Wa anhu swallallahu alayhi wasallama annahu qaal: af-dhwalu maa qultuhu anaa wan nabiyyuna min qablii, fa-a-lam annahu "Laa ilaha Illa llah"
Amesema Mtume Muhammad s.a.w ya kuwa: Bora zaidi ya niliyosema mimi na Manabii waliyokuwa kabla yangu ni: Laa ilaha illa llah.
Na akasema Mtume Muhammad s.a.w: Unapofanya ovu basi fatilisha na jema kwani hakika ya jema hufuta ovu. Akaulizwa; Yaa rasuula llah, aminal hasanaati laa ilaha illah llah? (Ni katika jema (hii dhikr ya Laa ilaha Illa llah).
Akasema kwa kujibu Mtume Muhammad s.a.w: Hiya af-dhwalul hasanaat. Hiyo ni bora zaidi.
Kwa msingi huo wakasema wanawazuoni; "Laa ilaha illa llah, nalo ni miongoni mwa mambo makubwa yaliyo bora zaidi ambayo yanafuta maovu.
Na akasema Mtume Mtume Muhammad s.a.w wasallam: Af-dhwalu dhikr; Laa ilaha illa llah ....(mpaka mwisho wa hadithi)
Qaala Musa swalallahu alayhi wasalllam: Yaa Rabbi, allimnii shay an adhkuruka wa ad-uka bihi.
Nabii Musa alayhi ssalaam alimwomba Allah kuhusu dhikr maalumu zaidi, ambayo atakayo mdhukuru na kumuomba.
Qala llahu taala (Allah akamjibu kumwambia): Qul Laa ilaha illa llah.
Sema: Laa ilaha illa llah
Qala (akasema Nabii Musa): Kullu ibaadika yaquuluna hadha.
(Yaa Rabbi, kila mja wako analitamka hilo.
---------------
Itaendelea inshaallah!