Dream Queen
JF-Expert Member
- Nov 4, 2015
- 8,263
- 18,201
Asante sana, japo naamini Sala au Funga bila matendo mema havifiki kwa Mungu pia (hiyo ni nyongeza kama hujaiona kwenye hadith)
Tunavyo sahau kuhimizana matendo mema kama nguzo muhimu ya kupokelewa sala (hata kipindi kisichokuwa cha mwezi mtukufu) ndio hapo unakuta watu wanasali ila washirikina, waasharati, mashoga, nk
Salah inakuweka mbali na Maasi, Salah inakukurubisha kwa Mola wako, Salah inakufanya uwe Mcha Mungu, Salah hutakasa Nafsi ya Muumini, Salah ndio Nguzo kuu na mengine hufatia,
Matendo Mema huja kwenye Salah sababu ni lazima uwe Msafi ili uweze Kusali,
Ukiona Mtu anasali lakini bado ni mwenye kutenda maovu basi huyo Imani bado haijamuingia, ukiishikilia Salah kwa dhati utajikuta tu unaacha Ushirikina, Uzinzi, Masengenyo na vinavyoendana na hivyo,
"...hakuna M'bora kati yenu isipokua Mcha Mungu" sasa hapo kwenye Ucha Mungu ndio penye Mtihani,
Tusiache kukatazana Mabaya na Kukumbushana Mazuri, sisi wote ni wa Mwenyeezi Mungu na kwake tutarejea.