Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Screenshot_2017-05-25-10-50-26_1.jpg
Ukhuty huyu ni wewe au?? Nimem'bamba mahali maneno anayopenda kuyaongea na wewe ndo hayo hayo unayapenda halafu kingine na yeye anaitwa Ukhuty

Screenshot_2017-05-25-10-54-40_1.jpg
 
Hamna mme na mke bila ndoa katika Uislam, hao ni mahawara na wanafanya zinaa, zinaa ni uchafu ktk Uislam, km alivyosema Allah fil Qur'anil kariim kwamba;
"Na msiikurubie zinaa hakika zinaa ni uchafu na ni dhambi kubwa"
Ili ufunge unatakiwa kuwa tohara, na hao watu wawili hawako tohara inaamaana hawana funga wanashinda na njaa.
Swadakta , Tenahii hata kwa wale wazee wa ndoa yabomani hawaruhusiwi pia coz haitambuliki kidini
 
Penelope mwanaume na mwanamke kukaa bila ndoa ni haramu ndani ya mwezi wa Ramadhan na miezi mingine pia, yaani ni haramu siku zote. Wakitaka kukaa pamoja ni lazima ndoa kwanza kisha mambo mingine, hakuna kuonja... Dalili ni kama alivyogusia hapo thatsit, na saumu zao zipo hatarini.
Na ni wajibu kwao kutubia kwa mola wao kama ikiwa ni wakweli katika dini yao, na Allah anamsamehe kila mwenye kutubia. Na miongoni mwa masharti ya toba ni; 1 kuacha hilo dhambi, 2 kujutia kulifanya, 3 kuazimia kutolirudia tena, 4 na kama kuna haki ya mtu ni lazima airudishe kisha amalizie na hayo matatu hapo mwanzo.
Allah atusamehe madhambi yetu yote. Amiin
 
Assalaam alaykum warahmatullahi wabaraakatuh ndugu zangu ktk imani.!
Nasaha!
Ni vizuri kuwa mkarimu, mpole, mwenye busara na hekima pamoja na uzuri wa tabia katika kauli na matendo ambayo hujengeka katika ya IKHLASW katika nafsi zetu katika nyakati zetu za maisha yetu hapa duniani.
Tuwe wazuri ndani na nje ya masiku ya mwezi mtukufu wa Ramadhani si vyema ukawa fedhuri,muhuni,mkorofi, mwizi na mwenye lugha chafu nje ya mwezi mtukufu na kuwa mwema ndani ya mwezi ujao wa ramadhani!
Usiwe Abubakr ndani ya msikiti na ukawa Abujahl nje ya msikiti!
Allah atufanyie wepesi katika maisha yetu bila kubagua miezi ya kufuata amri zake!
Amiyn.!
 
Penelope mwanaume na mwanamke kukaa bila ndoa ni haramu ndani ya mwezi wa Ramadhan na miezi mingine pia, yaani ni haramu siku zote. Wakitaka kukaa pamoja ni lazima ndoa kwanza kisha mambo mingine, hakuna kuonja... Dalili ni kama alivyogusia hapo thatsit, na saumu zao zipo hatarini.
Na ni wajibu kwao kutubia kwa mola wao kama ikiwa ni wakweli katika dini yao, na Allah anamsamehe kila mwenye kutubia. Na miongoni mwa masharti ya toba ni; 1 kuacha hilo dhambi, 2 kujutia kulifanya, 3 kuazimia kutolirudia tena, 4 na kama kuna haki ya mtu ni lazima airudishe kisha amalizie na hayo matatu hapo mwanzo.
Allah atusamehe madhambi yetu yote. Amiin
Allahuma aamina
 
MFUNGO UNAANZA LINI NA MIMI NIJITAHIDI KUFUNGA,,
NAWATAKIA MFUNGO MWEMA

SWALI;KWA MUME NA MKE WANOISHI PAMOJA BILA NDOA KWENYE MFUNGO HAPO INAKUAJE
Mimi nilimsikiliza Sheikh mmoja kutoka Saudia kama sjakosea alikuwa akitoa mawaidha kwa kiingereza, alichosema yeye kama unajua unatenda dhambi na kuna ibada unatakiwa ufanye we fanya ibada, kama ni ibada ya sala kasali hata kama wewe ni mnywaji pombe hata kama ni mzinzi wewe katekeleze ibada hiyo, usiache kufanya ibada kwa kisingizio kuwa wewe ni muovu au kwa kisingizio wewe una lala na mtu bila ya kufunga ndoa au kwa kisingizio wewe ni muuaji, tekeleza ibada kwanza huezi jua inawezekana kupitia ile ibada kama ya kufunga au kusali mungu akafanya wepesi ukaamua kuacha zambi unazofanya. Cha umuhimu we Funga ila hizo zambi unazofanya pia jaribu kuacha kwani Mungu ni mwepesi wa kusamehe.
 
[emoji432][emoji432]
[emoji432]

✮ *_صلاة التطوع_* ✮

[emoji403] *_SUNNA YA ALFAJIRI_* : ➊
•┈┈•┈┈•⊰✿[emoji432]✿⊱•┈┈•┈┈•

[emoji830]Swala za sunna ni zile ambazo zaidi au nyongeza ya swala za faradhi Na zina umuhimu na malipo makubwa Kwani swala za sunna zina inua Daraja ya mja

[emoji830]️ قَالَ رَسُولَ اللَّه ﷺ :

[emoji428] Juu yako kukithirisha kusujudu , kwani hautosujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa kwayo Allah ata kuinua Daraja na kukusamehe makosa yako ... [emoji428]
[[ *_أخرجه مسلم { ٤٨٨} _*]]

[emoji830] Miongoni mwa swala za sunna ambazo zimetiliwa mkazo ni *_RAKAA MBILI [ za sunna ] YA ALFAJIRI_*

Rakaa hizo zimetiliwa mkazo sanaa na mtume ﷺ Amesema :

*_Rakaa za ALFAJIRI ni bora kuliko dunia na vilivyomo_*

✾ ‏قال ابن القيم رحمه الله :

Na kwa maana hio ndio maana hakuacha mtume ﷺ Swala hio (rakaa mbili za sunna ya alfajiri ) na swala ya witri iwe yupo safarini au nyumbani ......

[emoji402] *_Rejea_* [emoji676]
[[ الزاد المعاد : { ١/٣١٥ } ]]
▂▂▂▂▂▂▂▂▂▂

*_SIFA YA SWALA HIO_*

[emoji830] Ni sunna kuifanya nyepesi swala hio (kutoirefusha sana) na zimethibiti hadithi nyingi kutoka kwa mtume ﷺ kuwa alikuwa akiifanya nyepesi : Miongoni mwa masimulizi Hayo ni kama yafuatayo :

➊ Alikuwa mtume ﷺ Akiswali rakaa mbili hafifu baina ya adhana na ikama ya swala ya asubuhi [[ Al bukhari : 584 ]]

➋ Alikuwa mtume ﷺ akizifanya nyepesi rakaa mbili Kabla ya swala ya asubuhi mpaka nikawa nasema Angalau amesoma mama wa kitabu ? (Suratul fat-ha) [[ Muslim : 1189 ]]

[emoji830] Kwaio ni sunna kuifanyia tahfifu na kuzifanya nyepesi rakaa hizo mbili za sunna za Kabla ya swala ya Alfajiri , Lakini pia tujitahidini kudumu na sunna hio kwani ni bora kuliko dunia na yaliomo

[emoji830] Pia katika sunna basi rakaa hizo mtu aziswali nyumbani kwake Kabla hajatoka kwenda kuswali swala ya Alfajiri

Kama mtu ataswali sunna hizo nyumbani kwake : kisha akafika msikitini Kabla watu hawajaanza kuswali basi ataswali pia (hapo msikitini ) rakaa mbili za maamkizi ya msikiti

[emoji830] Ama kama mtu ametoka nyumbani kwake hujaswali sunna hizo na akafika msikitini Bado watu hawajakimu basi ataswali rakaa mbili kwanza za sunna Kabla ya Alfajiri
✮✮✮✮✮✮✮✮✮✮✮✮✮
•┈┈•┈┈•⊰✿[emoji432]✿⊱•┈┈•┈┈•
 
MFUNGO UNAANZA LINI NA MIMI NIJITAHIDI KUFUNGA,,
NAWATAKIA MFUNGO MWEMA

SWALI;KWA MUME NA MKE WANOISHI PAMOJA BILA NDOA KWENYE MFUNGO HAPO INAKUAJE
Kama watu hawajafunga ndoa wanakuaje ni MKE na MUME???

Hiyo ni zinaa na zinaa ni uchafu, fungeni ndoa ili mfanye ibada zenu hali ya kua Mola yu radhi na ninyi.
 
...Amesema mtume swallallahu alahi wassallam:

“Funga ni kinga, ikiwa mmoja wenu atakuwa amefunga, basi asiseme maneno machafu, na wala asifanye mambo ya kijinga, na akitokea mtu akagombana nae, au akamtukana, aseme, “Mimi nimefunga”

[emoji263]βhυκhαrγ ηα Μυslιm[emoji263]

Usije kujikuta unashinda njaa bure kutokana na kuyafanya miongoni mwa mambo yaliyo katazaa kwa mfungaji kuyafanya. Kama vile Kutukana, Kuteta, Kusengenya, Kupigana. Haya ni miongoni mwa mambo yanaharibu funga. Hivo nivema tukazihifadhi ndimi zetu kwa kuyaepuka Maneno mabaya ili ianda ya funga iwe na manufaa kwetu. Pia kumbuka kwamba: Fitna nijambo zito sana na ndio maana Allah mtukufu akaandaa adhabu kali kwa wafitinishaji.

Allah ﷻ Anasema:

Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. (85:10)

Yaa Allah, Tujalie tuwe wenye kutekeleza ibada ndani na baada ya mwezi wa Ramadhani Iη Shαα Αllααh.
 
السلام عليكم و رحمة الله و بركاته

*KARIBU TUPANGE KWA AJILI YA RAMADHANI 1438*

_BAHASHA LA KUPANGA_

*1: Nini*
*2: Kwa nini*
*3: Nani*
*4: Vipi*
*5: Wapi*
*6: Lini*
*7: Gharama kiasi gani*
*8: Kwa faida ya nani*

Maswali haya tulisema yana tuongoza kufikiri na kutafakari kwa makini ili kuhakikisha tunakua na uelewa mpana kabla ya kutenda.

Kwa kuanza kufungua bahasha letu la kupanga kwa ajili ya ramadhani 1438.

*1: Nini lengo la kupanga kwa ajili ya ramadhani 1438 ?*

_Jibu: Kufikia lengo la swaum *kua wacha mungu*_

*2: Kwa nini , au lengo hili lina umuhimu gani kwa sasa ?*

_Jibu : Ili waislam waweze kutekeleza amri na kuacha makatazo_

*3: Vipi au namna gani lengo hilo litafikiwa ?*

_Jibu : Kwa kufanya maandalizi sahihi ya *Kinafsi , Kimwili na ya kijamii*_

*4: Lini au muda gani utekelezaji wake utakua muafaka na manufaa zaid ?*

_Jibu : Toka kuandama mwezi mwadamo Wa ramadhani hadi kuanza kwa mwezi Wa shawwaal._

*6: Wapi au ni sehemu ipi shughuli hii itafanikiwa zaid ?*

_Jibu : Nchini Tanzania chini ya mazingira ya kitwaghut_

*7: Kwa gharama kiasi gani ?*

_Jibu: Kwa kuandaa bajeti ya futari na daku za halali_

*8: Juhudi zote hizi kwa faida ya nani ?*

_Jibu: Kwa mwislam binafsi , familia yake na jamii ya kiislam_

*_Kwa tafakuri yako binafsi na wewe pia unaweza na majibu tofauti ni haya ila niya yetu ni kila mmoja wetu awe na uelewa kwa tunalotakiwa kutenda_*


*_KAZI BINAFSI YA LEO_*

✍ Kutokana na swali namba 1&2

_Andika malengo madogo 5 ambayo ungependa kuyatimiza Ktk ramadhani hii ya mwaka 1438 iwapo utakua ni miongoni watakao wezeshwa na Allah kuikamilisha_

*_Malengo hayo yawe:_*

_1: Mepesi yanayotekelezeka_
_2: Muda Wa kuanza na kukamilika_
_3: Na mtu wa kukusimamia kama umetekeleza_
_4: Kufanyiwa tathmini_
_5: Jiwajibishe mwenyewe iwapo utaona umeshindwa kutekeleza_

سبحانك اللهم و بحمدك اشهد ان لااله الا انت استغفرك واتوب اليك
 
*﴿ ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ ﴾*

_*MIONGONI MWA NASAHA MUHIMU KABLA YA RAMADHANI*
[emoji843][emoji843][emoji843][emoji843][emoji843][emoji843][emoji843][emoji843]


*♡ ﻓﻲ ﺭﻣﻀــــﺎﻥ:*
*Katika Ramadhani:*

*♡ ﻧﺤﻦ ﻣﻘﺒﻠﻮﻥ ﻋﻠﻰ ﺷﻬﺮ ﻋﻈﻴﻢ ﺃﻻ ﻭﻫﻮ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ.*
_Sisi umetukaribia mwezi wenye ubora. Enyi fahamuni nao ni mwezi wa ramadhan._

*♡ ﻭﻣﺎ ﺃﺩﺭﻙ ﻣﺎ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ ...؟*
_Kipi cha kukujuza ni nini mwezi wa ramadhani?_

*♡ ﺷﻬﺮ ﺍﻟﺒﺮ واﻹحسان.*
_Nimwezi wa kufanyiana wema na ihsani._

*Allah ﷻ Anasema:*

{لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ}
```KABISA HAMTAFIKIA wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda. Na kitu chochote mnacho kitoa basi hakika Mwenyezi Mungu anakijua.``` (3:92)

*♡ ﺷﻬﺮ ﺭﻣﻀﺎﻥ ﺷﻬﺮ ﺍﻟﺘﺴﺎﻣﺢ..*
_Mwezi wa ramadhan ni mwezi wa kusameheana (kwa waliyo kosana)_

*♡ ينبغى على المسلم أن ﻳﺘﺤﻠّﻰ ﺑﺎﻷﺧﻼﻕ الكريمة.*
_Yatakikana kwa muisilamu ajipambe na tabia nzuri._

*♡ ﻭﻳﻌﺎﻣﻞ ﺍﻟﻨﺎﺱ ﻣﻌﺎﻣﻠﺔ ﺣﺴﻨﺔ، ﻭﺇﺫﺍ ﺃﺧﻄﺄ ﺍﻟﻤﺴﻠﻢ ﻓﻲ ﺣﻖ ﺃﺧﻴﻪ ﻧﺪﻡ ﻋﻠﻰ ﺫﻟﻚ ﻭﺳﺎﺭﻉ ﺑﺎﻻﻋﺘﺬﺍﺭ ﺇﻟﻴﻪ.*
_Na awafanyiye watu muamala ulo mzuri kabisa, Na pindi akoseapo katika haqqi ya nduguye ajute juu ya hilo na akimbiliye kumtaka udhuru na (msamaha)_

*♡ ﻻ ﺗﻨﺴﻰ ﺍﻟﻔﻘﺮﺍﺀ واليتامى والمساكين واﻷرامل فى رمضان.*
_Usiwasahau mafuqara, mayatima, masikini, wajane (kuwasaidia) zaidi katika mwezi wa ramadhani._

*Allah ﷻ Anasema:*

*{إِنْ تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِيَ ۖ وَإِنْ تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ ۚ وَيُكَفِّرُ عَنْكُمْ مِنْ سَيِّئَاتِكُمْ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ}*
```Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.``` (2:272)

*♡ ﺍﺣﺬﺭ ﻣﻦ ﺍﻹﺳﺮﺍﻑ ﻓﻲ ﺍﻟﻤﺎﻝ والطعام ﻭﻏﻴﺮهما، ﻓﺎﻹﺳﺮﺍﻑ ﻣﺤﺮﻡ.*
_Tahadhari kufanya israfu katika mali na chakula pia vitu vinginevyo, kwani israfu imeharamishwa._

*Allah ﷻ Anasema:*

*{وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِين..}*
```Na kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye(Allah) hapendi wanao fanya israfu.```
(Al aarafu 31)
[emoji810][emoji810][emoji810][emoji810][emoji810][emoji810][emoji810][emoji810]

*WEKA MKAKATI WA KUFANYA KILA YALO MAZURI UFIKAPO MWEZI WENYE KHERI NA FADHILA NYINGI.

[emoji92]Itaqillaha Ayuhal Ghafil[emoji92]
 
Back
Top Bottom