Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Asante sana, japo naamini Sala au Funga bila matendo mema havifiki kwa Mungu pia (hiyo ni nyongeza kama hujaiona kwenye hadith)
Tunavyo sahau kuhimizana matendo mema kama nguzo muhimu ya kupokelewa sala (hata kipindi kisichokuwa cha mwezi mtukufu) ndio hapo unakuta watu wanasali ila washirikina, waasharati, mashoga, nk

Salah inakuweka mbali na Maasi, Salah inakukurubisha kwa Mola wako, Salah inakufanya uwe Mcha Mungu, Salah hutakasa Nafsi ya Muumini, Salah ndio Nguzo kuu na mengine hufatia,

Matendo Mema huja kwenye Salah sababu ni lazima uwe Msafi ili uweze Kusali,

Ukiona Mtu anasali lakini bado ni mwenye kutenda maovu basi huyo Imani bado haijamuingia, ukiishikilia Salah kwa dhati utajikuta tu unaacha Ushirikina, Uzinzi, Masengenyo na vinavyoendana na hivyo,

"...hakuna M'bora kati yenu isipokua Mcha Mungu" sasa hapo kwenye Ucha Mungu ndio penye Mtihani,

Tusiache kukatazana Mabaya na Kukumbushana Mazuri, sisi wote ni wa Mwenyeezi Mungu na kwake tutarejea.
 
Waaleykum Salaam Warahamtullah Wabarakatuh,
Nakujibu kwa Niaba ya Ukthy Angel Nylon,

Muda wako wewe kwa kua upo Mwanza basi utafungua swaumu saa kumi na mbili na dakika hamsini na saba (18:57) na daku yako utakula saa kumi na moja na dakika thelathini na tisa (5:39) mpaka muda wa Salah ya fajri ukifika itakua mwisho wako,

Wengi hula saa saba hadi saa tisa wengine wanataka wapate muda wa kufanya ibada za usiku, wengine hawawezi kula alfajir, wengine hawawezi kuamka alfajiri,

Mola wetu Mlezi mwingi wa Rehema anatuambia katika Qur'an,

(….Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]

Na Allah anajua zaidi.
Shukraan. Ni sawa.

Mtu ahakikishe walau dkk chache kabla swala ya alfajiri awe amemaliza kula.

Na vizuri kula kwa kiasi kuepusha makruh katika swaum yako

Wallahu A'alaam
 
IMG-20220410-WA0002.jpg
 
Kwa mtazamo wangu; swala bila matendo mema ni bure na kikapu cha swala ni matendo mema
Ila swala na funga hivi vinaweza kuwa vinajitegemea ila vikifanyika kwa pamoja ni vizuri sana
"tofauti ya muumin na asiye muumin ni swala" unatekelezaje funga(amrisho la allah) ikiwa wewe si muumin?
 
Kwa mtazamo wangu; swala bila matendo mema ni bure na kikapu cha swala ni matendo mema
Ila swala na funga hivi vinaweza kuwa vinajitegemea ila vikifanyika kwa pamoja ni vizuri sana
"tofauti ya muumin na asiye muumin ni swala" unatekelezaje funga(amrisho la allah) ikiwa wewe si muumin?
 
Natamani hii thread ingekuwa active nyakati zote, sio ramadhani tu, ili tuendelee kumkumbushana.

Kwa sababu ukumbusho unawafaa waumini.

Lakini si haba tuendelee kunufaika nayo kadri inavyowezekana.

Unajua jf japo kuna majukwaa mengi lakini ni ngumu kukutana na ukumbusho wa masuala ya dini, na hata kwenye hilo jukwaa la dini mtu akinzisha thread ya hivyo, basi Uzi utavamiwa na inakuwa tafrani.

Lakini lillahi llhadu madhari tuna Uzi huu hasa katika mwezi mtukufu kama huu si haba.

Binafsi huu ni katika nyuzi zangu bora humu jf, huwa nafurahi kuona comments za ndugu zangu wakizungumzia masuala ya dini, na jinsi utulivu ulivyotamalaki.

نسأل الله السلامة و العافية
Tunamuomba Allah atupe salama na afya
 
Natamani hii thread ingekuwa active nyakati zote, sio ramadhani tu, ili tuendelee kumkumbushana.

Kwa sababu ukumbusho unawafaa waumini.

Lakini si haba tuendelee kunufaika nayo kadri inavyowezekana.

Unajua jf japo kuna majukwaa mengi lakini ni ngumu kukutana na ukumbusho wa masuala ya dini, na hata kwenye hilo jukwaa la dini mtu akinzisha thread ya hivyo, basi Uzi utavamiwa na inakuwa tafrani.

Lakini lillahi llhadu madhari tuna Uzi huu hasa katika mwezi mtukufu kama huu si haba.

Binafsi huu ni katika nyuzi zangu bora humu jf, huwa nafurahi kuona comments za ndugu zangu wakizungumzia masuala ya dini, na jinsi utulivu ulivyotamalaki.

نسأل الله السلامة و العافية
Tunamuomba Allah atupe salama na afya
Kweli kabisa , umeongea jambo la msingi sana kwani uzi wa kimasihara upo active mda wote watu wanashusha visa vyao vya uovu lakini kwenye mambo ya kheri sikuzote watu tuko nyuma labda sababu mambo ya dini yanahitaji elimu na umakini coz kuna hatari kubwa ya kupotosha umma kama mtu usipo elezea na kuwasilisha vyema(kielimu) kile unachokifikisha .
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] muumini wa kweli hufanya ibada bila kumbugudhi mtu wala kujionesha onesha hovyo kama ni mcha Mungu .

Hiyo ndo tabia yangu ukiniona utadhani ni mtu nisiyejua chochote kuhusu dini.
[emoji23]
 
Miezi mitukufu ipo minne.ramadhani ni mmoja wapo.
Na una heshima kubwa.ni chuo cha kutenda mema.mwezi wa toba,mwezi wa kuchuma kheri
Mungu ana huruma.na sisi ndo maana ndani ya mwezi wa ramadhani malipo ya kutenda mema ni zaidi.kuliko miezi mingine
Tukitoka hapo haturuhusiwi kutenda dhambi.miezi mingine
Samahani mpendwa, kwa mujibu wa riwaya zilizothibiti kisharia mwezi wa Ramadhani si katika miezi minne mitukufu, miezi mitukufu iliyotajwa ni Dhul-Qadah, Dhul-Hijjah, Muharram na Rajab, ambapo hiyo mitatu ya mwanzo imeongozana na mwezi Rajab peke yake ndo umejitenga. Utukufu wa mwezi wa Ramadhani ni katika lugha tu na ada za watu 'mazoea' kutokana na kuenea fadhila nyingi ndani yake. Kama utahitaji marejeo 'reference' nifahamishe. Ahsante
 
Ramadhaan – mwezi wenye baraka

Imepokelewa katika Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ameueleza mwezi wa Ramadhaan kuwa ni mwezi uliobarikiwa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Umekujieni mwezi wa Ramadhaan – ni mwezi wenye baraka. Allaah amekufaradhishieni kufunga. Ndani yake milango ya Pepo hufunguliwa, milango ya Moto hufungwa na mashaytwaan waovu hutiwa pingu.”[1]

Tunacholenga katika Hadiyth ni pale ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameusifu mwezi wa Ramadhaan kuwa ni wenye baraka. Baraka za mwezi huu zinakusanya vipindi vyake vyote na kila saa, kuanzia mwanzo wa kuingia kwake mpaka kutoka kwake. Vipindi vyake vyote vimebarikiwa. Ndani yake kuna baraka, kheri nyingi na fadhila nyingi.

Miongoni mwa baraka za mwezi huu ni yale aliyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth hii ya kuwa inafunguliwa milango ya Pepo, inafungwa milango ya Moto na mashaytwaan waovu wanatiwa pingu. Baraka hizi ni maalum juu ya mwezi huu pekee. Ni baraka ambazo hazipatikani katika miezi mingine. Zote hizi ni baraka tukufu ambazo zinaamsha hima, maazimio na kuwapa uchangamfu watu kumwelekea Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

[1] Ahmad (7148) na an-Nasaa´iy (2106) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
Mfasiri: Firqatunnajia
Marejeo: Wa jaa´ Shahru Ramadhwaan, uk. 15-16
Imechapishwa: 13/04/2022
 
Back
Top Bottom