Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
Achana nae, Mwenye kipato hanaga zarau za kishamba hizi....hii kenge Moja tu inasubili ugari kwa Shemeji yake.
 
Mtaalamu hayo matundu yanasaidia nini?

Yasipowekwa itatokea shida gani ktk msingi au nyumba
Inasaidia ardhi kupumua kutokana na joto kali lililopo chini, usipoweka hayo matundu ardhi itashindwa kupumua na kufanya ukuta usukumwe na udongo ambapo itasababisha nyufa katika kuta za msingi.
 
Jamiiforums ni msaada mkubwa sana kwenye ulimwengu wa leo unaohitaji akili na matumizi sahihi ya pesa,post za mdau Hechy Essy zimenifungua akili kama hivi alivyoandika ningevijua mapema vingenisaidia sana.

Kwenye ujenzi tusiogope kutumia washauri kisa kukimbia gharama mimi sikuwa na akili hii majibu yake nimeshayaona,kwa mnaoanza ujenzi tafadhalini watumieni watu kama hawa watawasaidia sana.
Nashukuru ndugu kwa appreciation, ujenzi sio mgumu kama utaamua kujenga kwa awamu tofauti na kusubiri mpaka pesa yote itimie.

Unaweza ukaweka malengo ya miezi miwili miwili, mitatu mitatu n.k mfano mwezi januari mpaka machi ukajiwekea malengo ya kujenga msingi, mwezi april mpaka june ukainua boma, mwezi july mpaka septemba ukapaua n.k. ndani ya miaka miwili au mitatu unakuwa tayari umeshamaliza na kuhamia.

Katika hizo intervals za muda unakuwa na kazi ya kukusanya pesa kwa ajili ya hatua/malengo yanayofuata
 
Shukrani sana kwa ufafanuzi mkuu.

Kama hutojali pm namba yako ya simu kuna jamaa nimpe mnaweza mkafanya kitu kama utakuwa na bei rafiki na huduma nzuri.
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)

Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Kama hutojali, unijibu maswali yafuatayo:
1. Unapatikana wapi?

2. Unaweza kwenda mikoani? Kama jibu ni ndiyo, gharama yake ni sh ngapi nje na malipo ya kazi? Site ipo Arusha.

3. Ikiwa mtu anataka kuiboresha nyumba iliyokamilika kwa kubadili muundo wake, unaweza kuifanya hiyo kazi kwa kusaidia katika ushauri na pia kuichora ramani yake upya? Itakuchukua siku ngapi kukamilisha mchoro wake?

Asante.
 
Samahani ndg kwa kuchelewa kujibu, shida ipo kwenye app ya JF upande wa notification hivyo inanifanya niwe nakuja kuchungulia comment kila muda

1. Napatikana Dsm, Kimara

2. Kwa sasa ni ngumu kidogo kutoka nje ya mkoa, ila nina mafundi wangu wengi ambao ninawaamini, naweza nikakuconnect nao ukawasiliana nao

3. Ndio inawezekana, ramani huwa inachukua siku 3 mpaka 4 kutegemeana na ukubwa wa nyumba yenyewe. Bila shaka utakuwa unataka ubadili nyumba ya mfumo wa upauaji wa kawaida kwenda ktk mfumo wa paa la kuficha au vice versa
 
Ni ngumu sana kuviunganisha pamoja vitu viwili vyenye tabia tofauti mfano katika ule mfereji wa maji katika nyumba za paa la kuficha mafundi wengi wanamwaga zege kwenye ile slab ya mtaro, halafu kuta za mfereji wanazijenga kwa tofali.

Ikumbukwe kuwa kila material ina thermal expansitivity value yake, hivyo joto linapoongezeka au kupungua kila material itatanuka/kusinyaa kwa kiasi chake kutokana mabadiliko ya hilo joto. Kiasi cha utanukaji/kusinyaa itategemea na hiyo value yake ya thermal coefficient

Utofauti wa hizi values ndio unaofanya materials zilizounganishwa pamoja kuachana na kuleta nyufa ktk maungio kwa sababu kila kimoja kitatanuka/kusinyaa kwa namna yake

Ni vizuri ukatumia material ya aina moja au materials ambazo values zake angalau zinakaribiana sana ili kufanya huo muunganiko wa vitu viwili kutanuka na kusinyaa kwa pamoja pale kunapotokea mabadiliko ya joto.

Kwenye ule mfereji, ni vizuri ukatumia zege pote (yaani ile slab na kuta zake za pembeni) lakini kama ukishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ya kiuchumi basi unashauriwa baada ya kumwaga ile slab ya mfereji, pandisha ukuta mfupi wa zege hata wa sentimita 15 mpaka 20 halafu juu ndipo ulaze tofali , lengo ni kuepuka nyufa zinazojitokeza kwenye zile kona za mfereji (pale kwenye maungio ya slab na kuta za mfereji) kutokana na utofauti wa hizo thermal coefficient values.

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali
 
Kitaalam haishauriwi maji ya jikoni (kuoshea vyombo n.k) kwenda ktk shimo la choo kwa sababu maji ya jikoni yana mafuta ambayo hutengeneza tabaka juu ya maji na kuzuia hewa isiingie chini. Umeng'enyaji wa uchafu uliopo ktk shimo la choo hufanywa na bacteria ambao hao bacteria wanahitaji hewa ili waendelee kuishi.

Utakapomwaga maji ya jikoni kwenye karo la choo, lile tabaka la mafuta litafanya bacteria wakose hewa na kupelekea kufa hivyo karo litakuwa linajaa haraka (mara kwa mara) kutokana na kwamba umeng'enyaji wa uchafu haufanyiki au unafanyika kwa kiasi kidogo kutokana na uchache wa hewa na bacteria uliopo chini.

Vinginevyo itabidi ujenzi wa septic tank (lile shimo la pembe nne) uweke buffer wall kati kati (Mechanism ya Buffer wall nitaielezea siku nyingine, subscribe huu uzi uendelee kupata dondoo mbali mbali kuhusu ujenzi)

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali +255(0)624068809
 
Safi sana kiongozi , nikiwa Moshi ufundi nilisoma Plumbing , nilifundishwa kuwa hata system ya choo na bafu havitakiwi kuwa na same path(destination) sababu , ya hao bacteria (anaerobes bacteria) ambao ndio huvunja vunja uchafu.
 
Kabisa kabisa, hiyo ni kwa sababu ya zile kemikali za sabuni, body wash n.k....maji ya bafuni inatakiwa yaelekezwe moja kwa moja ktk shimo la duara (soak way pit) bila kupitia ktk shimo la mstatili (septic tank)
 
Kitaalam haishauriwi maji ya jikoni (kuoshea vyombo n.k) kwenda ktk shimo la choo kwa sababu maji ya jikoni yana mafuta ambayo hutengeneza tabaka juu ya maji na kuzuia hewa isiingie chini. Umeng'enyaji wa uchafu uliopo ktk shimo la choo hufanywa na bacteria ambao hao bacteria wanahitaji hewa ili waendelee kuishi.

Utakapomwaga maji ya jikoni kwenye karo la choo, lile tabaka la mafuta litafanya bacteria wakose hewa na kupelekea kufa hivyo karo litakuwa linajaa haraka (mara kwa mara) kutokana na kwamba umeng'enyaji wa uchafu haufanyiki au unafanyika kwa kiasi kidogo kutokana na uchache wa hewa na bacteria uliopo chini.

Vinginevyo itabidi ujenzi wa septic tank (lile shimo la pembe nne) uweke buffer wall kati kati (Mechanism ya Buffer wall nitaielezea siku nyingine, subscribe huu uzi uendelee kupata dondoo mbali mbali kuhusu ujenzi)

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali +255(0)624068809
Aiseee vzr sana, leo umenipa elim7 nyingine.... Mimi ni mechanical engineer, huwa nafanya plumbing(sewage and clean water) , lakin majengo mengi ambayo nimefanya design, nilikuwa naweka maji ya jikon direct kwenye septic, although nilikuwa najenga septic and soak away kwa pamojaa...
 
Safi sana kiongozi , nikiwa Moshi ufundi nilisoma Plumbing , nilifundishwa kuwa hata system ya choo na bafu havitakiwi kuwa na same path(destination) sababu , ya hao bacteria (anaerobes bacteria) ambao ndio huvunja vunja uchafu.
Sabbu hapo wanaogopa back pressure inaweza kurudi kwenye pipe za maji ya kuogea na kuanza kutoa harafu
 
Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
Umemjibu vema.
Asante sana kwa elimu unayoitoa na kwa uungwana wako.
 
Katika ubandikaji wa tiles sakafuni, kitaalam inatakiwa kwanza uweke timanzi (hii ni kama gauge ya kufanya sakafu yako iwe na usawa mmoja chumba kizima), kisha mwaga udongo (mortar) pote chumba kizima, shindilia vizuri kwa kufata timanzi zako kisha ndipo uanze kuweka tiles zako kwa kutumia udongo mwepesi na mwembamba (hii itakuwa ni kama gundi ya kati ya sakafu na tiles)

Ukitumia mfumo huu, tiles zako zitakuwa imara na hutosikia tiles zako zikilia kama ngoma unapotembea juu yake kwa sababu tiles zimelala katika udongo ambao umeshindiliwa vizuri. Lakini pia kwa mfumo huu, kazi ya ubandikaji inakuwa rahisi zaidi kwa sababu unazilaza tiles zako katika sehemu ambayo umeshaifanyia levelling tayari.

Mafundi wengi wanamwaga udongo kwa tiles moja moja, na kuigonga tiles ikiwa juu ya huo udongo kutafuta level kitu ambacho kinafanya udongo usambae pembeni na wakati mwingine kuacha uwazi ambao baada ya muda itafanya tiles zianze kulia kama ngoma. Na kingine mfumo huu wa kumwaga udongo kwa tiles moja moja unatumia muda mwingi, na uimara wake ni wa mashaka

Ikiwa unahitaji Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Moja kati ya vitu vya kuzingatia kabla hujanunua kiwanja ni pamoja na aina ya udongo uliopo k atika hicho kiwanja
Udongo mzuri ni ule wenye asili ya kichanga ambao wenyewe hauna kawaida ya kutanuka na kusinyaa pindi kunapotokea mabadiliko ya kiwango cha maji badala yake huruhusu maji kuzama chini kirahisi kutokana na nafasi kubwa iliyopo kati ya punje moja na nyingine

Udongo wa mfinyazi sio mzuri katika ujenzi, una kawaida ya kutanuka na kusinyaa hivyo husababisha nyufa katika kuta
 
Baada ya kuskim ukuta, ni vizuri ukaapply binder (primer) kabla ya kupaka rangi. Binder inaua lile vumbi la skimming na kufanya rangi inayokuja kupakwa baada ya primer ishike vizuri na kudumu muda mrefu.
Binder pia inapunguza matumizi ya rangi kwa sababu inazuia ukuta kufyonza rangi

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)

Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Tukitoka ya hii ya vyumba viwili tuone na ya vyumba vitatu
 
Ni ngumu sana kuviunganisha pamoja vitu viwili vyenye tabia tofauti mfano katika ule mfereji wa maji katika nyumba za paa la kuficha mafundi wengi wanamwaga zege kwenye ile slab ya mtaro, halafu kuta za mfereji wanazijenga kwa tofali.

Ikumbukwe kuwa kila material ina thermal expansitivity value yake, hivyo joto linapoongezeka au kupungua kila material itatanuka/kusinyaa kwa kiasi chake kutokana mabadiliko ya hilo joto. Kiasi cha utanukaji/kusinyaa itategemea na hiyo value yake ya thermal coefficient

Utofauti wa hizi values ndio unaofanya materials zilizounganishwa pamoja kuachana na kuleta nyufa ktk maungio kwa sababu kila kimoja kitatanuka/kusinyaa kwa namna yake

Ni vizuri ukatumia material ya aina moja au materials ambazo values zake angalau zinakaribiana sana ili kufanya huo muunganiko wa vitu viwili kutanuka na kusinyaa kwa pamoja pale kunapotokea mabadiliko ya joto.

Kwenye ule mfereji, ni vizuri ukatumia zege pote (yaani ile slab na kuta zake za pembeni) lakini kama ukishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ya kiuchumi basi unashauriwa baada ya kumwaga ile slab ya mfereji, pandisha ukuta mfupi wa zege hata wa sentimita 15 mpaka 20 halafu juu ndipo ulaze tofali , lengo ni kuepuka nyufa zinazojitokeza kwenye zile kona za mfereji (pale kwenye maungio ya slab na kuta za mfereji) kutokana na utofauti wa hizo thermal coefficient values.

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali
I appreciate what you are giving. It is beneficial and eye opener. Mimi nina opinion na pia nina swali if you won't mind. Opinion yangu ni kuhusu utoaji wako wa elimu. Elimu ni nzuri sana, kama itawezekana uongezee hata na simple sketch (illustrations) kutoa mwanga zaidi kwa point husika.

Swali langu ni kuhusu hii style mpya ya kuweka paa. Nimesikia mara nyingi sana kuna tatizo la maji kuvuja. Nawaza ni namna gani in a nutshell kuavoid hii changamoto?

Asante
 
Huu mfumo unahitaji umakini sana, mimi binafsi napembelea mfumo wa contemporary ambao mfereji wake unazungukia nje kama ilivyo pvc gutter. Upauaji unakuwa wa kawaida (angle ndogo) ila bati linakuwa halionekani na mzunguko wa bati wote unadondoshea maji kwenye huo mfereji (hakuna kuchimbia bati kwenye ukuta)

Ningewatumia picha ila sasa shida picha sio ya kwangu na mmiliki wa picha akiona nimetumia picha yake itakuwa shida
 
Back
Top Bottom