Ramadhan Special Thread

HILO NI NENO NALO (1818)
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kufunga si kuacha kula tu, bali ni kujiepusha na maneno machafu na mambo yote aliyochukia Allah (swt). Ikiwa una tabia mbaya, sasa ni wakati wa kujizuia na kufanya mabadiliko mazuri milele. Achana na porojo, porojo, matusi, uwongo na kashfa. Fanya kila kitu ili kuhakikisha mfungo wako unakubalika na kuwa bora zaidi.
IMETAYARISHWA NA
[emoji263]DARSA YA FIQHI[emoji263]
 
UJUMBE WA ASUBUHI
~~~~~~~~~~~~
LEO KTK UJUMBE WA ASUBUHI:

Mwanamke mmoja anasema: nilikuwa naswali na alikuwa mtoto wangu mdogo ananita mama mama mama na wala sikumuitikia kwa vile nipo kwenye sala, alikuja kaka yake ambaye amemzidi kiumri kwa miaka miwili tu na akasema kumwambia mdogo wake: zio vizuri juu yako kukatisha maongezi ya ya wawili, kwani mama asaivi anaongea na ALLAH.

Hakika mwili wangu ulitetemeka na zikanijia hisia za udhalilifu mbele ya mtukufu niliyesimama mbele yake na maneno hayo yanagonga masikioni mwangu na kwenye fikra zangu na moyoni mwangu kila nnapo soma takbira kwa ajili ya sala.
Ametakasika ALLAH ambaye ameingiza hekima kwenye vinywa vya watoto ambao hawajafikia umri wa kubalegh.

Ee Mola tunakuomba utupe unyenyekevu wa ukweli ( kwenye sala.)

[emoji263]DARSA YA FIQHI[emoji263]
 
Vipi updates za mwezi leo umeonekana mahali popote ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…