Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kwenye nguzo za vibaraza sio lazima uweke nguzo za zege, unaweza ukaweka nguzo ya shape ya "L" kwa kutumia tofali na bado nyumba yako ikavutia lakini pia ikakupunguzia gharama za nondo na ufundi
 
Upande wa frem ya mlango ambao umeflash na ukuta, ni vizuri ukapigilia Architrave ili kuziba ule mwanya unaotengenezwa kati ya ukuta na frem kutokana na mabadiliko ya joto. Mbali na hivyo, pia inaleta muonekano mzuri
 
Ramani, Makadirio na Ushauri tuwasiliane
Kaka nashukuru Kwa somo Kuna mengi ninejifunza Ila Mimi Nina mjengo wangu nimekwama kwenye kupaua maana mahesabu ya mafundi wengi yanagonga kwenye milioni kumi mpaka kumi na mbili Sasa nimewaza labda nibadilishe aina ya paa nipaue hii ya kuficha bati labda gharama zitapungua na je Kwa uzoefu wako naweza kusave kiasi gani? Nyumba ni room tatu master mbili ya kawaida moja na pablic toilet na jiko stoo siting room na dining Ila pia ni nyumba yenye konakona nyingi
 
Binafsi sikushauri utumie huo mfumo wa kuficha paa kwa sababu kwanza inahitaji umakini mkubwa sana katika upauaji, unaweza ukajikuta unaingia kwenye hasara ya kubadilisha huo mfumo ndani ya miezi michache ijayo.

Hiyo milion 10 mpaka 12 mbona ni nyingi sana? Au unatumia bati za versatile / romantile?
 
Ndio natumia aina hiyo ya bati
 
Ndio natumia aina hiyo ya bati
Hizo bati mita moja ni kati ya 23,000 mpaka 25,000 so mfano kwa bati moja la mita 3 itakuwa ni sawa na 23,000×3 = 69,000/pc

Tuchukulie mfano nyumba yako itatumia bati pc 125,
Jumla itakuwa 125×69000 ambayo ni sawa na 8,625,000 (hapo bado mbao, misumari,valleys, hips na ufundi). Kwa hiyo utaona estimation yao iko sahihi (kama wameongeza cha juu, basi ni kidogo sana[emoji846])
 
Kiongozi swali langu je nyumba ya kuficha paa inafaa kupaua na Bati mgongo mpana AU Mgongo mdogo?
Asante
 
Nyumba za kuficha bati huwa tunatumia bati za migongo midogo ili kupunguza risk ya uvujaji wa maji kipindi cha mvua. Bati za migongo mipana, migongo yake ina sehemu ambayo iko flat hivyo kama maji yatakuwa yanatembea kwa kasi ndogo kutokana na slope kuwa ndogo, uwezekano wa maji kuingia kwenye matundu ya misumari ni mkubwa zaidi licha ya misumari kuwa na rubber
 
Asante kiongozi
 
Sehemu ambazo zinakuwa na maji maji mfano bafuni, sehemu ya kuoshea magari (car wash) n.k ni vizuri dari lake ukatumia baard za PVC badala ya gympsum boards kwa sababu gympsum board huwa zinaharibika zikikutana na maji au hata unyevu unyevu.
 
Back
Top Bottom