Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Asalam Alykum warahmutulah wabarakat

Hii App ina Adhkari na Dua zilizothibiti...
Screenshot_20220407-135253.jpg
Screenshot_20220407-135010.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadithi ndio hizo nimekupa, kazi kwako sasa kuzipitia kwa utulivu, "Tofauti yenu na wao ni SALAH"
pia Allah (s.w)ameweka wazi hukumu kua asiyeswali basi amemfutia amali zake zooote duniani na akhera vipi tena hao wanazuoni waseme funga inakubalika na wakati amali zimeshafutwa??? kwa hiyo asiyeswali hata awe mwema kiasi gani hana anachoandikiwa mpaka atubu na kuanza kusali,

"Hakuna m'bora kati yenu isipokua MCHA MUNGU" Qur'an.

Kila la kheir.
Kwa mtazamo wangu; swala bila matendo mema ni bure na kikapu cha swala ni matendo mema
Ila swala na funga hivi vinaweza kuwa vinajitegemea ila vikifanyika kwa pamoja ni vizuri sana
 
Hivi tunafunga kama kufunga tu(mazoea) ama tunafunga kama tulivyofundishwa(mazingatio)

Katika kila jambo allah hajaleta hivi hivi tu kuna kuwa na elimu ndani yake na faida kubwa tukiachana na faida za kiafya na nyinginezo hebu twende kwenye mazingatio

Nataka nizungumzie jambo moja na kwa uchache mnoo, sababu hii ni mada pekee yake inayojitegemea, kwa sisi vilaza kwa mazungumzo tunaweza tumia dk 10 hivi, wenye elimu zao hata lisaa li1 linakatika, hivyo maongezi ya dk 10 siwezi hamishia katika maamdishi, ndugu zangu waislamu, uislam ni dini ya upendo na kujaaliana, hizi swaumu tunazofunga lazima ziwe na mazingatio, hizi njaa tunazokaa nazo tangu alfajiri mpaka magharibi kwa siku 30 basi kuna wenzetu ndio maisha yao, kuna wenzetu ni mlo mmoja kwa siku, inastaajabisha kukuta muislam anakula na kusaza mixer kumwaga chakula wakati jirani yake analala njaa, tupendane tujaliane, nini uislamu umetufundisha kwa majirani zetu ni zipi haki za majirani zetu, je tunazitekeleza, inatupasa uislam uingie kwenye maisha yetu, uislam ni mfumo wa maisha.

Allah anatuambia katika suratul an nisaa aya ya 36
Mwabuduni Mwenyezi Mungu wala msishirikishe na chochote. Na wafanyeni ihsani wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na maskini, na jirani walio karibu au jirani walio mbali.

Mtume(s.a.w) anasema kuna kipindi jibril alikuwa kila akija anamuhusia saana kuhusu jirani yake, kiasi mtume akajiuliza au huyu jirani yangu ndio mrithi wangu nini

Kwa haya machache unaweza kuona umuhimu wa jirani, sasa inakuwaje hatuwatembelei majirani zetu, hatuwasaidii, jirani anapata msiba huendi kuzika, anaumwa huendi kumuona, tunaishi nje ya misingi ya Kiislamu, na hii haijalishi jirani yako awe muislamu mwenzio, awe mkristu, myahudi, hata awe ni mbudha ni haki yake hiyo
Tujitahidi na allah atufanyie wepesi kwa kweli.
 
Asalam alaykum warahmatullah wabaratuh! ..
Naomba ufafanuzi kidogo kwenye hili jedwali la ratiba ya Ramadan muda wa kufungua swaum na kula daku.

Imezoeleka waislam katika maeneo mengi hujiwekea muda wao wa kula daku, wengine saa 9 usiku , wengine saa 10 hadi 10:30! Mara chache sana kukuta muislamu anakuambia yeye kala daku saa 11:00.
Hivyo basi kwa mujibu wa jedwali hili, Mimi nikiwa hapa mkuyuni jijini Mwanza natakiwa leo ramadhan 7 niishie saa ngapi kula daku ? Pia muda wangu wa kufungulia swaumu ni saa ngapi?

Natanguliza shukrani
 
Waaleykum Salaam Warahamtullah Wabarakatuh,
Nakujibu kwa Niaba ya Ukthy Angel Nylon,

Muda wako wewe kwa kua upo Mwanza basi utafungua swaumu saa kumi na mbili na dakika hamsini na saba (18:57) na daku yako utakula saa kumi na moja na dakika thelathini na tisa (5:39) mpaka muda wa Salah ya fajri ukifika itakua mwisho wako,

Wengi hula saa saba hadi saa tisa wengine wanataka wapate muda wa kufanya ibada za usiku, wengine hawawezi kula alfajir, wengine hawawezi kuamka alfajiri,

Mola wetu Mlezi mwingi wa Rehema anatuambia katika Qur'an,

(….Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]

Na Allah anajua zaidi.
 
Kwa mtazamo wangu; swala bila matendo mema ni bure na kikapu cha swala ni matendo mema
Ila swala na funga hivi vinaweza kuwa vinajitegemea ila vikifanyika kwa pamoja ni vizuri sana
Mtazamo wako???
Nani alikwambia kwenye Dini kuna Mitazamo binafsi??

Dini ya Uislam inaongozwa kwa Qur'an na Sunna basi hakuna Mitazamo binafsi,

Mtume wetu Muhammad (S.A.W) anasema,

(....Ahadi ambayo iko baina yetu na baina yao (makafiri) ni Swalaah, na mwenye kuiacha basi amekufuru.....) [Ahmad]

Unaijua hukumu ya mwenye kukufuru,
Sallah na Funga vinaenda Sambamba wala haviachani .

Na Allah anajua zaidi.
 
Asalam alaykum warahmatullah wabaratuh! ..
Naomba ufafanuzi kidogo kwenye hili jedwali la ratiba ya Ramadan muda wa kufungua swaum na kula daku.

Imezoeleka waislam katika maeneo mengi hujiwekea muda wao wa kula daku, wengine saa 9 usiku , wengine saa 10 hadi 10:30! Mara chache sana kukuta muislamu anakuambia yeye kala daku saa 11:00.
Hivyo basi kwa mujibu wa jedwali hili, Mimi nikiwa hapa mkuyuni jijini Mwanza natakiwa leo ramadhan 7 niishie saa ngapi kula daku ? Pia muda wangu wa kufungulia swaumu ni saa ngapi?

Natanguliza shukrani
Kutokana na mafundisho sahihi ya Mtume Muhammad(Upon him be paece and blessing of Allah )sunna ni mtu kuwahi kufuturu haraka muda unapoingia(jua kuzama) na daku kuchelewesha .Hata yeye mwenyewe Ktk hadithi sahihi imepokelewa muda alokuwa akijizuia (kula daku) mpk muda wa adhana ya alfajiri(ile alfajiri ya kweli adhana ya saa 11 kikwetu) ni wakati wa mtu kusoma aya 50 .

Hivyo mtu kuchelesha kula daku (mfano kula mida ya saa 9 ,10 ,10:30 nk ikiwa muda wa kujizuia unaanza 11 :00) ndiyo inapendeza zaidi na unapata fadhila kubwa ya kufuata sunna ya Nabii na yeye mwenyewe amesisitiza sana jambo hilo na kusema tuwe tofauti na fungal za watu wa kitabu (Mayahudi na Manasara) kwani wao wanawahi kula daku na wanachelewa kufuturu .

Kutokana na swali lako kama muda wa mwisho kula daku umeandikwa mwisho saa 11 :15 mtu ana haki kuanza kula hata saa 11:00 ilimradi isifike mpk muda wa kupambazuka alfajiri ya kweli (11:15 ikiwa ratiba inasema hivyo) wengine wanapunguza km lisaa au nusu saa nyuma kuhofia kupiga mboli nyingi mchana au kuwa na muda wa kumdhukuru Allah na ibada nyingine baada ya daku .

Nb:Mtu akila daku sasa 2 ,3 nk haiwi daku bali ni chakula cha usiku sunna ya daku mtu acheleweshe at least alale kisha aamke ili apate fadhila za daku kwani kina heri na fadhila nyingi ndio maana Mtume Muhammad SwallaAllahu'aleyhi wa salaam)alisisitiza mtu hata kama hana cha kukila usiku aamke anywe hata vikombe vya maji ili kupata fadhila za daku
#AllahuA'lamu
 
Jazakallah khaira
 
Waaleykum Salaam Warahamtullah Wabarakatuh,
Nakujibu kwa Niaba ya Ukthy Angel Nylon,

Muda wako wewe kwa kua upo Mwanza basi utafungua swaumu saa kumi na mbili na dakika hamsini na saba (18:57) na daku yako utakula saa kumi na moja na dakika thelathini na tisa (5:39) mpaka muda wa Salah ya fajri ukifika itakua mwisho wako,

Wengi hula saa saba hadi saa tisa wengine wanataka wapate muda wa kufanya ibada za usiku, wengine hawawezi kula alfajir, wengine hawawezi kuamka alfajiri,

Mola wetu Mlezi mwingi wa Rehema anatuambia katika Qur'an,

(….Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]

Na Allah anajua zaidi.
Shukran ,, Allah akuzidishie elimu na iwe yenye manufaa
 
Wa,alaykum salaam warahmatullah wabarakatuh!
Dua zilizothibiti ndio zinakuwaje ikhiwa?
Kuna vitabu vya adhkari vimejaa nyiradi za uzushi i.e utajipinda kuvisoma mwisho wa siku ni vumbi tupu( hupati ujira) ...

So hiyo app ina Dua na Adhkar (zilizothibiti katika hadith sahihi (Mwisho wa kurusa utaona uthibitisho)

Kwaiyo ukisoma utapata ujira na pia kama za kukukinga na mashytwan zitakukinga....

Allahu a'alm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtazamo wako???
Nani alikwambia kwenye Dini kuna Mitazamo binafsi??

Dini ya Uislam inaongozwa kwa Qur'an na Sunna basi hakuna Mitazamo binafsi,

Mtume wetu Muhammad (S.A.W) anasema,

(....Ahadi ambayo iko baina yetu na baina yao (makafiri) ni Swalaah, na mwenye kuiacha basi amekufuru.....) [Ahmad]

Unaijua hukumu ya mwenye kukufuru,
Sallah na Funga vinaenda Sambamba wala haviachani .

Na Allah anajua zaidi.
Asante sana, japo naamini Sala au Funga bila matendo mema havifiki kwa Mungu pia (hiyo ni nyongeza kama hujaiona kwenye hadith)
Tunavyo sahau kuhimizana matendo mema kama nguzo muhimu ya kupokelewa sala (hata kipindi kisichokuwa cha mwezi mtukufu) ndio hapo unakuta watu wanasali ila washirikina, waasharati, mashoga, nk
 
Back
Top Bottom