Ramadhan Special Thread

Ramadhan Special Thread

IMG_20250302_100410.jpg
 
RAMADHAN MWEZI WA TWAA NA IBADA

Alhamdulillah khatimae tumeidiriki ramadhani msimu wa ibada na twaa

ALLAH AWABAARIK NYOTE KWA KUUPATA MWEZI HUU WENYE BARAKA TELE

ikiwa katika mji kuna msimu wa biashara au mavuno basi watu husika wa msimu huo huusubiri kwa mipango madhubuti na imara na kila muhisika atakae zembea kusimamia mipango yake kuonekana hana mana wala umakini na hayupo sawa kwani huenda msimu ujao asiudiriki

kwetu sisi ni zaidi ya msimu tupo katika nyakati za kutafuta radhi na msamaha wa mola mlezi ni jukumu la kila mmoja wetu kusimamia dhamira zake na athibiti katika mipango yake

UMEUANZA VIPI MSIMU HUU WA TWAA NA IBADA ?

Katika kutafuta ujira wa kumaliza quraan mara nne ndani ya mwezi huu ukiwa ndio mpango wetu leo tumesoma juzuu 4 je umeifikia dhamira hii

kwa wale ambao hawana uwezo wa kusoma quraan yote soma kiasi unachoweza kusoma pamoja na kurejea rejea hicho hicho kidogo kwa nia ya kusoma juzuu 4 kwa siku

Niwatakie mwezi wenye baraka kwenu na familia zenu na muwe na swaumu njema yenye uchangamfu wa ibada namuomba Allah atujaalie ikhlaswi katika juhudi zetu na atukubalie juhudi zetu chache tuzifanyazo

Abu fat'hiya khamis kiza
 
Kuna demu wangu muislam kasema tufunge wote na tusilombane hadi ramazani iishe je yuko sahihi au ananizingua tu.
 
Ndio unaweza lakini haitahesabika kama unafanya Ibada na kupata ujira wa funga kwani Moja wapo la sharti la kukubaliwa kwa ibada ni lazima mtu awe Muislamu.
Kumbe muhammad ni muongo kuwa manaswara wa kweli ni waislamu
 
RAMADHAN MWEZI WA TWAA NA IBADA

Alhamdulillah khatimae tumeidiriki ramadhani msimu wa ibada na twaa

ALLAH AWABAARIK NYOTE KWA KUUPATA MWEZI HUU WENYE BARAKA TELE

ikiwa katika mji kuna msimu wa biashara au mavuno basi watu husika wa msimu huo huusubiri kwa mipango madhubuti na imara na kila muhisika atakae zembea kusimamia mipango yake kuonekana hana mana wala umakini na hayupo sawa kwani huenda msimu ujao asiudiriki

kwetu sisi ni zaidi ya msimu tupo katika nyakati za kutafuta radhi na msamaha wa mola mlezi ni jukumu la kila mmoja wetu kusimamia dhamira zake na athibiti katika mipango yake

UMEUANZA VIPI MSIMU HUU WA TWAA NA IBADA ?

Katika kutafuta ujira wa kumaliza quraan mara nne ndani ya mwezi huu ukiwa ndio mpango wetu leo tumesoma juzuu 4 je umeifikia dhamira hii

kwa wale ambao hawana uwezo wa kusoma quraan yote soma kiasi unachoweza kusoma pamoja na kurejea rejea hicho hicho kidogo kwa nia ya kusoma juzuu 4 kwa siku

Niwatakie mwezi wenye baraka kwenu na familia zenu na muwe na swaumu njema yenye uchangamfu wa ibada namuomba Allah atujaalie ikhlaswi katika juhudi zetu na atukubalie juhudi zetu chache tuzifanyazo

Abu fat'hiya khamis kiza
Huu ndiyo wasaa wa waislamu kula hadi kubeuwa....tusishangae vyakula kupanda bei mara dufu hawa waisiharamu siyo waislamu wao wanabadili tu muda wa kula ila wanakula zaidi ya mara dufu ya wanavyokula miezi isiyo ya Ramadhan
 
Ndugu zetu Waislam....
Mkiwa mpo mnaendelea na Ibada hii ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mkumbuke kuwa kuna Mambo mnatakiwa mjiepushe Nayo.
Kama:-

1.Tabia Mbaya na maneno maovu Mfano wa kusengenya, kusema uongo n.k (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

2.Kulala sana kwani kulala huko kunatupotezea Fursa za kufanya Ibada ya Kusoma Qur an na Ibada Nyenginezo (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).

3.Kupoteza wakati mwingi katika michezo na maongezi yasiyo na faida Vijiweni.
Kwa.....
Kucheza Bao, karata na kuacha kuutumia wakati huo katika kazi na ibada mbali mbali Mfano kuhudhuria Darsa Misikiti kipindi cha Swala ya Alasiri au kwa Mujibu wa Ratiba za Masheikh wasimamizi wa Darsa hizo (Mwezi huu sana na baki ya miezi ).
 
Shukrani mkuu kwa ukumbusho mzuri , ni sahihi kabisa hayo.
 
Huu uzi umejaa madini tupu .

Maswali muhimu karibia yote yamejibiwa kupitia huu uzi
 
Back
Top Bottom