Ramadhani Singano amwaga wino Azam FC

Azam Bhana! Hebu Angalieni Kwa Umakini Sana Simu Ya Huyo Kiongozi Wa Azam Aliyevaa Kofia ILIVYOCHOKA Na KUCHAKAA. Halafu Tunaambiwa Eti Ni Timu Ya Matajiri. Hata Mimi Ngumbaru ( Masikini ) Siwezi Kuwa Na Simu Ya Hovyo Iliyolika / Kuchakaa Kila Pembe.

Mkuu GENTAMYCINE heshima kwako,simu yake usikute ina air time yenye thaman ya simu yako teh teh teh
 
Last edited by a moderator:
Sawa mkuu ili kujikomboa kimaisha ila kumbuka kipaji chake ndiyo kazi yake

Kwa hivyo kipaji kinakua ukicheza simba pekee....hata bila kucheza mechi za kimataifa kama za Klabu Bingwa Africa....... .?
 
Kwa hivyo kipaji kinakua ukicheza simba pekee....hata bila kucheza mechi za kimataifa kama za Klabu Bingwa Africa....... .?

Mkuu tuvute subira msimu wa kwanza ukiisha tutajua huyu dogo kafikia wapi
 
Azam nao siku hizi ni kuchukua tu watu wa simba na yanga, si ajabu mpira wao umeshuka!
 
Mkuu tuvute subira msimu wa kwanza ukiisha tutajua huyu dogo kafikia wapi

Kwani alivyo kuwa simba sports club ndani ya misimu 2 alikuwa anaonyesha improvement yeyote.?

Singano ni wa kawaida sana,binafsi sitegemei kwamba hata angebaki simba kuna msimu angekuwa TopScorer wa VPL...!
 
Mkuu tuvute subira msimu wa kwanza ukiisha tutajua huyu dogo kafikia wapi

Kapombe alipoondoka tukajua tutapata wapi beki mzuri . Kapatikana Kessy mtu wa kazi hatumkumbuki tena Kapombe hivyo hata Messi tutapata tu replacement yake make Tanzania ina vipaji kibao huwezi amini. Tumwache kijana akaone challenges kwingine.SIMBA WILL GO ON EVEN WITHOUT MESSI. alikuwa hajafikia hata kiwango cha STEVEN MAPUNDA , msiumize vichwa
 
Azam nao siku hizi ni kuchukua tu watu wa simba na yanga, si ajabu mpira wao umeshuka!

Ushuke Mara Ngapi?

Wewe Unaona Wana AKILI Hao? Sasa Tega Sikio Usikie Tamko La Simba Weekend Hii Ambapo Litatoka Azimio La Wana Simba Wote Nchi Nzima Kugomea Products Zozote Za Azam Na Nadhani Kwa Hatua Hiyo Tutaheshimiana Hapa Mjini.

Na Mnaokumbuka Hii Haitakuwa Mara Ya Kwanza Kwa Simba Kufanya Hivi Kwani Kipindi Kile Radio One Kupitia Maulid Kitenge Walipotukorofisha Simba Aden Rage Alituasa Wana Simba Wote Kuacha Kutumia au Kununua Products Zozote Zile Za IPP Media Na Kwakweli Tulifanikiwa Hadi IPP Wakaomba Po Kwa Simba Kwani Walipata Hasara Kubwa Mno Haswa Ukizingatia Kuwa Watanzania Wengi Matajiri Ni Mashabiki Wa Simba Tu Hapa Nchi Huku Wa Yanga Wakiishia Kugongea Tu Na Kudoea Kwa Wana Simba Majumbani Mwao.
 
AMEPEWA 50milioni na mshahara wake utakuwa milioni 2 kwa mwezi amesaini mkataba wa miaka miwili

Kwa hela hiyo, mikia wangesaini wawili wa kuwakopa usafiri, pango na nusu ya ada ya usajili.
 

Azam wadhamini wa Simba. Halafu kuna Azam kampuni na Azam timu ya mpira. Sasa ukigomea Azam Cola ya kampuni kwa masuala ya kimpira huoni itakuwa ni kuchanganya madesa?
 
Azam wadhamini wa Simba. Halafu kuna Azam kampuni na Azam timu ya mpira. Sasa ukigomea Azam Cola ya kampuni kwa masuala ya kimpira huoni itakuwa ni kuchanganya madesa?

Mkuu,hivi unapoteza muda kumjibu jamaa yetu huyo?
 
Hagomewi mtu hapa ila Messi amekosa ushauri mzuri

Huyu dogo tusimfanye topic of a week. Sema mtu tutakaye mmisi ni Okwi ambaye Tayari amekabidhiwa jezi namba 25 na klbu yake mpya Denmark!
 
na tukienda kutetea kombe letu Unguja tutapanda boti gani kma sio zao jamaa
 
Kuna mtu povu linamtoka kweli kweli kakasirika haswaaa anatamani amkate RS amtafune mbichi teheee teheee ila nacheka zaidi wanapoamua kukataa kua hawamtambui kwa jina la Messi mara baada ya kuhamia Azam.
Etiiiii.....??watagomea bidhaa za Azam tunasahau kua mama,dada na shangazi zetu ni wauza maandazi wapi watanunua ngano au wafe njaa kisa SSC duh kuanzia viongozi mpaka mashabiki wanafanana aseee natamani nimsikie Manara aseme wagomee product za Azam ila mkumbe kuna Azam Tv na mpunga wao wa udhamini mnautaka sana.
 
Sawa mkuu ili kujikomboa kimaisha ila kumbuka kipaji chake ndiyo kazi yake
sasa kipaji bila hela kina faida gani? mwacheni akachukue mpunga dogo, ulishasikia mtu anaondoka azam huku anadai pesa yoyote?
 
sasa kipaji bila hela kina faida gani?

Kweli hakina faida, ila anajichimbia kaburi la kipaji chake

mwacheni akachukue mpunga dogo, ulishasikia mtu anaondoka azam huku anadai pesa yoyote?

Kama malengo yake ni hela tu bila kukuza kipaji chake na kufikia sehemu tukamsifu kama Samata namuunga mkono
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…