Ramadhan Special Thread

Hovyo kweli.
Huo mchanyiko Wa chakula ndo unavyowalishaga nyumbani kwako nini,,
Yan sa zingine heri kukaa kimya kuliko kuongea upuuzi.
 
MashaAllah
 
Yanayomlazimu Mtu Mzima Na Mwenye Ugonjwa Wa Kuendelea


Asioweza kufunga, kwa ajili ya utu uzima au kwa ajili sababu nyenginezo, hatofunga badili yake atalisha maskini mmoja kwa kila siku aliokosa kufunga. Allaah (Subhanahu wa Ta’ala) Amesema:

ﻭَﻋَﻠَﻰ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻳُﻄِﻴﻘُﻮﻧَﻪُ ﻓِﺪْﻳَﺔٌ ﻃَﻌَﺎﻡُ ﻣِﺴْﻜِﻴﻦٍ

“Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).”

(Suuratul Baqarah 02 : 184)


‘Atwaa’ amesema alimsikiya Ibn ´Abbaas akisoma Aayah hii kisha akasema

‘’Haikuondolewa. Inawahusu watu wazima waume kwa wake ambao hawawezi kufunga. Ndio watalisha masikini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga.”

[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl na.912 na Imerikodiwa na Imaam Al-Bukhaariy]
 
Mwanamke Mja Mzito (Mwenye Mimba) Au Mwenye Kunyonyesha


Mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha ambaye hana uwezo wa kufunga ama ambaye anahofia afya ya mtoto wake anaweza asifunge, atalisha maskini mmoja na hawajibiki kuilipa siku aliyokula. Ibn ´Abbaas amesema:


“Ruhusa amepewa mtu mzima mume au mke ambapo wataoneleya tabu kufunga, hawatofunga ambapo hawatopendeleya kufunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ya kufunga. Kisha hawatalipa siku walizokosa kufunga hii iliondolewa baada ya Aayah hii:


ﻭَﻋَﻠَﻰ ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻳُﻄِﻴﻘُﻮﻧَﻪُ ﻓِﺪْﻳَﺔٌ ﻃَﻌَﺎﻡُ ﻣِﺴْﻜِﻴﻦٍ


“Na wale wasioweza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. (kwa kila siku).”

(Suuratul Baqarah 02 : 184)


Baada ya hapo ikahakikishwa kuwa mtu mzima mume au mke ambao hawawezi kufunga na mwanamke mwenye mimba au mwenye kunyonyesha, ikiwa watahofia, hawatafunga na watalisha maskini kwa kila siku ambayo hawakufunga.

[Msururu wa Riwaayah hii ni madhubuti imeripotiwa na Al-Bayhaqiy].

Pia imerikodiwa kuwa alisema, ikiwa wakati wa ramadhaan mwanamke mwenye mimba anahofia afya yake, au mwenye kunyonyesha anahofia afya ya mtoto wake, hawatafunga na watalisha maskini mmoja kwa kila siku ambayo hawakufunga na hawatalipa siku hizo kwa kufunga.

[Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.19].


Nafi’iy alisema ‘’Mmoja katika mabanati wa Ibn ´Umar aliolewa na mwanamume wa ki-Quraysh. Akapata mimba na wakati wa Ramadhaan anashikwa na kiu sana. Ibn ´Umar akamwambiya funguwa swawm yako na ulishe masikini kwa kila siku.’’

[Msururu wa Riwaayah ni Swahiyh na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl mjallad 4 uk.20. Imerikodiwa na ad-Daraqutniy].
 
Kiwango gani cha chakula anawajibika kulisha?


Imeelezwa kwamba Anas Ibn Malik alidhoofika sana na hakuweza kufunga mwaka mzima akatayarisha sufuriya THARIYD (Mkate na nyama uliolowana katika supu) kisha akaalika masikini thelathini akawalisha mpaka wakaridhika’’.

[Msururu wa Riwaayah hii ni Swahiyh pia imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika I’rwa al-Ghaliyl, mjallad 4 uk.21 imerikodiwa na ad-Daraqutniy].


Itaendelea....!!!
 
Mm ningependa pia kuwaasa wafanyabiashara kupunguza bei katika mahitaji ya muhimu, huu ni mwezi wa kuchuma thawabu na sio kujiongezea kipato kwa kukomoa walio wanyonge. Nimeona mifano katika Mall nyingi hapa Oman kuna punguzo kubwa la Bei, mashaallah wao matajiri wanafanyiana ihsan jee ss maskini??
Tujitahd ili kila muislam aweze kumudu kula na kunywa katika mfungo wa Ramadhan.
Ramadhan Kareem!!
 
W.warahmatullah wabarakatu.
Mkuu, umetoa mada iliyo bora na nzuri, ila mbn umeshau hata huzo profile kubadili maana Uislam umekataza aian ya hicho ulich Kiweka hapo, nakuomba na kuwaomba wengine walio tayri kuutukuza mwezi mtukufu wabadili profile zao na ziwe zenye muonekano unaokubalika na Uislam.
 
Nawaombea wote Ramadhan njema, Mwenye ez Mungu atujaalie afya njema tuweze kufunga, na wale wagonjwa nawaombea Shifaa Mwenye ez Mungu mwingi wa Rehma na Huruma awaponye na awafanyie wepesi, na wale ambao wanabadilika tabia na khulka zao mwenzi huu wa Ramadhan na kuacha maaswi na tabia mbaya basi namuomba Mwenye ez Mungu awajaalie wabadilike hiov hivo na kamwe wasizirudie zile akhlaaq mbaya! huu ni Mwenzi Mtufuku Mwenzi wa Rehma , Maghf-ira bimaana kuomaba Toba! na Mwenzi unatuunganisha Waislam Dunia nzima! tunawaombe AMAni pia ndugu zetu msio waislam! karibuni tujumuike sote katika Mwenye huu wa BARAKA!
RAMADHAN MUBARAK KWA WAISLAM WOTE FII KULLI MAKAAN! DUNIANI KOTE AMIN
 
Nasikia wale Al shabaab wanasemaga ni haram mwislamu kutumia inernet ni kweli? Maana wao wenyewe wana account hadi Twitter.

Mitandao imeleta mapinduzi katika Iman sana tu! ila inategemea wewe unataka kutmia Mitandao kwa njia gani! Mitandao inafundisha na mitandao inapoteza! ni juu yako Ewe kiumbe wa Mwenye ez Mungu kutaka mitandao ikufundishe Dini yako Iman iongezeke au ikuingize katika shimo la maasi ikutumbukize pabaya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…