Ramadhani Brothers waibuka washindi shindano la America's Got Talent Fantasy League, wanyakua Tsh milioni 637

Ramadhani Brothers waibuka washindi shindano la America's Got Talent Fantasy League, wanyakua Tsh milioni 637

Wanasarakasi Kutoka Tanzania @ramadhanibrothersofficial 🇹🇿 wamefanikiwa Kuibuka washindi kwenye shindano la America’s Got Talent: Fantasy League Na Kujishindia PESA Kiasi Cha Dola $250,000 Ambazo Ni Sawa Na Tsh Milioni 637/=

Ramadhan Brothers wanaweka historia ya kuwa Waafrika wa kwanza toka Afrika kuwahi kushinda shindano hilo La AGT (America Got Talent: Fantasy League
 
Hongera zao, waendelee kujituma

Ila pamoja na yote hilo fungu la usd250000 Ni dogo san kwa watu wawil wakigawan hamn ktu
 
Kwa hakika Rais Samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge anastahili pongezi kubwa sana kwa ushindi wa vijana hawa kutokana na namna ambavyo ameleta hamasa kubwa sana katika michezo ,ambapo imepelekea vijana kuongeza ubunifu na hamasa kubwa sana katika michezo .

Imepelekea vijana kuongeza mazoezi na kujituma kwa hali ya juu sana.hii ndio maana tunaona vijana hawa wakirudisha ushindi nyumbani.
Umesahau kuweka namba ya simu
 
Mnasahau hata kuwataja kwa majina yao hawa vijana mnamtaja mama ila dhambi mnazo mliona namna walivyo hatarisha maisha yao? Hata motoni hamuendi
 
Hongera kwao. Walete sasa hayo mahela home tuchangie pato la taifa. Tozo ni muhimu sana.
 
Wanasarakasi wawili kutoka Tanzania kwa jina Ramadhan Brothers wameibuka washindi katika mashindano ya American Got Talent.

Wawili hao wanaoshirikisha Fadhili Ramadhan na Ibrahim Jobu, walishinda taji hilo Jumatatu usiku.

Waliwashinda wapinzani wao wakuu Pack Drumline, V. Unbeatable, Sainted na Musa Motha.

‘Tunaamini Maisha yetu yanabadilika kuanzia wakati huo’, Ramadhan alinukuliwa na jarida la US Today akisema. ‘’Ushindi huu una maana kubwa kwetu, tuna furaha sana isio na kifani’’.

Kwa mujibu wa US Today, ushindi huo wa tuzo ya AGT ni safari ya miaka miwili ya vijana hao wawili.

Ramadhani Brothers walipanga kufanya majaribio ya "AGT" Msimu wa 17, lakini Jobu hakuweza kupata visa yake ya kusafiri kwa wakati.

Kwa muda, wawili hao walionekana kwenye mfululizo kadhaa wa "Got Talent", ikijumuisha "Australia's Got Talent," "Got Talent España" na "Românii au talent," ambayo ilianzisha jukwaa lao la kwanza la "AGT" Msimu wa 18.

Katika shindano hilo Ramadhani Brothers waliwashangaza waamuzi kwa onyesho linalohusisha mwanasarakasi mmoja kusawazisha uzito wa mwili wa mwenzake kichwani huku wakipita seti tofauti.

Hatahivyo licha ya kuingia fainali kama wahitimu wakuu, walipoteza kwa mshindi wa Msimu wa 18 Adrian Stoica & Hurricane.

Credit : BBC

14b16f1a-de11-4131-84e6-db1fad276491.jpg
 
Nakipongeza chama cha mapinduzi serikali ya mama pia bunge letu kwa ushindi mkubwa duniani na rekodi ya kipekee ya ramadhani brothers
 
Kwa hakika Rais Samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge anastahili pongezi kubwa sana kwa ushindi wa vijana hawa kutokana na namna ambavyo ameleta hamasa kubwa sana katika michezo ,ambapo imepelekea vijana kuongeza ubunifu na hamasa kubwa sana katika michezo .

Imepelekea vijana kuongeza mazoezi na kujituma kwa hali ya juu sana.hii ndio maana tunaona vijana hawa wakirudisha ushindi nyumbani.
kumekucha!ahahha
 
Ramadhani Brothers kutoka Tanxania wameibuka washindi kwenye shindano la America's Got Talent Fantansy League na kujinyakulia kitita cha dola 250,000.

Kwa ushindi wao wanaweka historia ya kuwa Waafrika wa kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda shindano hilo.

Piga theluthi kodi hapo

Kata pesa za promota, maneja nk
 
Back
Top Bottom