Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #441
haya maelezo yangekua na kamchoro ingekua safiUkipita baadhi ya nyumba utaona kuna baadhi ya madirisha/milango kunakuwa na nyufa kati ya mkanda wa juu na ile kozi ya tofali ya chini ya mkanda.
Hii huwa inatokea pale mzigo uliopo juu ya mkanda katika madirisha ama milango ni mkubwa kiasi cha kupelekea mkanda upinde kwenda chini, mkanda ukipinda unafanya zile sehemu za mkanda za pembeni karibu na kuta (support) kupanda juu na kufanya mkanda uachane na tofali. Ufa huo huendelea kadri mkanda unavyozidi kuelemewa na mzigo na wakati mwingine kufanya uungane na ufa wa dirisha jingine
Ili kuzuia hii hali, ni vizuri sehemu zote zenye uwazi chini ya mkanda (mfano madirisha, milango n.k) ukaongeza kipande kimoja cha nondo chini kati kati ya nondo mbili, ambapo hicho kipande kikikaribia asilimia 25 ya urefu wa huo uwazi kutokea kwenye ukuta kuja katikati ya dirisha unakikunja kielekee juu kufungwa na nondo za juu kila upande (kulia na kushoto) na pia kipitilize walau kwa futi moja na nusu kutokea kwenye ukuta
Katika udongo wa mfinyanzi, pendelea kuanza na reinforced strip footing (hii kwa kiswahili sijui niite vipi, kiufupi ni zege nene yenye nondo ndani yake ambayo inakuwa inamwagwa kuzunguka msingi wote kabla ya kuanza kupanga tofali/mawe).Nikupongeze mkuu kwa elimu unayoitoa..swali langu kwako ni moja tuu..
Ni kwa namna gani unaweza kujenga msingi wa mawe kwenye ardhi ya udongo wa mfinyanzi..??
Nitawaletea ndghaya maelezo yangekua na kamchoro ingekua safi
Inaweza kughalimu kiasi Gani mpk inakwisha?Ramani ya vyumba viwili (vyote self), sebule, jiko, dining na choo cha jumuiya
+255(0)624068809View attachment 2969197
Hii bado sijaifanyia mahesabu yake ndg, makadirio yake yatakuwa tayari ndani ya siku mbili tatu hiziInaweza kughalimu kiasi Gani mpk inakwisha?
Asante.
Kazi ni kipimo Cha utu
10mm hapana mkuu, sikushauri. Yote hayo watu wanayafanya ili kukwepa ama kupunguza gharama ambazo baadae inaweza ikakuingiza hasara zaidi.Kuna fundi kanambia nyumba ya kawaida nondo za mm10 zinatosha kabsa
hii imekaaje?
Kitaalam inatakiwa ipigwe baada ya plaster (juu ya plaster)Hv chupping si wanapga bila plaster
Ili kupunguza gharama hatuwez pta shortcut 😁😁Kitaalam inatakiwa ipigwe baada ya plaster (juu ya plaster)
Katika ujenzi, ni vyema ukafuata hatua zote bila kuruka hatua yoyote maana kuja kurekebisha madhara yatakayojitokeza baadae unaweza ukajikuta unatumia gharama kubwa kuliko gharama za ile hatua uliyoirukaIli kupunguza gharama hatuwez pta shortcut [emoji16][emoji16]
Mkuu ni material gani nzuri kwa skimming kati wall putt, gipsum powder na White cementWapo wanaokwepa hatua ya skimming wakidhani kwamba wanapunguza gharama, mtu amemaliza kupiga ripu (plaster) halafu anapiga rangi. Ukuta ambao haujafanyiwa skimming, ukipaka rangi juu yake rangi nyingi inafyozwa na ukuta na hautakuwa na muonekano mzuri ukilinganisha na ukuta uliofanyiwa skimming kisha ukapakwa rangi