Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ndg yangu mmoja alipewa quotation ya vifaa vya umeme na fundi wake, basi akaona anishirikishe na mimi kuhusu hiyo quotation aliyopewa. Nikaiangalia ile quotation, nikamuambia huyu jamaa yangu anitumie na ramani yake. Nikapiga mahesabu nikaona kwamba fundi amezidisha vifaa ktk item zote karibu mara mbili ya uhalisia.

Nikamtumia quotation yangu niliyompigia hesabu, nikamuambia mwambie fundi aanze na hivyo vifaa kwanza vikipelea utamuongezea vingine maana alikuwa ameshampa advance kabla hajaanza kazi (mimi sikutaka nitubue mipango yao). Fundi akaangalia vile vifaa alivyoletewa, akawa amestuka kwa hivyo akahisi labda kuna fundi mwingine aliitwa pale site apige tena mahesabu ya vifaa. Baada ya fundi kuviangalia na kuhesabu akamuambia huyo boss kwamba hivi vinaweza vikatosha lakini, ngoja tuangalie. Kazi ikafanyika mpaka ikaisha,ikawa hakuna kilichopelea. Sasa swali ni kwamba vile vifaa vinavyozidishwa kwa makusudi na fundi huwa wanaviibaje?

Hapo kuna option mbili, ukimpa hela akanunue vifaa atakata hela huko huko na ukinunua mwenyewe vifaa alivyokupigia hesabu, hivi ilivyozidi anavichukua anaenda hardware kuuza kwa bei ya hasara au anakaa navyo ili boss mwingine atayekuja amuuzie (atakuambia kuna duka mahali wanauza bei rahisi, ukimpa hela akanunue anaenda kufata vifaa vyake alipoviweka hela anaweka mfukoni)
 
Katika ujenzi ukiwa na management nzuri ya site (materials, time, human resource n.k) utaokoa gharama nyingi ambazo unaweza kuziepuka.

Mfano katika ujenzi wa makaro ya choo, kuna mbao ambazo huwa zinatumika kwa ajili ya slab ambazo hizi huwezi ukazitumia tena baada ya kumwaga zege.

Sasa ukisema ununue hizi mbao mpya kutoka hardware katika hiyo stage ya kumwaga zege la makaro wakati kuna hatua za nyuma (mfano kufunga box la mkanda wa juu) zilikuwa zinahitaji mbao, wewe ukaenda kukodi mbao zote na kufanya hizi mbao ulizoweka kwenye karo zitumike mara moja tu tena zikiwa mpya kabisa. Huu ni mfano mdogo lakini kuna mifano mingi ambayo wakati mwingine unajikuta unaingia hasara hata ya 500,000/= na zaidi kwa kutojua namna ya kuendesha site.

Site Management ni moja ya factor inayoweza kufanya gharama za ujenzi ziwe juu au chini
 
Katika ufungaji wa nyaya za umeme (wiring), ni vyema ukatenganisha kila sakiti ikawa inajitegemea. Sakiti ya taa (lightings) iwe kivyake (hii tunatumia nyaya za 1.5mm²) na sakiti ya sockets (power) pia iwe kivyake (hii tunatumia nyaya za 2.5mm²)
 
Katika mfumo wa plumbing, traps (p-trap, gely trap n.k) huwa zinatumika kwa kazi ya kuzuia harufu na gesi zisiweze kurudi ndani ambapo maji huwa yanatuama kwenye tumbo la trap na kufanya hizo hewa (harufu/gesi) zisipate nafasi ya kupita kurudi ndani
 
Ni bora ukatumia twin socket moja kuliko kutumia single socket mbili katika chumba. Hii itasaidia kupunguza gharama ya vifaa na ufundi pia kwa sababu jumla ya bei ya single socket mbili ni kubwa kuliko bei ya twin socket moja.

Upande wa switch pia ni bora ukatumia 2 gang au 3 gang one way switch kuoperate taa mbali mbali (mfano taa ya sebleni, taa za nje na koridoni zote zikawa ktk switch moja ya 3 gang switch) kuliko kutumia 1 gang switch zaidi ya moja, itakufanya uongeze idadi ya metal box pia achilia mbali idadi ya hizo switch
 
Mafundi wengi wanatumia pipe level kwenye kozi ya mwisho (mfano kama msingi una kozi 7, basi ile kozi ya 7 ndio wanaitafutia level). Sasa kuna muda inatokea upande mmoja unadai udongo mwingi (mortar thickness) ili kufikia level ya upande mwingine hivyo inashauriwa utumie pipe level angalau katika kozi mbili kabla ya kuifikia ile kozi ya mwisho ili in case kama kuna upande utadai udongo mwingi uweze kubalance katika hizo kozi kuliko kurundika udongo sehemu moja katika kozi ya mwisho

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane

Mkuu samahani, nini maana ya pipe lever?
 
Mkuu samahani, nini maana ya pipe lever?
Pipe level ni kibomba chembamba (kina urefu wa kama mita 15) ambacho kinatumika kutafutia level ya sehemu (point) mbili tofauti. Kwenye hicho kibomba huwa tunaweka maji (unachanganya na rangi ya chakula kidogo kwenye maji ili iwe rahisi kuona maji yanavyoshuka na kupanda kwenye hicho kibomba).

Upande mmoja wa hicho kibomba unaushikilia, huku upande mwingine unakuwa unaupandisha/kuushusha kufuata level ya upande ambao umeshikiliwa, maji yakitulia maana yake hizo pande mbili za bomba maji yanapoishia zipo ktk level moja kwa hiyo unaweka alama zako then unaendelea kutafuta level upande mwingine kwa kutumia hizo point ambazo tayari zipo level
20240313_101914.jpg
 
Pipe level ni kibomba chembamba (kina urefu wa kama mita 15) ambacho kinatumika kutafutia level ya sehemu (point) mbili tofauti. Kwenye hicho kibomba huwa tunaweka maji (unachanganya na rangi ya chakula kidogo kwenye maji ili iwe rahisi kuona maji yanavyoshuka na kupanda kwenye hicho kibomba).

Upande mmoja wa hicho kibomba unaushikilia, huku upande mwingine unakuwa unaupandisha/kuushusha kufuata level ya upande ambao umeshikiliwa, maji yakitulia maana yake hizo pande mbili za bomba maji yanapoishia zipo ktk level moja kwa hiyo unaweka alama zako then unaendelea kutafuta level upande mwingine kwa kutumia hizo point ambazo tayari zipo level View attachment 2933217

Ahsante sana mkuu nimekuelewa vizuri.
 
Milango ya vyumba inatakiwa ikae pembeni kabisa (usiweke kati), upande mdogo uwe na angalau futi moja (hapa ipatikane tu nafasi ya kuweka switch ya kuwashia taa na feni pale mtu anapoingia ndani), na upande mkubwa inatakiwa usiwe chini ya futi 8 ili kuruhusu kitanda kukaa ktk uelekeo wowote bila kuathiri ufungukaji wa mlango.

Mlango inatakiwa ukiufungua ufungukie upande wa kuta ambao ni mkubwa ili kufanya vyumba kuwa na privacy (hapa namaanisha kama mtu amefungua mlango hata kwa nyuzi 20 kwa lengo la kuchungulia, basi akutane na ukuta wa pembeni na sio aone ndani chumba kizima kilivyo)

Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi wa msingi, sehemu ya kibaraza inatakiwa iwe chini kwa kozi moja. Mfano kama msingi wako unajenga kozi 7, basi sehemu ya kibaraza inabidi iwe na kozi 6 ili mtu anapotaka kuingia ndani kuwe na step ya kupanda. Hii itasaidia hata mvua inaponyesha maji ya kibarazani yasiweze kuingia ndani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Huduma ya kutembelea site na kushauriana mawili matatu ipo kwa wakazi wa Dsm na Pwani
 
Kama unaenda kununua nondo kwa tani na hujui hiyo tani moja inatakiwa iwe na nondo ngapi basi tumia hii formula ili usije ukaibiwa

N = 1000/((D²/162)×12)

Ambapo "D" ni diameter ya nondo ktk milimita, na "N" ni idadi ya nondo katika tani moja

Mfano
Kwa nondo za milimita 12, idadi ya nondo katika tani moja itakuwa
N=1000/((12²/162)×12))
N= 93.75 (Approximately 94pcs)

Nondo pia ni kama misumari, kg 1 ya misumari ni tsh 4000 haijalishi unachukua misumari ya size gani (ukichukua misumari midogo utapata misumari mingi, ukichukua misumari mikubwa utapata misumari michache)

Hizi dondoo zingine ilibidi nisiwape kabisa ili mtutafute hewani tuwapige hela za vocha[emoji846]

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane +255(0)624068809
 
Ndg yangu mmoja alipewa quotation ya vifaa vya umeme na fundi wake, basi akaona anishirikishe na mimi kuhusu hiyo quotation aliyopewa. Nikaiangalia ile quotation, nikamuambia huyu jamaa yangu anitumie na ramani yake. Nikapiga mahesabu nikaona kwamba fundi amezidisha vifaa ktk item zote karibu mara mbili ya uhalisia.

Nikamtumia quotation yangu niliyompigia hesabu, nikamuambia mwambie fundi aanze na hivyo vifaa kwanza vikipelea utamuongezea vingine maana alikuwa ameshampa advance kabla hajaanza kazi (mimi sikutaka nitubue mipango yao). Fundi akaangalia vile vifaa alivyoletewa, akawa amestuka kwa hivyo akahisi labda kuna fundi mwingine aliitwa pale site apige tena mahesabu ya vifaa. Baada ya fundi kuviangalia na kuhesabu akamuambia huyo boss kwamba hivi vinaweza vikatosha lakini, ngoja tuangalie. Kazi ikafanyika mpaka ikaisha,ikawa hakuna kilichopelea. Sasa swali ni kwamba vile vifaa vinavyozidishwa kwa makusudi na fundi huwa wanaviibaje?

Hapo kuna option mbili, ukimpa hela akanunue vifaa atakata hela huko huko na ukinunua mwenyewe vifaa alivyokupigia hesabu, hivi ilivyozidi anavichukua anaenda hardware kuuza kwa bei ya hasara au anakaa navyo ili boss mwingine atayekuja amuuzie (atakuambia kuna duka mahali wanauza bei rahisi, ukimpa hela akanunue anaenda kufata vifaa vyake alipoviweka hela anaweka mfukoni)
Duu noma sana.

Ahsante kwa kuendelea kutuelimisha
 
Box za switch na socket utakazonunua hakikisha ni za material ya chuma (metal), ili waya wa ground/earth upate sehemu ya kuungia. Ikitokea mfumo wako wa umeme una leakage au waya unaobeba moto umegusa hizo box, umeme unapelekwa moja kwa moja ardhini kupitia waya wa earth na kuepuka risk ya mtu kupigwa shoti

Offer ya kutembelea site na kupeana ushauri kuhusu ujenzi kwa gharama nafuu kabisa bado inaendelea kwa mwezi huu wote.
 
Endapo ukipewa picha ya nyumba ambayo mtu ameipenda halafu wewe uichore ramani yake, si inawezekana? au ramani nzuri ni ile unayoichora wewe kutokana na specifications za mteja?
 
Back
Top Bottom