Ramadhani Brothers waibuka washindi shindano la America's Got Talent Fantasy League, wanyakua Tsh milioni 637

Ramadhani Brothers waibuka washindi shindano la America's Got Talent Fantasy League, wanyakua Tsh milioni 637

Sisi kama wizara ya michezo na utamaduni tunatoa pongezi za dhati kwa serikali ya Awamu ya sita chini ya Dr Mama Mbeba maono SSH Kiongozi shupavu na mtetezi wa wanyonge kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana wa kitanzania kama Ramadhani brothers kujishughulisha kwenye michezo nakujipatia kipato.

kwako Lucas mwashambwa
mnasifia hadi mnaharibu.
 
Ramadhani Brothers kutoka Tanxania wameibuka washindi kwenye shindano la America's Got Talent Fantansy League na kujinyakulia kitita cha dola 250,000.

Kwa ushindi wao wanaweka historia ya kuwa Waafrika wa kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda shindano hilo.

Congratulations Brothers.

Hii ni kubwa sana.

Tupac Never lose Hope
 
Wasubiri kutumika kisiasa, ikijulikana siku ya kurudi nyumbani watapokelewa airport na kufikia Ikulu ya Dar, then the next day kwenye mhimili wa bunge, na wakishangaa hata ule mhimili mwingine utawaalika..hahahaha.....

Walijiandaa sana kupitishia mambo yao ya kisiasa kwa Taifa stars bila kujua kwamba uwezo wa timu yetu uko chini, limebuma hata walivyorudi hatukujua wala hawakuhangaika kuwapokea na kuwatia moyo kwamba tuanze sasa maandalizi mengine, so kitu ambacho hakina manufaa kwa siasa zao huwezi waona hawa watu.
 
Ramadhani Brothers kutoka Tanxania wameibuka washindi kwenye shindano la America's Got Talent Fantansy League na kujinyakulia kitita cha dola 250,000.

Kwa ushindi wao wanaweka historia ya kuwa Waafrika wa kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda shindano hilo.

Safi kabisa wameitangaza nchi kuliko hata royal tour
 
Sisi kama wizara ya michezo na utamaduni tunatoa pongezi za dhati kwa serikali ya Awamu ya sita chini ya Dr Mama Mbeba maono SSH Kiongozi shupavu na mtetezi wa wanyonge kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana wa kitanzania kama Ramadhani brothers kujishughulisha kwenye michezo nakujipatia kipato.

kwako Lucas mwashambwa
Kwa hakika Rais Samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge anastahili pongezi kubwa sana kwa ushindi wa vijana hawa kutokana na namna ambavyo ameleta hamasa kubwa sana katika michezo ,ambapo imepelekea vijana kuongeza ubunifu na hamasa kubwa sana katika michezo .

Imepelekea vijana kuongeza mazoezi na kujituma kwa hali ya juu sana.hii ndio maana tunaona vijana hawa wakirudisha ushindi nyumbani.
 
Wasanii wa sarakasi kutoka Tanzania Ibrahim na Fadhili Ramadhan wanaounda kundi la The Ramadhan Brothers wameibuka Washindi wa mashindano ya kusaka vipaji ya ‘America’s Got Talent Fantasy League’, usiku wa kuamkia leo Nchini Marekani na kujinyakulia $250,000 (Tsh milioni 637.5) pamoja na tuzo ya kwanza ya msimu huu wa mashindano hayo.

Mashindano ya ‘America’s Got Talent’ yalianza rasmi mwaka 2006 ambapo dhamira yao kubwa ilikuwa ni kusaka vipaji kwenye nyanja mbalimbali Marekani kabla ya baadaye kupanua wigo na kuvisaka vipaji vya maeneo mbalimbali Duniani.

Kwa mwaka huu 2024 mashindano hayo yamefanyika kwa utofauti kidogo, kutokana na Majaji kupewa nafasi ya kuwarudisha Washiriki waliopita katika misimu iliyopita kisha kuwapatia nafasi ya kushindanishwa upya ili kuwania kitita cha $250,000 pamoja na tuzo.

Ramadhani Brothers walishiriki katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza mwaka 2023 kwenye msimu wa 18 wa America’s Got Talent wakishika nafasi ya 5 na ikimbukwe kuwa haya sio mashindano ya kwanza kwa Ramadhani Brothers kushiriki kwenye safu ya kimataifa kwani walishiriki kwenye mashindano Nchini Ujerumani, Slovakia, Ufaransa , Australia pamoja na Marekani.

Credit - AyoTv
 
Kwa hakika Rais Samia mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge anastahili pongezi kubwa sana kwa ushindi wa vijana hawa kutokana na namna ambavyo ameleta hamasa kubwa sana katika michezo ,ambapo imepelekea vijana kuongeza ubunifu na hamasa kubwa sana katika michezo .

Imepelekea vijana kuongeza mazoezi na kujituma kwa hali ya juu sana.hii ndio maana tunaona vijana hawa wakirudisha ushindi nyumbani.
Wakuu tayali hukuu kumekucha 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom