Waaleykum Salaam Warahamtullah Wabarakatuh,
Nakujibu kwa Niaba ya Ukthy
Angel Nylon,
Muda wako wewe kwa kua upo Mwanza basi utafungua swaumu saa kumi na mbili na dakika hamsini na saba (18:57) na daku yako utakula saa kumi na moja na dakika thelathini na tisa (5:39) mpaka muda wa Salah ya fajri ukifika itakua mwisho wako,
Wengi hula saa saba hadi saa tisa wengine wanataka wapate muda wa kufanya ibada za usiku, wengine hawawezi kula alfajir, wengine hawawezi kuamka alfajiri,
Mola wetu Mlezi mwingi wa Rehema anatuambia katika Qur'an,
(….Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]
Na Allah anajua zaidi.