Ndg yangu mmoja alipewa quotation ya vifaa vya umeme na fundi wake, basi akaona anishirikishe na mimi kuhusu hiyo quotation aliyopewa. Nikaiangalia ile quotation, nikamuambia huyu jamaa yangu anitumie na ramani yake. Nikapiga mahesabu nikaona kwamba fundi amezidisha vifaa ktk item zote karibu mara mbili ya uhalisia.
Nikamtumia quotation yangu niliyompigia hesabu, nikamuambia mwambie fundi aanze na hivyo vifaa kwanza vikipelea utamuongezea vingine maana alikuwa ameshampa advance kabla hajaanza kazi (mimi sikutaka nitubue mipango yao). Fundi akaangalia vile vifaa alivyoletewa, akawa amestuka kwa hivyo akahisi labda kuna fundi mwingine aliitwa pale site apige tena mahesabu ya vifaa. Baada ya fundi kuviangalia na kuhesabu akamuambia huyo boss kwamba hivi vinaweza vikatosha lakini, ngoja tuangalie. Kazi ikafanyika mpaka ikaisha,ikawa hakuna kilichopelea. Sasa swali ni kwamba vile vifaa vinavyozidishwa kwa makusudi na fundi huwa wanaviibaje?
Hapo kuna option mbili, ukimpa hela akanunue vifaa atakata hela huko huko na ukinunua mwenyewe vifaa alivyokupigia hesabu, hivi ilivyozidi anavichukua anaenda hardware kuuza kwa bei ya hasara au anakaa navyo ili boss mwingine atayekuja amuuzie (atakuambia kuna duka mahali wanauza bei rahisi, ukimpa hela akanunue anaenda kufata vifaa vyake alipoviweka hela anaweka mfukoni)