Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kama mfuko unaruhusu, kuta zote zinazozunguka nyumba kwa nje tumia tofali za nchi 6...hii itakupa nafasi ya kutosha kuweka madirisha ya grill na aluminium katika muonekano mzuri zaidi lakini pia kwenye milango ya nje ambayo inakuwa na mlango wa mbao na geti la grill. Ukuta wa nchi 6 ukipigwa plaster ndani na nje unene wake utakaribia/kufikia nchi 7
 
Wakati mwingine mtu anaweza akapendelea kutumia size mbali mbali za tiles katika nyumba, mfano sebleni akatumia tiles za 50x50, vyumbani akatumia tiles za 40x40, chooni akatumia tiles za 30x30 n.k. Kwa case hii, itabidi itengenezwe step mahali ambapo tiles (zenye size tofauti) zinakutania ili kuua zile pattern zisikutane maana mistari itapishana kutokana na utofauti wa size
 
Binafsi sikushauri utumie huo mfumo wa kuficha paa kwa sababu kwanza inahitaji umakini mkubwa sana katika upauaji, unaweza ukajikuta unaingia kwenye hasara ya kubadilisha huo mfumo ndani ya miezi michache ijayo.

Hiyo milion 10 mpaka 12 mbona ni nyingi sana? Au unatumia bati za versatile / romantile?
Kampuni gani ina bat zuri za hizo versatile/ romantil
 
Kabla hujaanza ujenzi, ni vizuri ukajua upande ambao jua huwa linachomoza (mashariki)...Mada ni ndefu, kwa leo nitaelezea upande ambao jiko (kitchen room) linatakiwa likae

Jiko linatakiwa likae upande wa Kusini Mashariki ambapo mida ya asubuhi jua linakuwa ni la wastani (jua la vitamin D, hapa mpishi atapata muda wa kuandaa breakfast akiwa comfortable kabisa), baada ya hapo jua litakuwa linaendelea kuhama taratibu ambapo mpaka kufikia mida ya saa tano tano kuelekea saa sita, jua litakuwa lipo juu ya nyumba linapiga bati kwa juu (hapa pia mpishi atakuwa katika mazingira rafiki kuandaa chakula cha mchana bila kusumbuliwa na joto la jua)

Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane
 
Baada ya madirisha ya grill (na vitu vingine vya chuma kama mlango wa geti n.k) kupakwa red oxide (ile rangi nyekundu), ni vizuri ukatumia (kupaka) rangi yenye viambata vya aluminium (Aluminium paint) ili kuzuia chuma kutopata kutu
 
Kama mfuko unaruhusu, kuta zote zinazozunguka nyumba kwa nje tumia tofali za nchi 6...hii itakupa nafasi ya kutosha kuweka madirisha ya grill na aluminium katika muonekano mzuri zaidi lakini pia kwenye milango ya nje ambayo inakuwa na mlango wa mbao na geti la grill. Ukuta wa nchi 6 ukipigwa plaster ndani na nje unene wake utakaribia/kufikia nchi 7
Swali je kuchanganya nchi 6 Kwa nje na ndani 5 muingiliano unakubali kwenye joint
 
Kabla hujaanza ujenzi, ni vizuri ukajua upande ambao jua huwa linachomoza (mashariki)...Mada ni ndefu, kwa leo nitaelezea upande ambao jiko (kitchen room) linatakiwa likae

Jiko linatakiwa likae upande wa Kusini Mashariki ambapo mida ya asubuhi jua linakuwa ni la wastani (jua la vitamin D, hapa mpishi atapata muda wa kuandaa breakfast akiwa comfortable kabisa), baada ya hapo jua litakuwa linaendelea kuhama taratibu ambapo mpaka kufikia mida ya saa tano tano kuelekea saa sita, jua litakuwa lipo juu ya nyumba linapiga bati kwa juu (hapa pia mpishi atakuwa katika mazingira rafiki kuandaa chakula cha mchana bila kusumbuliwa na joto la jua)

Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane
Leo tuangalie upande ambao SEBULE na VYOO vinapotakiwa vikae

Katika pande zote nne yaani Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi, upande wa Kaskazini ndio upande ambapo unapokea jua ama joto kwa kiasi kidogo na upande wa Kusini ndio upande ambao unapokea jua ama joto kwa kiasi kikubwa katika masaa yote ya siku (asubuhi mpaka jioni). Upande wa Mashariki hupokea joto jingi kuanzia asubuhi mpaka mida ya mchana, na upande wa Magharibi hupokea joto jingi kuanzia mchana mpaka jioni

Sebule inatakiwa ielekee Kaskazini kwa sababu ni sehemu ambayo muda mwingi watu watakuwa hapo (asubuhi mpaka jioni) hivyo haitakiwi iwe upande ambao utakuwa sio rafiki kukaa katika mazingira hayo

Tukija upande wa Kusini ambao unapokea joto jingi zaidi katika masaa yote ya siku, kitu ambacho unaweza kuweka upande huu (kusini) ni vyoo na mabafu. Hii ni kwa sababu chooni sio mahali ambapo watu hukaa muda mrefu, watu hukaa muda mfupi na pia ni kwa mara chache.

Ramani, Makadirio na Ushauri wa kitaalam tuwasiliane +255(0)624068809
 
Swali je kuchanganya nchi 6 Kwa nje na ndani 5 muingiliano unakubali kwenye joint
Ndio mkuu, tofali zote zinakuwa zinasimamishwa (utofauti utakuwepo kwenye unene wa tofali, ambao wenyewe hauna shida kwa sababu haziunganishwi parallel)
 
Kuna mahali nimepita nimekuta taa za nje angle holder zake zimeelekezwa juu (sijui ni fashion au wanaweka kwa malengo gani)
Angle holder kuelekezwa juu ni hatari kwa sababu mvua itakaponyesha,maji yataingia kwenye holder na hivyo inaweza kuleta shida kwenye mfumo wa umeme ikiwemo moto
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)

Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Nipe namba yako
 
Katika makubaliano ya gharama za kazi na fundi, jitahidi makubaliano yasiwe juu juu (ile kazi husika iwekee na vipengele vyake ili mwisho wa siku fundi asije akakuruka).

Mfano unaweza ukakubaliana na fundi kazi ya kukata miti katika eneo lako la ujenzi, sasa usishangae kuona mafundi wanakuja kukudai pesa yao baada ya kukata hiyo miti maana ukiwaambia mbona hamjaitoa watakuambia sisi tumekubaliana kazi ya kukata miti sio kuikata na kuitoa. Mpaka hapo itakulazimu uingie tena gharama zingine, maana itabidi mfanye tena makubaliano ya kazi ya kuhamisha miti

Sasa kwa mfano huu wa miti, itatakiwa uwaambie kwamba hiyo kazi itainclude kukata miti yote, kuihamisha eneo la ujenzi (na ikibidi waoneshe mahali ambapo unataka yakae hayo magogo, wasije wakayaweka tu pembeni baadae ukaingia tena gharama ya kutafuta watu wayasogeze pembeni zaidi), na malipo yote ni baada ya kazi kukamilika/kuisha. Ukijichanganya kuwalipa malipo kwa kazi waliyofanya, kesho wanaweza wasirudi hasa pale kazi inapokuwa ni ngumu, lakini kama hujawalipa kabisa au umewalipa kidogo hawawezi kukutoroka kesho wasije site.

Ramani, Makadirio na Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane +255(0)624068809
 
Unaijua Nilu? Nilu ni mchanganyiko wa saruji na maji ambapo ukichanganywa hutengeneza kitu kama uji uji (Cement paste)
Huwa inatumika kusakafia kuta za visima ili maji yasifyonzwe na hizo kuta na kupotelea ardhini, huwa inatumika kusakafia sakafu ili iwe rahisi kusafisha (mfano mafuta yanapomwagika sakafuni n.k), pia huwa inatumia kusakafia kuta za bafu/vyoo kwa wale ambao hawaweki tiles za ukutani, lengo likiwa ni lile kuzuia kuta zisifyonze maji na pia kuwa na urahisi wa kusafishika

Nilu hupakwa baada ya kuta kupigwa plaster, au sakafu kuwekwa ile rough floor, haipakwi moja kwa moja kwenye tofali
 
UFUNDI UMEME

(1) Hata kama unampa ela ya vifaa fundi basi ni vizuri kuakikisha alichokiandika ni sahihi maana mafundi uwa tuna tamaa baada ya ela kuwa mikononi.unakuta fundi kakuandikia waya(kampuni ya euro)ila unashangaa analeta site waya usiojulikana.hii ni hatari sana kwa usalama wako na vifaa vyako.

(2) Kabla ya kufanya wiring ni vizuri wewe muhusika kumwambia fundi maitaji yako yote ya vitu ambavyo utakuja kutumia baadae ili isije ikatokea changamoto ya kufanya upanuzi wa maitaji mengine ya umeme.mfano kwenye stage ya kwanza(kuchimbia bomba) ni vizuri kuweka point nyingi ili hata ikitokea unaitaji kuongeza kibu basi kusiwe na changamoto.

(3) hakikisha umeme wowote unaopita chini ya ardhi basi ununue waya maalum kwa ajili ya chini ya ardhi.sio kila waya una uwezo wa kupita chini ya ardhi.hii baadae itakuja kukuletea shida wakati huo utashindwa kufanya kitu kwa sababu gharama ya marekebisho itakuwa kubwa.

(4)Hakikisha unanunua vifaa vya umeme ambayo kwa ndani vimetengenezwa kwa copper na sio chuma kilicholambishwa copper.kampuni yenye vifaa vilivyotengenezwa kwa pure copper kwa hapa nchini ni( Tronic,ABB,Africab,havels)

(5)Hakikisha fundi anatumia bomba kwenye kufanya wiring na pia anafunga na mifuniko kwenye sehemu zenye juction box ili kuzuia wadudu kufika kwenye switch au main switch.

(6) Hakikisha fundi anaorodhesha matumizi yako yote kwenye kuomba mita tanesco ili usije ukapewa mita ndogo ukashangaa umeme unaenda mwingi kumbe mita inazidiwa.hakikisha taarifa za matumizi alizoweka kwenye mchoro ni sahihi.

Kwa ushauri pamoja na kazi piga namba
0652868486
 
Kwa ushauri na kazi nicheki 0652868486
Ubarikiwe mkuu kwa kutoa hints mbali mbali kuhusu umeme lakini sio busara kutangaza biashara yako kwenye uzi wa mtu mwingine ambaye nae pia yupo kibiashara. Chochote kitakachotokea baina yako na mteja, mimi pia naweza nikahusishwa, mtu anaweza akakupigia wewe akajua anaongea na mimi kwa sababu namba ameikuta kwenye uzi niliouanzisha mimi.

Kuanzisha uzi ni bure, hakuna malipo yoyote...kwanini na wewe usiwe na uzi wako ukajibrand wewe kama wewe?!!

Mtu kutangaza biashara yake ndani ya uzi wa mtu mwingine inafanya wateja wasikuamini kwa sababu ni rahisi kufuta comment kuliko kufuta uzi hasa pale kunapotokea tatizo baina ya mteja na mtoa huduma
 
Futa hii post mkuu
 
Back
Top Bottom