Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Kumbe na wewe black sniper ni Muislamu? Nilikua nakutukana bure Jana, sorry!

Sema una hulka fulani hivi hufananii kabisa na Muislamu muungwana, sijui wewe ndo wale 'waislamu jina'

Unaona unavyotafuta dhambi kwa nguvu
Unawezaje kumjua mtu kwa comments zake? Na kumhukumu juu
Hivi hapo unaona makosa yako halafu unaniita tena Muslim jina eti sifanani na muungwana duu

Kwa taarifa yako nimeenda Hijja 1987 na Umra x2
Nikupe darsa dogo don’t judge the book by its cover
Pia humu nimefanya Uungwana sana tu kwa wanaohitaji

Hayo uliyonihukumu jitafakari sana wewe
Je unazo sifa njema?
Ftari njema mwanangu
 
Asalam alaykum vipi hali zenu ndugu zangu waislamu.
Alhamdulillha rabil alaamin leo mimi nipo katika swaumu sijui tuko wangapi humu?
Mwezi huu ni mwezi wa kuchuma thwawabu tele kwa kufanya kheri ndogo unalipwa kwa wingi zaidi,tujikurubishe katika madarasa ya qur an misikitini na pia tusome sana Qur an ndani ya mwezi huu wa Ramadhan tujipime imani zetu kuna mabadiliko kila baada ya Ramadhani.Tumuombe allah atulipe kheri zote ndani ya mwezi huu,nawatakia Ramadhani njema waislamu wote humu Jf.
 
Unaona unavyotafuta dhambi kwa nguvu
Unawezaje kumjua mtu kwa comments zake? Na kumhukumu juu
Hivi hapo unaona makosa yako halafu unaniita tena Muslim jina eti sifanani na muungwana duu

Kwa taarifa yako nimeenda Hijja 1987 na Umra x2
Nikupe darsa dogo don’t judge the book by its cover
Pia humu nimefanya Uungwana sana tu kwa wanaohitaji

Hayo uliyonihukumu jitafakari sana wewe
Je unazo sifa njema?
Ftari njema mwanangu
Kama ulienda Hijja 1987 basi wewe ni sawa na Faza...unastahili heshma kubwa nawe uishi kwa kujiheshimu kwa kuwa una darja kubwa kuliko watu wengi allah akuongoze insha allah.
 
Kama ulienda Hijja 1987 basi wewe ni sawa na Faza...unastahili heshma kubwa nawe uishi kwa kujiheshimu kwa kuwa una darja kubwa kuliko watu wengi allah akuongoze insha allah.

Sijamkosea mtu humu najujua sana
Rejea comments zangu na michango yangu humu
Hasha siwezi kumvunjia mtu heshima kwani nina wajukuu humu

Una maana gani niishi kwa kujiheshimu
 
.
Screenshot_20220403-045949~2.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijamkosea mtu humu najujua sana
Rejea comments zangu na michango yangu humu
Hasha siwezi kumvunjia mtu heshima kwani nina wajukuu humu

Una maana gani niishi kwa kujiheshimu
Kutokana Na maelezo ya yule kijana mlolongo eti alikuwa anakutukana nikahisi ulikuwa unamfanyia mizaha...ila samahani sheikh Kama nimekukosea.
 
Asalam alaikum ndugu waislamu vipi Hali zenu popote mlipo Mimi sijambo, alhamdulillah.

Je umesoma Qur an leo Kama ndio basi Allah akulipe zaidi Na zaidi,Kama bado basi jitahidi usome au ufundishwe Na mjuzi aliyekuzidi...pia no vyema kuhudhuria darsa misikitini...Mara nyingi kipindi hichi misikitini huwa Kuna darsa la tafsir ya Qur an...naamini ukisikiliza kwa hata dakika tano,utapata malipo Kama msomaji..Allah atufanyie wepesi inshallah.

Mpaka Sasa nime jitahidi kusoma juzuu 2,nimeweka Nia kusoma juzuu zote 30 ndani ya mwezi huu kwani Kuna malipo makubwa Sana kwa sababu ni mwezi ambao ilishuka Qur an...Kila ukisoma herufi moja unalipwa thwawabu 10....kwa hiyo Kuna malipo makubwa tukiweza kusoma juzuu zote 30 au kiasi ulichojaaliwa kufahamu.

Kila mmoja wetu ajitahidi kusoma Qur an kadri alivyojaaliwa ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
 
Kutokana Na maelezo ya yule kijana mlolongo eti alikuwa anakutukana nikahisi ulikuwa unamfanyia mizaha...ila samahani sheikh Kama nimekukosea.

Nilichangia hoja nae akaandika mawazo yake that’s all
Hakunitukana ila anahisi hivyo
Nawaombea mfungo mwema nyote
 
Pia Waislamu tusifunge bila kuswali...kwani imekuwa desturi yet kufunga swaumu bila kudiriki ibada ya Sala tano...funga yako haiwezi kupokelewa ikiwa umefunga bila kuswali Kama tulivyoamrishwa,tusimamishe au tudumishe Sala,tutor zaka na tufunge mwezi mtukufu wa Ramadhani..swala tano na swaumu ni kurwa na doto hivyo tuvitekeleze vyote kwa pamoja insha allah tuweze kurehemewa
 
Back
Top Bottom