Tuziangali sifa za waumini wanao mcha Allah na kumwogopa Allah kama zilivyoelezwa Katika ayah za mwanzo za suratul baqara
Aya imeanza Kwa Kusema hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake na ni mwongozo kwa wale wanao mcha Allah
Kwanza wanaamini ghaibu bimaana yale yasiyoonekana kwa milango ya fahamu ya kawaida,,,, mfano Allah mwenyewe, malaika, Pepo na moto nakadhalika.
Wanasimamisha sala,,, tujitahidini sana kusimamisha swala tano kwani hii ndio nguzo ya dini, katika mfumo wa hadith Mtume rehma na amani ziwe juu yake anasema Allah ameahidi kuwasamehe wale wanao simamisha swala, na ama ambao hawaswali hakuna ahadi juu yao, ima aweza kuwasamehe au kutowasamehe,,,, na swala ndio ya kwanza kuhesabiwa siku ya kiama,,, tuizingatie.
Na sifa nyingine ni kutoa katika yale ambayo Allah ameturuzuku, Allah anasema ktk Quran si wema tu huo pekee yake kuelekea magharibi na mashariki kwa maana kuswali bali kuna wema mwingine kama hayo mambo ya kutoa kwa kutaka radhi za Allah,,,huu ni mwezi wa kuchuma basi tukisirisheni sana kutoa kwa kadri tulivyo jaaliwa ili tupate kufaulu.
Sifa nyingine ni kuamini yale akiyoteremshiwa Mtume,na yale ya kabla yake,,,, hapa ni kuamini hii Quran pamoja na vitabu vilivyo teremshwa kabla yake kwa mitume wengine kwa maana zaburi, injili na torati lkn si hivi vya leo ambavyo vimechezewa na kuingizwa maneno ambayo siyo ya Allah.
Na sifa nyingine ni kuamini siku ya mwisho, kwamba kuna kuhesabiwa na mizani, kwamba ipo siku ambayo tutalipwa kwa matendo yetu
Basi hakika waumini hawa wameongozwa katika njia iliyonyooka na hakika watapata makazi bora kabisa.