Nitakutafuta unipe ramani kwa vigezo nitakavyovitaja. Najua kwenye ramani ndio itazaa makadirio na ushauriRamani, Makadirio, na Ushauri tuwasiliane
Bado offer ya punguzo la bei inaendelea mpaka tarehe 15/02/2024
Ndio ndg, karibu sana. Mungu akufanyie wepesi katika dhamira yakoNitakutafuta unipe ramani kwa vigezo nitakavyovitaja. Najua kwenye ramani ndio itazaa makadirio na ushauri
Ngoja niendelee kuvuta pumzi kidogo
Mafundi wengi wanatumia pipe level kwenye kozi ya mwisho (mfano kama msingi una kozi 7, basi ile kozi ya 7 ndio wanaitafutia level). Sasa kuna muda inatokea upande mmoja unadai udongo mwingi (mortar thickness) ili kufikia level ya upande mwingine hivyo inashauriwa utumie pipe level angalau katika kozi mbili kabla ya kuifikia ile kozi ya mwisho ili in case kama kuna upande utadai udongo mwingi uweze kubalance katika hizo kozi kuliko kurundika udongo sehemu moja katika kozi ya mwisho
Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
Pipe level ni kibomba chembamba (kina urefu wa kama mita 15) ambacho kinatumika kutafutia level ya sehemu (point) mbili tofauti. Kwenye hicho kibomba huwa tunaweka maji (unachanganya na rangi ya chakula kidogo kwenye maji ili iwe rahisi kuona maji yanavyoshuka na kupanda kwenye hicho kibomba).Mkuu samahani, nini maana ya pipe lever?
Pipe level ni kibomba chembamba (kina urefu wa kama mita 15) ambacho kinatumika kutafutia level ya sehemu (point) mbili tofauti. Kwenye hicho kibomba huwa tunaweka maji (unachanganya na rangi ya chakula kidogo kwenye maji ili iwe rahisi kuona maji yanavyoshuka na kupanda kwenye hicho kibomba).
Upande mmoja wa hicho kibomba unaushikilia, huku upande mwingine unakuwa unaupandisha/kuushusha kufuata level ya upande ambao umeshikiliwa, maji yakitulia maana yake hizo pande mbili za bomba maji yanapoishia zipo ktk level moja kwa hiyo unaweka alama zako then unaendelea kutafuta level upande mwingine kwa kutumia hizo point ambazo tayari zipo level View attachment 2933217
Duu noma sana.Ndg yangu mmoja alipewa quotation ya vifaa vya umeme na fundi wake, basi akaona anishirikishe na mimi kuhusu hiyo quotation aliyopewa. Nikaiangalia ile quotation, nikamuambia huyu jamaa yangu anitumie na ramani yake. Nikapiga mahesabu nikaona kwamba fundi amezidisha vifaa ktk item zote karibu mara mbili ya uhalisia.
Nikamtumia quotation yangu niliyompigia hesabu, nikamuambia mwambie fundi aanze na hivyo vifaa kwanza vikipelea utamuongezea vingine maana alikuwa ameshampa advance kabla hajaanza kazi (mimi sikutaka nitubue mipango yao). Fundi akaangalia vile vifaa alivyoletewa, akawa amestuka kwa hivyo akahisi labda kuna fundi mwingine aliitwa pale site apige tena mahesabu ya vifaa. Baada ya fundi kuviangalia na kuhesabu akamuambia huyo boss kwamba hivi vinaweza vikatosha lakini, ngoja tuangalie. Kazi ikafanyika mpaka ikaisha,ikawa hakuna kilichopelea. Sasa swali ni kwamba vile vifaa vinavyozidishwa kwa makusudi na fundi huwa wanaviibaje?
Hapo kuna option mbili, ukimpa hela akanunue vifaa atakata hela huko huko na ukinunua mwenyewe vifaa alivyokupigia hesabu, hivi ilivyozidi anavichukua anaenda hardware kuuza kwa bei ya hasara au anakaa navyo ili boss mwingine atayekuja amuuzie (atakuambia kuna duka mahali wanauza bei rahisi, ukimpa hela akanunue anaenda kufata vifaa vyake alipoviweka hela anaweka mfukoni)
Tupo pamoja ndg yanguDuu noma sana.
Ahsante kwa kuendelea kutuelimisha
Endapo ukipewa picha ya nyumba ambayo mtu ameipenda halafu wewe uichore ramani yake, si inawezekana? au ramani nzuri ni ile unayoichora wewe kutokana na specifications za mteja?Box za switch na socket utakazonunua hakikisha ni za material ya chuma (metal), ili waya wa ground/earth upate sehemu ya kuungia. Ikitokea mfumo wako wa umeme una leakage au waya unaobeba moto umegusa hizo box, umeme unapelekwa moja kwa moja ardhini kupitia waya wa earth na kuepuka risk ya mtu kupigwa shoti
Offer ya kutembelea site na kupeana ushauri kuhusu ujenzi kwa gharama nafuu kabisa bado inaendelea kwa mwezi huu wote.