Ramadhan Special Thread

Hapa tunabishania nini mbona hoja niliijibu kwa ushahid na ndo nilipokugeuzia swali wewe tena unijibu
 
mfunge kwa kuonekana kwa mwezi kwa sababu hii mipaka ya nchi ya tanzania haikuwepo wakat wa mtume
 
S
Sio sio kweli kwamba wanaangalia mwezi kwa vifaa na wanawazuoni pia wanakataa kuuungalia mwezi kwa vifaa na tunazo fatuaa za wanazuoni wa kisaudia wanakataa kuangalia mwezi kwa vifaa na hilo la kulipa fidia pia sio la kweli nakutumia na uthibitisho na hivyo vifaa unavyosema ni vifaa gani
 
Kwa hiyo na wao pia walitofautian kufunga kwa sababu walitofautiana hiyo miji wakati wa mtume
Isome vizuri hiyo Hadith ya Kureib ya "fungeni na fungueni kwa kuoona mwezi". Utakutana na fatw'a ya Ibn Abbas(Swahaba mkubwa sana huyu) akimfafanulia na kumtaka Kureib aliyetoka safarini Shamu afuate mwezi wa Madina. Suala sio "kuonekana" bali "kuuona". Mtume SAW alikua ni fasaha wa lugha na kila neno lake moja lina maana
 
Wewe umeielewa vipi hiyo hadith
 
Dada yangu ukhuty they uses telescope belive na sio local kama tufanyavyo sisi huku nyumbani. Kwa siku waliotangaza mwezi ulikuwa bafo mchanga kabisa sio wa kuonekana. Wanaogopa kuaibika pia kwa vile njia wanayotumia sio sahihi na hata hivyo tunatakiwa tuangalie mwezi localy. Wanahofia pia kupata aibu maana shaaban ingekuwa na siku 31 njia wanayoitumia imewapeleka chaka kiasi kwamba ikabidi watangaze mwezi kilazima ili kulinda aibu zao.

"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 


"Fᵒˡˡᵒʷ ᵉˣᶜᵉˡˡᵉⁿᶜᵉ ˢᵘᶜᶜᵉˢˢ ʷⁱˡˡ ᶜʰᵃˢᵉ ᵖᵃⁿᵗˢ ᵈᵒʷN"
 
Wasafiri watakaopenda kuswali waje kuswalia hapo Msata Hotel halafu mnawauzia futari kwa sh. 3000,

Kama sijaelewa nieleweshe.

Corona Virus: Stay Home the only Medicine found.
 
Assalam aleykm warahmatullah wabatakatul! Naomba kujuzwa juu ya ulaj/ kutokula daku.Je nikiacha kula daku funga yangu itaswih?
Ukiacha kula daku funga yako itasihi,kwa kweli ukila daku ukashiba siku ya pili saumu inakuwa Kali Sana.

Daku Suri Ni kula tende na masiwa,usisahau kunywa maji mengi..
 
Madai yyt ya dini yanatakiwa yaongozwe na dalili ima ktk qur an au sunna achana na habari za wasaudia kwa sababu wao sio rejea ya dini rejea za dini zinafahamika.
Wakati wa mtume s a w iliwahi kutokea kukhitilafiana kufunga?
Tuna ushahidi kuwa mtume s a w alifunga kwa kuuona mwezi pia alifunga kwa kupewa taarifa za kuonekana kwa mwezi .
 
Ndugu zangu waislamu

Mwezi mtukufu umeshaingia na utaondoka, basi tusiwe tunafunga kwa mazoea ila kwa kutaka radhi za Mwenyezi Mungu

Mtume saw sidhani kama alifunga ramadhan zaidi ya tano akiwa na maswahaba lakini kila ilipofika ramadhan kulikuwa na mabadiliko makubwa katika imani kwa maswahaba na imani na uchamungu ulikuwa unaongezeka

Sisi waislamu tokea tuanze kufunga wengi wetu tumeshafunga zaidi ya ramadhan ishirin, je ramadhan zinatusaidia kubadilika??yatakiwa tujitafakari na tuweke azima tumuombe Mungu atuzidishie Imani na uchamungu isije kuwa ramadhan zinakuja na kuondoka haziachi taathira zozote kwetu sisi

Yatakiwa tujitathimini ndugu zangu lengo la kufunga ni kutusaidia tuwe wachamungu

Tumuombe Mungu atuongeze katika kila lililo na heri la kumpendeza yeye🙏🙏
 
Wewe umeielewa vipi hiyo hadith
Jamhuri moja inasema wakati wa Mtume SAW maendeleo ya Sayansi hayakua makubwa. Ila wakati huu **** mawasiliano ya simu Radio TV n.k na ki jiografia hakuna nchi inayoipita nchi nyingine kwa zaidi ya saa 12. Kwa hiyo kimsingi inafika wakati dunia nzima inakua katika siku moja kwa hiyo lazima kutumia mwezi mmoja muandamo

Jamhuri ya pili inasema Mtume SAW alikua anajua kua miji tofauti ina tofauti za kijiografia pia. Ndio maana kwa mfano swala ya magharibi ya Dar haiswaliwi kwa wakati mmoja na Kigoma au Makka hata kama wote itakua ni saa kumi na mbili na nusu. Maana yake. Mungu ana alama zake kama jua na mwezi kwa hiyo pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni wajibu wetu kurekebisha vyombo vyetu kama saa na satelait ili kufuata alama za Mwenyezi Mungu na Sio alama za Mungu kama jua na mwezi zifuate vyombo vyetu kama saa nk

Hapo mimi nafuata Jamhuri ya pili ya wanazuoni
 
kuacha sala haibatilishi funga.over

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuacha sala haibatilishi funga.over

Sent using Jamii Forums mobile app
Funga yako itakuwa na mashaka

Mtume saw anasema swala ndiyo nguzo ya dini. Nadhani we mwenyew tafakari hapo aliposema ni nguzo ina maana ukiicha sala na wew kama ni muislamu basi imani yako haipo sawa,

swala sio jambo la ridhaa ni amri kwa waumini, na siku ya kiyama ndio amali ya kwanza itakayoanza kuhesabiwa

kama mtu anafunga na haswali ajue kwamba anapata faida tu za kiafya, ila hana faida anayopata kiimani kwani huyo bado hajawa muumini,

huyo anaefunga bila kuswali hana tofauti na mtu ambae hana dini akaamua tu kufunga ili aone funga ikoje
 
In ShaaAllah , Ameen. , na tusiwasahau masheikh wetu waliopo Segerea.
katika wale masheikh yupo m1 anaitwa Msellem Aly... ni miongon mwa wanadam ninaowahusudu sana kutokana na ufundishaj wake ni jins anavyoitumia elim yake kunufaisha wengne..

Allah amjaalie kila lenye kher duniani na Akhera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…