Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

Naam kama herufi wazitambu vzr hii hapa . Hii ni dua baada ya kumaliza kula daku.


الْحَمْـدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَنـي هـذا وَرَزَقَنـيهِ مِنْ غَـيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلا قُوَّةٍ

Una we za niandikia kwa kiswahili
 
Unaweza ukatupisha kwenye uzi wetu ukaenda kwa wagalatia wenzako.
تعلم أن تكون محترماً أخي. الذي لم تجب عليه في أي مكان قال أنه مجالاتي. يوجد هنا على المسرح أناس لا يؤمنون بوجود الله. هل أنت متأكد أن كل من ينتقدك هو مسيحي؟
 
Napenda kuwakumbusha Ibada za makumi ya Mwezi wa Ramadhaan:

1. KUMI LA KWANZA
Hili ni kumi la REHMA

Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni: YAA ARHAMA R-RAAHIMIYN

IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU

NIA YA URADI:
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na unijaze rehma zilizopo katika kumi hili la mwanzo wa ramadhwaan. Nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.

Ukijitahidi kufanya uradi huu mpaka ukamaluza kumi la mwanzo basi in shaa Allah utapata rehema zilizomo katika kumi hilo la mwanzo.

2. KUMI LA PILI
Hili ni kumi la MSAMAHA yaani kusamehewa madhambi yote yaliyopita.

Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni: ASTAGHFIRULLAAH LA'ADHWIM WA ATUUBU ILAYHI

IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU

NIA YA URADI:
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na unisamehe madhambi yangu yote niliyofanya kwa makusudi au kwa bahati mbaya naomba unipe radhi zako na msamaha wako uliopo katika kumi hili. Nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.

3. KUMI LA TATU
Hili ni kumi la kuokolewa katika moto wa JAHANNAM

Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni: ALLAHUMMA AJIRNAA MINA NNAAR SAALIMIYN

IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU

NIA YA URADI:
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na uniepushe na adhabu za duniani na adhabu za jahannam nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA NYIRADI HIZO NI[emoji1370]

1. Hakikisha unao UDHU.

2. Hakikisha unaelekea KIBLA.

3. Usikatishe uradi kwa ajili ya mazungumzo isipokua kwa dharura.

4. Chagua sehemu moja maalum ya kufanya nyiradi zako zote mpaka RAMADHAN itakapoisha. Labda itokee dharura kama KAZI,SAFARI, n.k.

5. Hakikisha baada kumaliza uradi kila siku kwa makumi yote omba dua ya shida zako na kisha mswalie Mtume (rehma na amani ziwe juu yake).

6. Muda mzuri wa kusomwa nyuradi hizi ni kabla ya kutoka adhana ya maghrib kwani muda huo ni muafaka kukubaliwa dua nyingi katika mwezi wa ramadhani. Ingawa inaruhusiwa kusoma nyuradi muda wowote.
 
Mayahudi waliolaaniwa hawana haki napo pale muda wa kuwa hawajajisalimisha kwa Allah Peke yake na wakawa Waislam. Na ndio maana walitolewa pale kwa udhalili kwa sababu pale hapapaswi kuwa sinagogi au hekalu la kufanyia ushirikina.


Halafu Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) aweze kuandika Qur'an halafu wasiweze wengine? Unajua kuna wenzio walidai hilo wakati wake Mtume wakawa challenged nao watunge kama wanaweza? Na wakashindwa japo walikuwa ni wafasaha wa lugha ya Kiarabu. Na vipi Mtume Muhammad aandike Qur'an ilhali hakuwa akijua kusoma na kuandika na wala hakuwa na historia ya kusoma? Na kama yeye Mtume ndio katunga Qur'an kwanini Qur'an haifanani na maneno yake Mtume? Kungekuwa na ufanano. Na kama kasaidiwa na wengine mbona hawakuiweza challenge waliyopewa ya kutunga nyengine mfano wake, au hata sura kadhaa au hata sura moja tu?

Qur'an ni Maneno ya Allah.

Na pia Qur'an sio kiumbe bali ni Maneno yake Allah, hayakuumbwa.

Haya nenda katafute nyuzi za kubishana. Usiharibu uzi.
Kiukweli hata ulichokijibu hakieleweki kabisa swali langu nililokuuliza ni kwamba wayahudi walikuwa wanasali wapi kabla ya Mohammad?
 
Walikuwa wanaswali Waislam. Masajid zote zipo kwa ajili ya kuabudiwa Allah peke yake.

Ila umekubali kuwa ulikuwa hujui Masjid al Aqsa ni eneo lote lile? Na hivyo kuondoa mshangao wako kuwa Mtume aliswalije wakati hakukuwa na jengo?

So, usiharibu uzi kwa kuruka ruka. Hatutaki mijadala isiyo na tija humu.
Hauwezi kujibu swali la wayahudi walikuwa wanasali wapi kabla ya Mohammad kuja?
 
Tuziangali sifa za waumini wanao mcha Allah na kumwogopa Allah kama zilivyoelezwa Katika ayah za mwanzo za suratul baqara

Aya imeanza Kwa Kusema hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na ni mwongozo kwa wale wanao mcha Allah

Kwanza wanaamini ghaibu bimaana yale yasiyoonekana kwa milango ya fahamu ya kawaida,,,, mfano Allah mwenyewe, malaika, Pepo na moto nakadhalika.

Wanasimamisha sala,,, tujitahidini sana kusimamisha swala tano kwani hii ndio nguzo ya dini, katika mfumo wa hadith Mtume rehma na amani ziwe juu yake anasema Allah ameahidi kuwasamehe wale wanao simamisha swala, na ama ambao hawaswali hakuna ahadi juu yao, ima aweza kuwasamehe au kutowasamehe,,,, na swala ndio ya kwanza kuhesabiwa siku ya kiama,,, tuizingatie.

Na sifa nyingine ni kutoa katika yale ambayo Allah ameturuzuku, Allah anasema ktk Quran si wema tu huo pekee yake kuelekea magharibi na mashariki kwa maana kuswali bali kuna wema mwingine kama hayo mambo ya kutoa kwa kutaka radhi za Allah,,,huu ni mwezi wa kuchuma basi tukisirisheni sana kutoa kwa kadri tulivyo jaaliwa ili tupate kufaulu.

Sifa nyingine ni kuamini yale akiyoteremshiwa Mtume,na yale ya kabla yake,,,, hapa ni kuamini hii Quran pamoja na vitabu vilivyo teremshwa kabla yake kwa mitume wengine kwa maana zaburi, injili na torati lkn si hivi vya leo ambavyo vimechezewa na kuingizwa maneno ambayo siyo ya Allah.

Na sifa nyingine ni kuamini siku ya mwisho, kwamba kuna kuhesabiwa na mizani, kwamba ipo siku ambayo tutalipwa kwa matendo yetu

Basi hakika waumini hawa wameongozwa katika njia iliyonyooka na hakika watapata makazi bora kabisa.
 
Nawaitu
Swaumu
Agadi

N.k

Ndo nahitaji mkuu niendikie
Bismillahi rrahmani rrahiim.
Nawaitu swawmaghadi. An-adaai min-yawmi shahar ramadhwaani. Haadhihi sana, faradhwa alayna lillahi taala, imaanan wahti saaban liwajihillahi kariim. Alhamdulillahi rabbil aalamiin.

Nafikiri ni hii uliyokuwa unaihitaji!
 
Una we za niandikia kwa kiswahili
الْحَمْـدُ للهِ الَّذي أَطْعَمَنـي هـذا وَرَزَقَنـيهِ مِنْ غَـيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلا قُوَّةٍ

Alhamdulillahi lladhii atu-amanii
Hadhaa warazaqanii min ghayri hawlin minniii walaa quwwah.
 
Bismillahi rrahmani rrahiim.
Nawaitu swawmaghadi. An-adaai min-yawmi shahar ramadhwaani. Haadhihi sana, faradhwa alayna lillahi taala, imaanan wahti saaban liwajihillahi kariim. Alhamdulillahi rabbil aalamiin.

Nafikiri ni hii uliyokuwa unaihitaji!
Perfect Mkuu thank you
 
Nina maswali kuhusu muda wa kula daku.......Kwa ratiba ya sasa jua kuchomoza ni saa 11:19 asubuhi.....Jee mwisho wa kula daku inapaswa kuwa saa ngapi??
 
Nina maswali kuhusu muda wa kula daku.......Kwa ratiba ya sasa jua kuchomoza ni saa 11:19 asubuhi.....Jee mwisho wa kula daku inapaswa kuwa saa ngapi??
Kama upo Dar, ratiba hiyo hapo
IMG-20240312-WA0001.jpg
 
Nina maswali kuhusu muda wa kula daku.......Kwa ratiba ya sasa jua kuchomoza ni saa 11:19 asubuhi.....Jee mwisho wa kula daku inapaswa kuwa saa ngapi??

Kula mpaka kuingie alfajiri ya kweli
Swali: Kulikuwa na kitambo gani kati ya daku na swalah ya Fajr?
Jibu: Wakati wa daku unatanda mpaka kuingia kwa alfajiri. Amesema (Ta´ala):
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ
“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi.”[1]
Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Ibn Umm Maktuum alikuwa kipofu na haadhini mpaka aambiwe kuwa kumepambazuka. Kwa hivyo inapendeza kuchelewesha daku.
´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy
´Abdullaah bin Ghudayyaan
´Abdullaah bin Qu´uud
[1] 02:187
Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (10/334) nr. (5611)
Imechapishwa: 24/04/2022
 
Nina maswali kuhusu muda wa kula daku.......Kwa ratiba ya sasa jua kuchomoza ni saa 11:19 asubuhi.....Jee mwisho wa kula daku inapaswa kuwa saa ngapi??
Muda huo ndio wa kupambazuka Alfajiri au ni muda wa kuchomoza Jua huko kwenu? Sijaelewa.

Kula mpaka kupambazuke Alfajiri. Huko kwenu Alfajiri inaingia saa ngapi ndugu yangu?
 
Back
Top Bottom