AL -WAAQIA'H - 77 ]
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,

Qurani ni Allah?
Qurani ni mtume?
Qurani ni waumini?
Mbona Neno Qurani limepewa sifa ya ukarimu kama ukarimu haupaswi ila kwa Allah,mtume na Waumini pekee?

قالت يا أيها الملأ إني ألقي إلي كتاب كريم

[ AN-NAML - 29 ]
(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.

Hapo tumeona NENO BARUA LIMESIFIWA KWA NENO KARIYM.
Je aya imekosea kwa kuwa neno kariym ni sifa ya Allah,mtume au waumini pekee?

Lughaa inapoikhalif Qurani basi tunaacha lugha tunaifata Qurani imeweka msingi gani.

Qurani mara nyingi imetumia neno kariym kama sifa sehemu ambazo wala sio Allah,wala sio Mtume wala sio waumini.kama nilivyotangulia kutaka hapo juu.

Kariym inategemea inakuna vipi.ikija na kitu chenye sifa ya kutenda basi itakuwa na maana ya mtenda.

Ikoja na kitu chenye sifa ya mtendwa(hakitendi) basi itatafsiriwa kwa maaana ya mtendwa.

Mfano
قالت يا أيها الملأ إني ألقي إلي كتاب كريم

[ AN-NAML - 29 ]
(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.

Barua metendwa ndo ikawa barua,lakini ikapewa sifa ya KARIYM kwa maana hapo maana yake ni BARUA ILIYOFANYWA KUWA TUKUFU.

Mbona Qurani imwtumia neno kariym kwa asiyekuwa Allah wala Mtume wala Waumini?


 
Assalam aleykm warahmatullah wabatakatul! Naomba kujuzwa juu ya ulaj/ kutokula daku.Je nikiacha kula daku funga yangu itaswih?


Usiwe mwehu kijana, hakuna aliyekukataza kula....kufunga si lazima.....usipende kuendekeza hizi dini za kuletewa na maboti. jiulize, uache kula ili iweje, inakuja kichwani mwako kweli? Amini Mungu wako tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…