Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Katika ubandikaji wa tiles, hakikisha mchanga wako umeuchekecha vizuri kwa kutumia wavu (coffee wire) ili kuondoa vichangalawe vidogo vidogo. Mchanga wenye changalawe unatia sana hasara, unapoweka tiles katika udongo (mortar) wenye changalawe then ukaigonga lazima itapasuka, mpaka uje umalize kazi utakuwa na wastage nyingi ambazo ungeweza kuzikwepa.
 
Katika nyumba za mtindo wa paa la kuficha (contemporary) ni vizuri kuweka slab hata ya urefu wa futi moja kuzunguka nyumba yote ili kuzuia maji yanayotiririka ukutani (kutokea juu kuja chini) yasiweze kuingia madirishani

Kwa mahitaji ya Ramani au makadirio tuwasiliane tafadhali
20230825_144423.jpg
 
Katika nyumba za mtindo wa kuficha paa (contemporary) ni vizuri ukatumia bati za kupima kiwandani (kama urefu wa bati unaohitajika unazidi futi 10) kuliko kutumia bati za futi 10 kwa kuziunga.

Pia ni vizuri ukatumia bati za migongo midogo kuliko bati za migongo mipana ili kupunguza risk ya bati kuvuja kutokana na maji kutembea juu ya migongo ya bati kwa speed ndogo hivyo kufanya maji yaingie kupitia matundu yaliyotobolewa na misumari ya bati
 
Mkuu umetisha sana.

Ahsante sana kwa nondo iliyoenda shule.

Mimi naomba unisaidie picha ya baadhi ya kazi zako iwe ni nyumba ya chumba 3 na nyingine 4 zenye sebule, jiko, vyoo 2,dining na uzio ili nijiridhishe muonekano na ubora wake kabla sijafanya maamuzi.

Ahsante sana.
 
Mkuu umetisha sana.

Ahsante sana kwa nondo iliyoenda shule.

Mimi naomba unisaidie picha ya baadhi ya kazi zako iwe ni nyumba ya chumba 3 na nyingine 4 zenye sebule, jiko, vyoo 2,dining na uzio ili nijiridhishe muonekano na ubora wake kabla sijafanya maamuzi.

Ahsante sana.
Habari mkuu
Nilikutext pm muda mrefu nikaona kimya, hii ni ya vyumba vinne ina hizo features zote ulizoainisha hapo juu. Karibu sana
20230904_140449.jpg
 
Katika uchanganyaji wa zege, ukitumia kokoto ambazo umbo lake ni la duara utatumia cement mifuko michache ukilinganisha na kokoto zingine (kwa ujazo wa zege na uwiano (ratio) unaofanana), hii ni kwa sababu nafasi iliyopo kati ya kokoto na kokoto (void space) katika hizi kokoto za duara ni ndogo kulinganisha na kokoto zingine
 
Wakati mwingine design inaweza kuchangia ongezeko la gharama za ujenzi mfano unaweza ukakuta chumba kina urefu wa mita 3.7 kwa upana wa mita 4.3 ambapo ukija kwenye kazi kama za tiles, gympsum n.k unabaki na wastage (vipande visivyotumika) nyingi wakati kama chumba hicho hicho kingekuwa na urefu wa mita 3.6 kwa upana wa mita 4.2 au 3.9 ungepunguza hii wastage na kuokoa gharama

Nikitolea mfano wa tiles, tiles zipo za 30cmx30cm, 40cmx40cm,50cmx50cm n.k

Mita 3.6 inagawanyika kwa 30cm au 40cm bila kubaki lakini mita 3.7 inagawanyika kwa 30cm na kubaki 10cm hivyo itakulazimu ukate vipande ili uweze kujazia hizo sehemu zilizobakia. Ni vyema ktk designing ukazingatia vitu kama hivi ili mwisho wa siku usiingie gharama zisizo na ulazima
vipande kutoka Room A si vitaenda kutumika Room B?
 
Moja ya aspects za building design ni pamoja na usalama, hakutakiwi nje kuwe na access yoyote ya kuingia ndani bila kuingilia mlangoni. Wezi mara nyingi wanaposhindwa kuingilia mlangoni, huwa wanatoboa dari la kwenye kibaraza na kutambaa juu kwa juu (kwenye dari) na kuingia ndani hivyo inashauriwa kuta za juu zinazozunguka kibaraza ziende mpaka juu kabisa kugusana na bati ili ikitokea mwizi ametoboa dari nje ashindwe kuingia ndani mpaka avunje ukuta

Ni ngumu kumzuia mwizi lakini inabidi utengeneze mazingira yatakayomfanya mwizi atumie muda mwingi zaidi kuweza kufanya tukio, hii itamfanya asitishe zoezi lake la kuiba kwa kuhofia kukamatwa

Kwa mahitaji ya ramani za kitaalam zinazozingatia aspects zote za usanifu majengo tuwasiliane
 
Back
Top Bottom