Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

mkuu hayo maneno umefanya nimkumbuke Iman Petro( Mungu amrehemu)
ipo debate moja alikuwa anawapiga jamaa zetu pentagoni,kama utahitaji video nnayo ntakurushia
Hebu nirushie mkuu nipate kuiona mkuu..
 
Assallam Allaykum warhmatullah wabarakatuh"
Ama kwa hakika hatuna budi kukushkuru wewe muumba wa hii dunia"
Tunakushkuru kwa kutuwwzesha kuiona tena siku ya Leo tukiwa katika ardhi yako tukufu"
Tunakuomba Yaa Rabbi utulinde na utuongoze katika kuitekeleza vyema ibada hii tukufu na nyenginezo"
"Ramadhan Kareem "
 
kalenda ya kufunga na kufungua wakuu tuwekeeni hapa
IMG-20170601-WA0003.jpg
 
Assalaam alaykum. amesema Allah, "Mmehalalishiwa usiku wa kufunga Swiyaam kujamiiana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. Allaah Anajua kwamba nyinyi mlikuwa mkijifanyia khiyana nafsi zenu, hivyo Akapokea tawbah yenu na Akakusameheni. Basi sasa waingilieni na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe (mapambazuko) wa Alfajiri kutokana na uzi mweusi (wa kiza cha usiku). Kisha timizeni Swiyaam mpaka usiku. Na wala msiwaingilie hali ya kuwa nyinyi wenye kukaa i’tikaaf Misikitini. Hiyo ni mipaka ya Allaah basi msiikaribie. Hivyo ndivyo Allaah Anavyobainisha Aayaat (na hukmu) Zake kwa watu wapate kuwa na taqwa." baqara 187.
muda wa mwisho kula daku ni wakati kunapoanza kupambazuka au wakati wa adhana ya alfajiri ya kweli (coz adhana hii huadhiniwa panapoanza kupambazuka.- japokuwa baadhi ya waadhini hawaangalii kupambazuka wanategemea hayo makalenda. jifunze namna ya kuangalia ufanye mwenye coz kaburini utaingia peke yako wala hakuna yeyote atakae kubebea mzigo wako-) kama Alivyoeleza Allah katika aya hapo juu na muda wa mwisho ni pale jua litakapozama, na huwezi kukadiria muda wa masiku yajayo kama wafanyavyo watu wengi coz hilo jua wala kupambazuka hukupaona bali utakua unabahatisha tu na katika mambo ya dini hayahitaji shaka wala kubahatisha bali uwe na yakini, na ukitaka kuhakikisha hilo fuatilia hiyo aya kisha ifanyie kazi kama walivyoifanyia maswahaba ambao ndio watu bora ambao Allaah kawaridhia kisha angalia na hilo jedwali lenu alaf uangalia kama watapatia yote. na bila shaka muongozo wa Allah na mtume wake ni bora kwetu kuliko juhudi za wale wenye kutaka kuipendezesha dini hii hali ya kuwa hawakupewa fursa hiyo Allah anasema "leo hii nimekukamalishieni kwenu nyinyi dini yenu". bila shaka kitu kilicho kamili hakihitaji nyongeza wala mbwembwe zozote zile, fanya yale uliyoamrishwa nayo ni mengi huwezi kuyatekeleza yote, vp leo ujiongezee wakat hata haya ujayamaliza??? loo! utapasuka....
hayo tu ndugu zangu nisije andika sana alafu msielewe. pamoja sana, tafadhalini msinichoke.
NB. DINI NI KUNASIHIANA.
 
Kiukweli mimi napenda sana nizungumzie ama nichangie kulingana na Dini yangu kwani waislamu huwa tunaaambiwa na Mola wetu kwamba:

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ

"Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu". [Ash-shuraa aya ya 10]

Pili niseme kwamba mwanaume yyte wa kiislamu anaemruhusu mkewe kufanya kazi hizi za Saloon huyo ni Muislamu Jina sio Muislamu anaeijua dini. Mtume (Swallah Allaahu alayhi wasallam) anasema: "Al-Mar'at Khawra" kwa maana "mwanamke ni Uchi".

Na Allaah akasema:

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ

"Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake......" [Al-Imraan aya ya 14].

Mwanamke ni pambo la mume sio la kila mtu wewe mwanamke wa kiislamu unaejiheshimu utakwendaje saloon ukaanza kuwapapasa wanaume, je wajua kwamba jinsi gani wanavyojihisi. Na ndio maana unakuta wengine vichwa vyao pengine para ila watakwenda kwa ajili ya Massage tu basi.

Tuelewe dada zangu na mama zangu haya yanatakiwa afanyiwe mume ndani huna mume wacha usijitie madhambi. Duniani tunapita hatupo hapa kuridhisha watu ama kutafuta mamali na kujiridhisha tuna mali kiasi gani. Mungu yupo siku zote sio kwamba yupo pale muda unapopatwa na tatizo ama kufiwa na kipenzi chako.

Tambueni "AHADI PEKEE AMBAYO HAINA RATIBA NI KIFO" Hujui muda gani na wapi kitakujia. Allaah mtukufu anasema:-

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ

"Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda" [Al-Hashr aya ya 18]

Na akasema tena katika Suuratul Taa-Haa aya ya 123 hadi 126

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ

".....Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika"

وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ

"Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu".

Huyu atakaefufuliwa kipofu atasema kumwambia Allaah azza wajallah.

قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرْتَنِي أَعْمَىٰ وَقَدْ كُنتُ بَصِيرًا

"Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?"

Na Allaah mtukufu atamjibu

قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتْكَ آيَاتُنَا فَنَسِيتَهَا ۖ وَكَذَٰلِكَ الْيَوْمَ تُنسَىٰ

"...Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika leo unasahauliwa".

Kutaabika kwenyew ndio huko mara ndoa zimevunjika, mara unaziniwa na mwanaume huyu kesho huyu, mara akija huyu umemshika hapa siku mbili tatu utamsikia kwamba [HASHTAG]#HEDHI[/HASHTAG] hapati au anapata kwa shida mpaka achomwe [HASHTAG]#MASINDANO[/HASHTAG] haya yote ni kw7bu hatutaki kuenda sambamba na amri za Muumba wetu. Pumzi zinatuhadaa mpaka tunamuona Allaah mtukufu si chochote si lolote. Wengine waliokuwa na imani dhaifu husema hakuna maisha baada ya kufa kwnini wewe ulianza ukiwa maiti tumboni mwa mama yako na sasa unaishi. Usijidanganye. Mwanamke mwema ni yupi?
[emoji673]Mwanamke mwema ni yule anaetulia kwake. Allaah kahimiza haya kwa kusema:

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ

"Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani......."
[emoji673]Mwanamke mwema ni yule anaehifadhi tupu yake ila kwa mume wake tu.
[emoji673]Mwanamke mwema ni yule anaeheshimu mipaka ya ndoa yake na kumtwii muumba wake.

Wengi wa wanawake wataingia Motoni kw7bu ya:
[emoji267]Kukithirisha Mambo ya laana.
[emoji267]Kutokumbuka Ihsaan na Fadhila za waume zao hata wafanyiwe mema kiasi gani.
[emoji267]Kushughulishwa na Starehe za dunia.

Waume majumbani iwapo tutawaachia wake zetu kuyafanya haya tujiandae na moto ambao hata uwe shabbab kiasi gani hutouweza kwni haiwi mvuke wa moto wa duniani wakushinda kuvumilia je Akhera utaweza. Allaah azza wajallah anasema:

( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ )

التغابن (14) At-Taghaabun

"Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu. Basi tahadharini nao..."

Maneno haya Allaah mtukufu katwambia sisi wanaume haina maana maadui kw7bu wana silaha lah ila tukishindwa kuwalea wake na watoto wetu katika misingi ambyo Allaah azza wajallah anataka basi akhera watakuwa maadui wakubwa na huenda tukaingia motoni kw7bu yao.

Kiufupi hili suala ni HARAMU na mimi sioni haja mama zetu kwenda saloon wakajidhalilisha. Niseme tu

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

"Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri".

Na Allaah Ni Mjuzi Zaidi.
(Al-Kamaalu Lillaah)
 
منهج الأنبياء:

[emoji257]DUA YA QUNUUT[emoji257]

Qunuut kwa maelezo ya Fuqahaa (wanachuoni wa fiqh), ni du'aa inayosomwa katika Swalah katika sehemu maalum wakati mtu anapokuwa amesimama baada ya kurukuu (au kabla kwenye kauli nyingine). Na inatumika katika Swalah ya witr kwenye raka'ah ya mwisho baada ya kurukuu kwa kauli yenye nguvu.

Qunuut ni du'aa itumikayo wakati wa matatizo, majanga na maafa yanapowafika Waislam. Na wakati huo ndipo du'aa hii huombwa na huwa inaombwa katika kila Swalah na si Swalah ya alfajiri tu kamailivyozoeleka na baadhi ya watu kwa kutumia baadhi ya hadiyth ambazo hazijasihi kuhusiana na Qunuut ya kudumu (katika Swalah ya Alfajir). Du'aa hii si fardhi bali ni Mustahab, na Swalah ya mtu ni sahihi kabisa hata kama hajasoma Qunuut, na wala usiposoma Qunuut huhitaji kufanya sijdatus-sahw (sijida za kusahau) kama wanavyodhani wengine. Inapendezwa kufanywa wakati ikifikia dharura kamatulivyotaja juu. Na vilevile wakati mwingine wa kuisoma Qunuut ni wakati wa Swalah ya Witr.

Ni kinyume na Sunnah kuisoma Qunuut kwenye Swalah za asubuhi na kudumu nayo kama inavyofanywa kwani hilo halijathibiti katika hadiyth sahihi kutoka kwa Mtume (Swallah Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam).

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma du'aa hiyo wakati Maswahaba zake sabini wajuzi wa Qur-aan walipouliwa kwenye sehemu iitwayo Bi-ir Ma'uunah na Makabila ya Bani Sulaym ya Ri'il, Dhakwaan, Ussayah wakati alipowatuma kwenda kuwafundisha diniyao. Aliisoma du'aa ya Qunuut kwa muda wa mwezi mzima dhidi ya hao Wauaji. (Hadiyth ya Anas iliyopo kwenye Al Bukhaariy na Muslim).

Pia kwenye Hadiyth nyingine iliyopokelewa na Abu Hurayrah, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahi kuwaombea baadhi ya Maswahaba waliokuwa wamepotea kwa maadui, na aliomba kiasi cha mwezi kisha akaacha, na Abu Hurayrah alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwanini ameacha kuwaombea, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu,''Je,huoni kuwa washarejea?" (Al Bukhaariy na Muslim)

Hivyo, inaonyesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisoma Qunuut hiyo ambayo inaitwa Qunuut an Nawaazil kwa muda ambao yale aliyokuwa akiyaomba, yamejibiwa ndipo akaacha.

Vilevile imethibiti kuwa alikuwa akiwaombea wale waliokuwa dhaifu, wananyanyaswa na maadui na kuwa chini ya wavamizi kama hali tuliyonayo leo huko Iraq, Afghanistan, Palestina, Chechnya na kwengineko.

Imepokewa pia kuwa Abu Maalik Al-Ash'ariy alisema: "Nilimuuliza baba yangu, 'Ee baba yangu, uliswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nyuma ya Abu Bakr, 'Umar, 'Uthmaan na 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhum ajma'iyn). Je, walikuwa wakisoma Qunuut katika Swalah ya alfajiri?' Akajibu, Ee mwanangu, hili ni jambo jipya lililozushwa,'" (Imesimuliwa na wapokezi wote (watano) isipokuwa Abu Daawuud). Hakika muongozo mzuri na bora ni ule wa Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Na Qunuut inaposomwa, basi ni vizuri kusoma kwa ile shida inayoombewa kwa wakati huo; kama ni njaa au udhaifu au manyanyaso n.k., iombwe kutokana na masuala hayo, na si kusoma du'aa ile iliyozoeleka kwenye Qunuut 'Allahumma ihdiyna fiyman hadayta, wa'afina fiyman 'afayta...' Du'aa hii inawezwa kusomwa kwenye Qunuut ya witr na si kwenye Qunuut ya Nawaazil.

Na endapo utaswali nyuma ya Imaam anayesoma Qunuut katika Swalah ya Alfajiri, basi unatakiwa umfuate na Swalah yako ni sahihi, kwani kumfuata Imam ni wajibu, na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:

"Imaam amechaguliwa ili afuatwe" na akasema: "Msitofautiane na Maimaam wenu",

na pia katika Swahiyh Al-Bukhaariy amesema:

"Wanawaongoza katika Swalah; ikiwa wamepatia, (ujira) ni wenu na wao, na wakikosea, (ujira) ni wenu na (dhambi) ni zao."

Wa Allaahu A'alam

☘[emoji257]☘☘[emoji257]☘[emoji257]☘☘[emoji257]
السلام عليكم
Baada salaam, kaka kama unayo Qunuut yenyewe naomba utuwekee.
جذاك الله الهير.
 
السلام عليكم
Baada salaam, kaka kama unayo Qunuut yenyewe naomba utuwekee.
جذاك الله الهير.


Dua'a Ya Qunut


اللّهُـمَّ اهْـدِنـي فـيمَنْ هَـدَيْـت، وَعـافِنـي فـيمَنْ عافَـيْت، وَتَوَلَّـني فـيمَنْ تَوَلَّـيْت ، وَبارِكْ لـي فـيما أَعْطَـيْت، وَقِـني شَرَّ ما قَضَـيْت، فَإِنَّـكَ تَقْـضي وَلا يُقْـضى عَلَـيْك ، إِنَّـهُ لا يَـذِلُّ مَنْ والَـيْت، [ وَلا يَعِـزُّ مَن عـادَيْت ]، تَبـارَكْـتَ رَبَّـنا وَتَعـالَـيْت.


“Ewe Mwenyezi Mungu niongoze pamoja na uliowaongoza, na unipe afya njema pamoja na uliowapa afaya njema, na nifanye kuwa ni mpenzi wako pamoja na uliowafanya wapenzi na nibariki katika ulichonipa na nikinge na shari ya ulilolihukumu kwani Wewe unahukumu wala huhukumiwi. Hakika hadhaliliki uliemfanya mpenzi (wala hatukuki uliemfanya adui ) Umetakasika Ewe Mola wetu na Umetukuka


اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ سَخَطِـك، وَبِمُعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك



“Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako na kwa msamaha wako kutokana na adhabu yako, na najilinda kwako kutokana na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe”


اللّهُـمَّ إِيّـاكَ نعْـبُدْ، وَلَـكَ نُصَلّـي وَنَسْـجُد، وَإِلَـيْكَ نَسْـعى وَنَحْـفِد، نَـرْجو رَحْمَـتَك، وَنَخْشـى عَـذابَك، إِنَّ عَـذابَكَ بالكـافرين ملْحَـق. اللّهُـمَّ إِنّا نَسْتَعـينُكَ وَنَسْتَـغْفِرُك، وَنُثْـنـي عَلَـيْك الخَـيْرَ، وَلا نَكْـفُرُك، وَنُـؤْمِنُ بِك، وَنَخْـضَعُ لَكَ وَنَخْـلَعُ مَنْ يَكْـفرُك



“Ewe Mwenyezi Mungu , Wewe tu ndie tunaekuabudu, na kwako tunasali na tunasujudu, na kwako tunakimbilia na tunakutumikia, tunataraji rehema yako na tunaogopa adhabu yako, kwani adhabu yako hakuna shaka kuwa makafiri itawifikia. Ewe Mwenyezi Mungu hakika sisi tunakutaka msaada na tunakutaka msamaha na tunakusifu kwa kheri na wala hatukukufurishi na tunakuamini Wewe, na tunakunyenyekea na tunamuepuka anaekukufuru”
 
HAMASAAT

Swala ni nguzo ya pili na funga ni nguzo ya nne hakuna funga bila swala enyi waja wa Mwenyezi Mungu.

{Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na ihsani na kuwapa jamaa}, waangalie jamaa zako.. wao ni watu awla wa kuwafanyia ihsani

Ramadhan ni fursa ya umri kama Mola akikutakabalia, na katika hadithi ya Mtume SAW: "Anayefunga ramadhan kwa imani na kutaraji malipo anasamehewa dhambi zake zilizotangulia na zilizopita"

Ni adhimu ilioje athari ya dua, tafakari pamoja nami Makkah ikiwa imejaa wanaoizuru, ambapo ilikuwa ni bonde lisilo na mimea, likiwa halina mambo muhimu ya maisha, likabadilika kuwa ni tamanio la nyoyo za waumini kutokana na dua ya Ibrahim

Mtu anamezwa na samaki, na mwingine alipoteza mali watoto na afya, na watatu alidhoofika mifupa na nywele zikajaa mvi, na kila mmoja alimpelekea haja zake Mola karima, na matokeo: "tukamuitikia"

{Na kama ukijikupurusha nao kwa kutaraji rehema itokayo kwa Mola wako basi sema nao maneno laini" kama humiliki mali basi hata maneno laini na mazuri usiyazuie


Wakati una umuhimu katika maisha ya watu wema, ndiyo maana kuna sura katika qur-an tukufu zimeitwa kwa sehemu za wakati: alfajr, ad dhuhaa, al asr, allayl... basi kuwa makini katika kudhibiti wakati wako kama wewe ni mtu mwema

Sulaiman AS alikuwa ni mjuzi wa mwenendo wa dunia pale aliporuzukiwa umakinifu mkubwa juu yake, akasema: "hii ni katika fadhila ya Mola wangu ili anijaribu je nitashukuru au nitakanusha, na anayeshukuru hakika anashukuru kwa ajili ya nafsi yake

"Na tukamjaalia nuru anayokwenda nayo kwa watu" kwa kadiri ya bahati yako katika qur-an ndivyo kadiri bahati yako katika nuru. Wakati wenu uwe nuru

Ewe Mola wape shifaa wagonjwa wetu na wagonjwa waislamu na warehemu maiti wetu na maiti waislamu;
ewe Mola hakika sisi tuna wapendwa waliofariki dunia; ewe Mola tukutanishe pamoja kwenye pepo yenye neema.
Ewe Mola zihifadhi nchi zetu na zihifadhi nchi za kiislamu na waislamu.
Ewe Mola tupe amani kwenye watani zetu.
Ewe Mola tuhifadhi na fitina za siri na za dhahiri

TUAMRISHANE
MEMA

Asalaam aleikum warahmatullah wabarakatuh
 
Dua'a Ya Wakati Wa Kufungua Saumu


ذَهَـبَ الظَّمَـأُ، وَابْتَلَّـتِ العُـروق، وَثَبَـتَ الأجْـرُ إِنْ شـاءَ اللهُ

“Kiu kimeondoka na mishipa imelainika, na yamethibiti malipo Allaah Akipenda”

Imepokelewa kutoka kwa 'Abdullaah bin 'Amr bin Al-'Aasw رضي الله عنه amesema: ‘Amesema Mtume wa Allaah: “Aliyefunga wakati wa kufuturu kwake ana du'aa isiyorudishwa.”

اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ بِرَحْمَـتِكَ الّتي وَسِـعَت كُلَّ شيء، أَنْ تَغْـفِرَ لِي

“Ee Allaah hakika mimi nakuomba kwa rehema zako ambazo zimeenea kila kitu, unisamehe”
 
Hii vipi Maulamaa, inaswihi:

Bi faiza, me km siamn nahic ni editing[emoji23] [emoji23] [emoji23] .
Lkn pia km ni kweli bac haifai mana ktk shurti za swala kuna kitu kinaitwa tumaanina yn utulivu au unyenyekevu, unatakiwa kuwa na khushui na taq-wa wkt wa sala yn hapo unamuomba Mungu sasa haraka ya nn??
Sisi ndio tuna shida hebu tuwe wanyenyekevu bac tufanye ibada kwa kutaraji malipo na c kwa kuonesha watu kwamba na ww umefanya jambo fulani.
Wallahu aalam.
 
Back
Top Bottom