[emoji617] MATENDO KATIKA KUMI LA MWISHO
❁::العمـل فِي العشـر الأوَاخِرِ مِنْ رَمَضـَانَ::❁
❍ عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ : «كَانَ النَّبِيُّ ﷺ إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ شَدَّ مِئْزَرَهُ وَأَحْيَا لَيْلَهُ وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ»
"Imepokelewa kutoka kwa Mama 'Aaishah (Allaah amridhie) , Amesema:
"Alikuwa Mtume (swalla Llaahu 'alayhi wasallam) linapoingia kumi la mwisho , hukaza kibwebwe chake (anaacha jimai) , na kuuhuyisha usiku wake na huwaamsha watu wake".
[ صحيح البخاري - رقم : (2024)]
❍ وقَالَتْ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا :
Na Amesema (Allaah amridhie):
«كَانَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ يَجْتَهِدُ فِي الْعَشْرِ الْأَوَاخِرِ مَا لَا يَجْتَهِدُ فِي غَيْرِهِ»
"Alikuwa Mtume wa Allaah (swalla Llaahu 'alayhi wasallam) akijipinda katika kumi la mwisho jitihada ambayo haionekani katika siku zingine".
[صحيح مسلم رقم : (1175)]
❍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، عَنِ النَّبِيِّ ﷺ ، قَالَ :
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) , kutoka kwa Mtume (swalla Llaahu 'alayhi wasallam) amesema:
"Yeyote atakayesimama usiku wa cheo (Laylatul-Qadr) kwa Iymaan na kutaraji malipo (kutoka kwa Allaah) atasamehewa yaliyotangulia katika madhambi yake".
« مَنْ قَامَ لَيْلَةَ الْقَدْرِ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»
[ متفق عليه :2014-760 ]
❍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ :
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Allaah amridhie) amesema:
قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ :
Amesema Mtume wa Allaah (swalla Llaahu 'alayhi wasallam):
« ،،، لِلَّهِ فِيهِ لَيْلَةٌ خَيْرٌ مِنْ أَلْفِ شَهْرٍ، مَنْ حُرِمَ خَيْرَهَا فَقَدْ حُرِمَ »
"Hakika Allaah ana usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu moja , atakayenyimwa kheri za usiku huo basi huyo ndiye aliyenyimwa (fanaka na kheri nyingi)".
[ صححه الألباني في صحيح النسائي رقم :2105 ]
❍ عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ قَالَ : « تَحَرَّوْا لَيْلَةَ الْقَدْرِ فِي الْوِتْرِ مِنَ الْعَشْرِ الْأَوَاخِرِ مِنْ رَمَضَانَ »
Imepokelewa kutoka kwa 'Aaishah (Allaah amridhie) , kwamba hakika Mtume wa Allaah (swalla Llaahu 'alayhi wasallam) amesema:
"UtafutUtafuteni usiku wa cheo katika siku za witri katika kumi la mwisho la Ramadhani ".
صحيح البخاري رقم 2017 ]
❍ عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ : قُلْتُ : يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ عَلِمْتُ أَيُّ لَيْلَةٍ لَيْلَةُ الْقَدْرِ، مَا أَقُولُ
فِيهَا ؟ قَالَ ﷺ قُولِي : « اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ ؛ فَاعْفُ عَنِّي»
Imepokelewa kutoka kwa 'Aaishah (Allaah amridhie) , amesema:
Nilisema kumuuliza Mtume (swalla Llaahu 'alayhi wasallam) , Ewe Mtume wa Allaah! Unaonaje lau nikijua kuwa usiku fulani ndio usiku wa cheo niyapi yakuyasema humo?
Akajibu Mtume (swalla Llaahu 'alayhi wasallam):
" Sema : Ewe Allaah! Hakika wewe ni Msamehevu na unapenda kusamehe basi nisamehe Mimi".
[صححه الألباني في صحيح الترمذي رقم 3513 ]
❍عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا :
Imepokelewa kutoka kwa 'Aaisha (Allaah amridhie) kuwa:
« أَنَّ النَّبِيَّ ﷺ كَانَ يَعْتَكِفُ الْعَشْرَ الْأَوَاخِرَ مِنْ رَمَضَانَ حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ، ثُمَّ اعْتَكَفَ أَزْوَاجُهُ مِنْ بَعْدِهِ »
"Hakika Mtume (swalla Llaahu 'alayhi wasallam) , alikuwa akikaa itikafu katika kumi la mwisho la Ramadhan , kisha wakaendelea wake zake kukaa baada ya kuondoka kwake".
[متفق عليه :2026-1172]
. [emoji3502]•┈•◈◉✹❒[emoji432]❒✹◉◈•┈•[emoji3502]
[emoji1002]
Duaatsalaftz.net
[emoji402]tembelea Channel yetu ya telegram ili kupata faida zaidi
[emoji748]جزى الله خيرا كل من قرأها وساعدنا على نشرها.