Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

بسم الله الرحمن الرحيم

[emoji2970][emoji2970] ALLAAHUMMA INNAKA 'AFUWWUN TUHIBBUL 'AFWA FA'AFW'ANII"...."((EE ALLAAH HAKIKA WEWE NDIYE MWENYE KUSAMEHE UNAPENDA KUSAMEHE [ALLAAH] BASI NISAMEHE))." [emoji2970][emoji2970]

[emoji294] KWA NINI DU'AA HII IKAWA MAALUMU KWA ATAKAYESIMAMA LAYLATUL QADRI? [emoji294]

Mpenzi msomaji; tukiwa tunajongea jongea "Kumi la Mwisho la Mwezi Mtukufu wa Ramadhwaan", kumi lenye "Kheri na Fadhila kubwa" ndani yake, kumi la "Itikaafu, Qiyaamu Llayl", kumi ambalo unatarajiwa ndani yake Usiku Wa Cheo au "Laylatul Qadri", hili ni kumi la lala salama kwa lugha isiyo rasmi, inayoashiria matumizi makini sana ya muda uliobaki... ni "kumi la "kukithirisha sana Du'aa".

[emoji294] Kama tulivyoashiria ndani ya kumi hili, kuna usiku wa "Cheo au Laylatul Qadri" ambapo ndani yake; huteremka Malaika akiwemo Malaika Mtukufu,... yaani Jibril [Alayhi Ssalaamu] ndani yao, ni usiku wenye "Kheri, Barakah,....." bila shaka ni 'Utukufu wa Usiku huu' kiasi katika usiku huu huwa kuna utulivu, usiku unakuwa hauna "vimondo, upepo..." kiasi hata jua huchomoza bila miale, haya yako nje ya sababu za 'Kisayansi', wala "Wanasayansi" hawawezi kuyaelezea.

[emoji294] Jambo moja zito katika "Usiku Huu Wa Cheo" ni kuwa "Malaika", wanapewa orodha ya matukio ya mwaka mzima ujao, ambayo huchukuliwa kutoka katika [Lawhil Mahfuudhi]. Ndani ya orodha hiyo kuna mambo yoote yatakayotokea mwaka mzima, yakiwemo majina ya wale ambao hawataidiriki "Ramadhwaan ijayo", yaani majina ya 'watakaokufa' katika kipindi cha kati ya Ramadhwaani hii na ijayo, ambao hawataidiriki Ramadhwaan ijayo! [Allaahul Mustaanu]! Hao kama sio mimi ni wewe!!!

[emoji294] Naam hao kama sio mimi ni wewe! Ndiyo ikawa Mtume [Swalla Allaahu Alayhi Wasallama], likifika kumi hili alikuwa anajifunga "kibwebwe", "akikesha", na "akiwaamsha ahli zake....." kwa ajili ya kufanya ibada mbalimbali katika nyusiku hizi ili kudiriki Usiku wa Laylatul Qadri sio kuona kinachoitwa "nyota ya jaha" ambacho hakiko, ibada ndiyo kitu muhimu; "Swala, Du'aa, Dhikri, Kisomo cha Qur'aani....n.k" Hakuna anayenyimwa "Fadhila za Usiku Huu Mtukufu", "hata kama ni wanawake walio katika siku/ada zao au katika nifaasi". Kwa hiyo dada yangu usihofu utapata tu Fadhila hizi maadamu una unafanya yale uliyoelekezwa, kwa kadiri utakavyoweza kuyafanya, yako mambo mengi unayoruhusika kuyafanya "Kishari'ah", hivyo usilale tumia vizuri "Tunu Hii Adhwiimu"!

[emoji294] Na'am... miongoni mwa mambo muhimu kabisa katika "Usiku Huu" na hili ni kwa watu wote, ni kuomba "Du'aa" mbalimbali; omba kwa "lugha" unayoifahamu, omba "Du'aa ya kutoka moyoni mwako....". Pamoja na ujumla wa "Du'aa" katika "Usiku wa Laylatul Qadri", Du'aa inayobeba 'anuwani ya makala hii' ni Du'aa maalumu kabisa kwa atakayediriki "Laylatul Qadri". Kuna hadithi ambayo Bi ‘Aaishah [Radhwiya Allaahu ‘anhaa], anasimulia ya kwamba alisema kumuuliza Mtume wa Allaah [Swalla Allaahu Alayhi Wasallama]: "Ee Mtume wa Allaah, je, nitakaposimama usiku wa Laylatul Qadri niombe nini?" Mtume alisema, ((Sema Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe, basi Nisamehe)).
[Ibn Maajah na kaisahihisha Albaniyyu].

[emoji294] Du'aa hii ni Du'aa nzito mnoo, ndani yake Allaah [Tabaaraka Wata'alaa], anaombwa kwa Jina miongoni mwa Majina Yake Matukufu yaani '[Al 'Afuwwu]', hili ni jina miongoni mwa majina "Matukufu ya Allaah [Tabaaraka Wata'alaa]". Ndani ya "Qur'aani Tukufu" Jina hili limekuja "mara tano"; limekuja likiambatana na Jina jingine la Allaah [Tabaaraka Wata'alaaa] yaani '[Alqadiiru]' katika [Suratu Nnisa'a aya ya [149]].

[emoji294] Mwanadamu anaweza kukusamehe hali ya kuwa hakuwezi, lakini Allaah [Sub'hanaahu Wata'alaa] Ana Uwezo usio na kikomo, pamoja na Uwezo Wake anasamehe. Mara nne zilizobaki Jina hili, limeambatana na Jina lingine la Allaah [Sub'haanahu Wata'alaa], ambalo ni '[Alghafuuru]' kama ilivyokuja katika [Suratu Nnisa'a aya ya [43] na aya ya [99]]. Ambapo ndani yake kuna Msamaha, na hakika ni juu ya Msamaha!!!
"Jina hili Kilugha" linatokana na neno 'afaa' ambalo lina maana mbili; maana ya kwanza ni kitu kizuri cha halali kinachotolewa kwa ridhaa ya nafsi, bila kuombwa kama ilivyokuja katika [Suratul Baqarah aya ya [219]].

[emoji294] Maana ya pili ni kuondosha.
Kwa hiyo katika Jina hili la Allaah [Sub'haanahu Wata'alaa] kuna vitu vitatu; "[Kuondosha, Kufuta na kisha Kuridhia]"!! Allaah [Aliyetukuka] "Anaondosha, Anafuta dhambi za waja wake na kuondosha kabisa athari zake, kisha anawaridhia, na kuwapa baada ya kuridhia msamaha hata bila kuombwa".
Allaah [Sub'haanahu Wata'alaa] ni "Ghafuuru" yaani "Anasamehe Dhambi, anasitiri Duniani na Akhera". Kwa kweli ni "sitara" tu ya Allaah [Sub'haanahu Wata'alaa], ndiyo inayotufanya tupendeze, tusifukue au kuchimbua makaburi. Yule mtunzi wa Nuuniyya Sheikh Alqahtwaaniyya anasema: Wallaahi lau watu wangelijua uozo wa nafsi yangu wangekataa kunisalimia wenye kukutana na mimi na kwa hakika ningelikuwa ni mwenye kudhalilika, ni sitara ya Allaah tu juu ya aibu zangu ndiyo inayonifanya nipendeze mbele ya watu!!!
[Alghafuuru] Anasemehe japo dhambi ingalipo katika 'suhufa' ama, [Al 'afuwwu] "Anasamehe na Kuifuta kabisa Dhambi". Kwa kweli uwepo wa "dhambi Siku ya Qiyamah" katika 'suhufa ya mtu', utampa mtu wasiwasi mkubwa hata kama dhambi hiyo imesamehewa, lakini kwa kuwa Allaah [Sub'haanahu Wata'alaaa] ni "Al 'afuwwu" Anafuta kabisa dhambi, kama vile haikufanywa. "Siku ya Qiyamah" atakuja mtu Allaah [Mtukufu Aliyetukuka] Atamwambia; "sogea ewe mja wangu", atasogea. Allaah [Mtukufu Aliyetukuka] "atamfunika kwa Sitara Yake"; kisha Atamwambia: "unakumbuka dhambi kadhaa wa kadhaa, ulizofanya; nazo ziko katika daftari lako"; atasema "na'am ewe Mola wangu" hadi atadhani kuwa anaangamia"! hapo Allaah Atamwambia; "Nilikusitiri Duniani Nakusitiri na leo Akhera". Huu ni Msamaha [Maghfirat] ama kwa sifa ya ['Afuwwu] Allaah Atamwambia mja Wake: "Nimekuridhia, Nimeridhia uliyoyafanya duniani ingia Peponi"!!! Kama vile mja hakufanya dhambi yoyote.

[emoji294] Ndiyo "Du'aa Adhwiim hii" tunaomba ije kuwa hivyo; tunasema [Allaahumma Innaka 'Afuwwun tuhibbul 'Af'wa Fa'afuwannii].

[emoji2970][emoji2970] [[NDUGU YENU TAWAKKAL HUSSEIN....ABUU THUBAYTA & TAWFIIQ]]
[emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970][emoji2970]

Shukraan Jazaaka Allah
 
IMG_2941.jpg
 
Back
Top Bottom