Ramadhan Special Thread

Nani Anawajibika Kufunga


Maulamaa wamekubaliana kufunga ni wajibu kwa mwenye akili timamu, Baleghe, mwenye afya na mkazi wa mji. Tukiongezea wanawake waliotwaharika na hedhi na nifasi.

Kwa wale ambao Swawm si wajibu juu yao ni wale ambao hawana akili timamu, hawajabaleghe.


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:

“Kalamu (kurekodiwa ‘amali) imeinuliwa (hairekodi) kwa watu watatu: anayepatwa na usingizi mpaka aamke, mtoto mpaka afike umri wa kubaleghe, na aliorukwa na akili mpaka atakapopata akili timamu.”
[Hadiyth imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jami´, na. 3513 na Imerikodiwa na Abu Daawuwd].


Ama kwa wale wasioweza kufunga ni kutokamana na maneno Yake Allaah:

ﻓَﻤَﻦ ﺷَﻬِﺪَ ﻣِﻨﻜُﻢُ ﺍﻟﺸَّﻬْﺮَ ﻓَﻠْﻴَﺼُﻤْﻪُ ﻭَﻣَﻦ ﻛَﺎﻥَ ﻣَﺮِﻳﻀًﺎ ﺃَﻭْ ﻋَﻠَﻰ ﺳَﻔَﺮٍ ﻓَﻌِﺪَّﺓٌ ﻣِّﻦْ ﺃَﻳَّﺎﻡٍ ﺃُﺧَﺮَ


“Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini (akafunga baadhi ya siku); basi (akamilishe) idadi (ya siku anazotakiwa kufunga) katika siku nyinginezo.

” [Suwratul-Baqarah 02: 184].


Ikiwa mgonjwa au msafiri atafunga basi inawatosheleza, ama wakichukua ruhsa ya kula hapo wameondolewa uzito. Ama wakiamua kufunga kwa kuwa wanataka kufunga hapo pia wako sawa.
 
Asalam alyekum Ndugu zangu katika imani, Mwezi mtukufu wa ramadhani ni mwezi wa toba kwetu waislam hivyo tunatakiwa tuzidishe unyenyekevu kwa Allah na tuombe rehma na maghufira kwa mole wetu mlezi wa viumbe vyote.Ndugu zangu waislam tusisahau kutoa sadaka na zakka ili tupate thawabu.Tusimame sana usiku kwa sasa na dua pia tusome sana Quran tukufu.Eeh mola wetu tunaomba utufanyie wepesi
 
Jazakallah kheir
 
Ni kupi bora: Kutofunga au Kufunga?


Ikiwa mgonjwa au msafiri hawatoona tabu yoyote katika kufunga, basi kufunga kunapendekezwa. Ama wakikhofia kupata tabu kutokamana na kufunga, basi hapo kutofunga kunapendekezwa.

Abu Sa’iyd al-Khudriy ameelezea:

‘’Tulikuwa vitani na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) wakati wa Ramadhaan. Wengine katika sisi walikuwa wamefunga na wengine walivunja Swawm zao.

Wale waliofunga hawakuwaona waliovunja Swawm zao kuwa wako makosani na waliokula pia hawakuwaona waliofunga kuwa wako na makosa. Waliona wenye uwezo wa kufunga (walifunga) na hilo ni jambo zuri. Na ambao hawakuweza kufunga walivunja Swawm zao kwa udhaifu wa kufunga (hawakufunga) na hili pia ni jambo zuri.’

’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-At-Tirmidhiy na. 574. Pia imerikodiwa na Imaam Muslim].


Ushahidi wa wanawake wasio Twahara kuwa hawafungi ni Hadiyth ya Abu Sa´iyd ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) amesema:


’’Je, si kwa kesi kwamba anapopatwa na damu yake ya mwezi, haswali wala hafungi? huo ni upungufu katika Dini yake.

’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy, katika Mukhtaswar Swahiyh Al-Al-Bukhaariy na. 951. Imerikodiwa na Imaam Al-Al-Bukhaariy].


Ikiwa mwanamke asiyo Twahara atafunga basi swawm yake haikubaliki kwani katika masharti ya kukubalika swawm ya mwanamke ni awe katika Twahara. Mwanamke pia itamlazimu alipe siku alizokosa kufunga. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:


“Tulipokuwa tukipatwa na siku zetu za ada wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa Sallam) tuliamrishwa kulipa Swawm za siku tuliokosa kufunga na hatukuamrishwa kulipa Swalah tulizokosa.

’’ [Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Sunan At-Tirmidhiy na.630. Imerikodiwa na Imaam Muslim, Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-An-Nasaaiy].


itaendelea....!
 
Ni kweli mkuu hapo ndipo kuna kuwaga na mtafaruku hapo
ila kikubwa hitirafu zipo zilikuwepo na zitakuwepo
Na ktk hitirafu kuna zinazo kubalika na zisizo kubalika.mf:Hitirafu isio kubalika kuna watu wana dai Mitume inaendelea ,Baada ya Muhammadi swalla allah alayhi wasallam alikuja Mwingine (Mirriza Ghuram Ahmedy) n.k. hizi hazikubaliki

Hitirafu ya Mwezi ni hitirafu inayo kubalika kikubwa yapaswa kufunga kutokana na ulivyo amina sio kwa kumuhufia mtu fulani au nyumbani wao wanaanzaga basi na mm nitaanza kwa kuhufia nyumbani.au sianzi kwa kuhufia nyumbani au mtu fulani .Siai Tunafunga kwa ajili ya Allah .
 
ni kweli kabisa na ndomana tunasisitizwa tusome ili kuijua dini yetu ,maana ukisoma hutoburuzwa wala hutofauta mkumbo,
maana dini haiendeshwi kwa rai za mtu au kufata mkumbo ,

Unaposoma basi unajua unachokisimamia

Kukhtilafiana kupo na kulikuwepo ila hakumaanishi tufarakane
 
Hivi Ramadhan waislamu wanafunga au wanabadili muda wa kula? Na je mnaposema Ramadhan ni mwezi wa kutenda mema je miezi mingine ni ya kutenda mambaya? Asalam Allykum
Wanafunga...
Kubadili mda ina maana tungekua tunakunywa chai saa moja usiku,,lunch saa saba usiku afu dinner sa 12 asubuhi.
Tunafunga na kufungua kwa kuzama na kuchomoza kwa jua?!

Miezi mingine sio ya kutenda mabaya,ila mwezi Wa ramadhan matendo mema yanalipwa Mara kumi zaidi kulinganisha na miezi mingine.

Una swali lingine umeacha kiporo tukujibu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…