[emoji287]Masaa matatu kwa siku katika mwezi wa Ramadhani yasikupite kwa thamani yoyote ile ukiyahifadhi, nayo ni masaa matatu kwa idadi ya siku za Ramadhani yanakua kwa Jumla masaa (90) nayo ni kama yafuatavyo:[emoji287]
1- [emoji314]Saa moja wakati wa kufuturu hakika andaa futari yako mapema na ujipe faragha kwa ajili ya dua, kwasababu mwenye kufunga wakati wa kufungua kwake ana Dua ambayo hairudi patupu, jiombee mwenyewe na vipenzi vyako na waombee maiti wa kiislamu kwasababu wanahitaji kutoka kwako Dua.[emoji314]
2- [emoji314]Ama lisaa la pili: Ni mwisho wa usiku jipe faragha uwe pamoja na Allah kwasababu yeye ana ita akisema nani anaomba nimpe nani anataka msamaha nimsamehe, na uzidishe katika usiku huo kwa kumuomba Allah msamaha.[emoji314]
3- [emoji314]Ama lisaa la tatu: Ni kukaa kwako baada ya swala ya Alfajiri katika mahali uliposwali ukifanya adhkar mpaka jua likachomoza kwasababu ni sawa na umra na hijja iliyo kamilika.[emoji314]
[emoji314]Haya ni masaa tisaini, na kua na pupa na wakati mwengine uliobaki wote kwa kumtaja Allah, na ujiepushe na usengenyaji kwasababu unamaliza thawabu zako, na weka azma isikupite swala ya faradhi na uchukue fursa ya kutekeleza Swala za sunna, kwasababu ni siku thalathini, na niharaka iliyoje tukijipata tukisema imeisha, Allahul Mustaan![emoji314]
[emoji314]Hata ukinuwia kueneza maneno haya nuwia kwa ajili ya kheir, huenda Allah akakufariji kwa mazito katika mazito ya Dunia na Akhera[emoji314]
[emoji314]Na kumbuka: fanya kheir hata ukaiona ndogo vipi kwasababu hujui jema gani litakuingiza peponi[emoji314]
[emoji287] [emoji619]RAMADHAN MUBAARAK[emoji287] [emoji619]