Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Katika ubandikaji wa tiles sakafuni, kitaalam inatakiwa kwanza uweke timanzi (hii ni kama gauge ya kufanya sakafu yako iwe na usawa mmoja chumba kizima), kisha mwaga udongo (mortar) pote chumba kizima, shindilia vizuri kwa kufata timanzi zako kisha ndipo uanze kuweka tiles zako kwa kutumia udongo mwepesi na mwembamba (hii itakuwa ni kama gundi ya kati ya sakafu na tiles)

Ukitumia mfumo huu, tiles zako zitakuwa imara na hutosikia tiles zako zikilia kama ngoma unapotembea juu yake kwa sababu tiles zimelala katika udongo ambao umeshindiliwa vizuri. Lakini pia kwa mfumo huu, kazi ya ubandikaji inakuwa rahisi zaidi kwa sababu unazilaza tiles zako katika sehemu ambayo umeshaifanyia levelling tayari.


Mafundi wengi wanamwaga udongo kwa tiles moja moja, na kuigonga tiles ikiwa juu ya huo udongo kutafuta level kitu ambacho kinafanya udongo usambae pembeni na wakati mwingine kuacha uwazi ambao baada ya muda itafanya tiles zianze kulia kama ngoma. Na kingine mfumo huu wa kumwaga udongo kwa tiles moja moja unatumia muda mwingi, na uimara wake ni wa mashaka

Ikiwa unahitaji Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
unamaanisha udongo mkavu wakujengea?
 
Moja kati ya vitu vya kuzingatia kabla hujanunua kiwanja ni pamoja na aina ya udongo uliopo k atika hicho kiwanja
Udongo mzuri ni ule wenye asili ya kichanga ambao wenyewe hauna kawaida ya kutanuka na kusinyaa pindi kunapotokea mabadiliko ya kiwango cha maji badala yake huruhusu maji kuzama chini kirahisi kutokana na nafasi kubwa iliyopo kati ya punje moja na nyingine

Udongo wa mfinyazi sio mzuri katika ujenzi, una kawaida ya kutanuka na kusinyaa hivyo husababisha nyufa katika kuta
Hiii inatukumba arusha na sijui solution nzur ni ipi mm kama mjenzi mtarajiwa.. udongo wa huku unatanuka na kusinyaa ukitanuka unapasuka hapo solution n nn
 
unamaanisha udongo mkavu wakujengea?
Baada ya hapo, ni kibandika tiles kwa udongo mwepesi. Huo udongo mkavu tayari umeshashindiliwa na kuwekwa level.
20231013_101707.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
Oya mwamba achana nae watu km hao wapi wengi sn ambao kazi Yao ni kukatisha watu tamaa Sasa ukianza kuangaika nao utakikuta muda mwingi unamaliza Kwa ajili Yao badala ya kufikiria ya msingi na kufanya kazi zako. Kwa upande wng nakuunga mkono ndg endelea kutuelimisha, tupo wengi ambao hatujui mengi au lolote kuhusu ujenzi
 
Ni muhimu sana kuweka vent pipe katika mfumo wa maji taka ili kuzuia harufu kurudi ndani ya nyumba ( kwa wale wanaotumia vyoo vya ndani)

Unaweza ukaweka T connector kwenye kile kipande cha bomba kinachounganisha P-trap na chemba halafu ukaweka bomba refu kuelekea juu (usisahau kuweka na mfuniko wake ambao unakuwa na matundu pembeni ili mvua inaponyesha maji yasiwe yanaingia kupitia hilo bomba) nkipata picha nitawaletea ili iwe rahisi kueleweka

Pia unaweza ukaweka vent pipe na kwenye karo la choo ili kupunguza joto na pressure ya hewa iliyopo ndani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oya mwamba achana nae watu km hao wapi wengi sn ambao kazi Yao ni kukatisha watu tamaa Sasa ukianza kuangaika nao utakikuta muda mwingi unamaliza Kwa ajili Yao badala ya kufikiria ya msingi na kufanya kazi zako. Kwa upande wng nakuunga mkono ndg endelea kutuelimisha, tupo wengi ambao hatujui mengi au lolote kuhusu ujenzi
Tupo pamoja mkuu, uwepo wao ndio unatupatia changamoto ya kupambana zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni muhimu sana kuweka vent pipe katika mfumo wa maji taka ili kuzuia harufu kurudi ndani ya nyumba ( kwa wale wanaotumia vyoo vya ndani)

Unaweza ukaweka T connector kwenye kile kipande cha bomba kinachounganisha P-trap na chemba halafu ukaweka bomba refu kuelekea juu (usisahau kuweka na mfuniko wake ambao unakuwa na matundu pembeni ili mvua inaponyesha maji yasiwe yanaingia kupitia hilo bomba) nkipata picha nitawaletea ili iwe rahisi kueleweka

Pia unaweza ukaweka vent pipe na kwenye karo la choo ili kupunguza joto na pressure ya hewa iliyopo ndani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane

Sent using Jamii Forums mobile app
Vent pipe
20231014_084353.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine mkanda wa zege sio lazima uwekwe nondo za juu na za chini, ni vile tu kwa sababu ringi hatizoweza kukaa kwa kufunga nondo za chini pekee ndio maana unakuta zinafungwa nondo chini na juu.

Wengine hutumia nondo za milimita 12 upande wa chini, na juu wanatumia nondo za milimita 10 hivyo inapunguza gharama (hii ni kama mkanda wako ni singly reinforced beam).

Katika mkanda, zege huwa inakabiliana na compressional forces upande wa juu, na nondo huwa inakabiliana na tension forces upande wa chini hivyo kama zege uliyotumia inaweza kukabiliana yenyewe na compressional force bila msaada wa nondo, basi hakuna haja ya kuweka nondo mbili juu na nondo mbili chini, ni bora ukaweka nondo tatu chini, nondo moja juu ukatumia ringi za pembe tatu ambapo mkanda wako utakuwa imara zaidi kuliko mtu aliyefunga nondo mbili juu, nondo mbili chini. (Hapa nazungumzia singly reinforced beam)

Upande wa Doubly reinforced beam, mkanda nondo zake zinafungwa chini na juu na hii hutumika pale zege yenyewe inashindwa kukabiliana na compressional forces hivyo inahitaji msaada wa nondo upande wa juu. Katika doubly reinforced beam, nondo za juu zinakuwa na kazi ya kubeba mzigo pia lakini kwa singly reinforced beam, nondo za juu zinakaa kwa ajili ya kushikilia ringi

Utajuaje kama mkanda wako ni singly au doubly reinforced beam? Hapo sasa ni mpaka mahesabu yafanyike (tuishie hapo kwa leo)

Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika uchanganyaji wa zege, ukitumia kokoto ambazo umbo lake ni la duara utatumia cement mifuko michache ukilinganisha na kokoto zingine (kwa ujazo wa zege na uwiano (ratio) unaofanana), hii ni kwa sababu nafasi iliyopo kati ya kokoto na kokoto (void space) katika hizi kokoto za duara ni ndogo kulinganisha na kokoto zingine
Kokoto za duara hazifai kutumika kwenye ujenzi; au nasema uongo ndugu zangu?
 
Baada ya kupanga mawe (hardcore) katika msingi, inashauriwa umwage mchanga mwingi ndipo uje umwage zege la jamvi (oversite concrete). Hii ni kwa sababu unapopanga mawe, ile nafasi iliyopo kati ya jiwe na jiwe zege inaweza isipite kwenda kuziba hizo nafasi. Kama hiyo sakafu itapata mgandamzo mkubwa (mfano gari ikapita) inaweza kusababisha hiyo sakafu kutitia kutokana na uwepo wa uwazi (matundu) uliopo chini yake

Kama unahitaji ramani za kitaalamu na makadirio ya vifaa vya ujenzi tuwasiliane
Hoja yako haina mashiko, labda ungeeleza msingi wa nini.
Nyumba gani gari itaingia au kukanyaga?

Ongelea godauni labda
 
Kitaalam haishauriwi maji ya jikoni (kuoshea vyombo n.k) kwenda ktk shimo la choo kwa sababu maji ya jikoni yana mafuta ambayo hutengeneza tabaka juu ya maji na kuzuia hewa isiingie chini. Umeng'enyaji wa uchafu uliopo ktk shimo la choo hufanywa na bacteria ambao hao bacteria wanahitaji hewa ili waendelee kuishi.

Utakapomwaga maji ya jikoni kwenye karo la choo, lile tabaka la mafuta litafanya bacteria wakose hewa na kupelekea kufa hivyo karo litakuwa linajaa haraka (mara kwa mara) kutokana na kwamba umeng'enyaji wa uchafu haufanyiki au unafanyika kwa kiasi kidogo kutokana na uchache wa hewa na bacteria uliopo chini.

Vinginevyo itabidi ujenzi wa septic tank (lile shimo la pembe nne) uweke buffer wall kati kati (Mechanism ya Buffer wall nitaielezea siku nyingine, subscribe huu uzi uendelee kupata dondoo mbali mbali kuhusu ujenzi)

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane tafadhali +255(0)624068809
Bacteria wanaochakata uchafu hawahitaji oxygen ili kuishi au bacteria wa kwako ni special?
 
Back
Top Bottom