Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #621
mpaka wanachanganya izo ratio nitakua nazijua kabsaaUkishinda site kinachofata ni kukukomoa, mahali ambapo panahitajika mifuko mitatu ya cement, wenyewe watachanganya mifuko mitano. Lengo lao hasa ni kukutia hasara zaidi baada ya wewe kuamua kuwabana kupita kiasi
Ukinunua au kuagiza kupitia kwa wakala wao, bei huwa inapungua kidogo. Nafikiri wamefanya hivi makusudi ili kupunguza mrundikano wa wateja kiwandani.Hivi inakuaje bati la simba dumu kiwandani apa Arusha wanauza 40,9000 kwa bando alafu mtaaani bando ni 390k wengine 380k hii imakaaje asee nimeshindea kuelewa
haya bati la versatile online Alaf wameandika 27,800/m kiwandani nimeambiwa 28,200/m
sasa kuna faida gan ya kusema naenda kiwandani?
Mtalamu kwa mjengo wa ghorofa moja,nini kianze kati ya nguzo na ukuta? Pia kati ya ukuta na slab?Ujenzi wa nyumba huwa unaenda kwa mtiririko maalum. Ukivuruga huo utaratibu, unaweza ukaingia gharama zaidi na pengine hata jengo lako kupata madhara licha ya kufata standards zote za ujenzi
Mfano kati ya ripu (plaster) na sakafu (rough floor), inatakiwa ianze sakafu kisha ripu ndio ifatie (plaster ya kuta isimame juu ya sakafu) vinginevyo nyufa zitajitokeza katika maungio ya sakafu na kuta
Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
Kuta ndio zinatakiwa zianze kujengwa, ambapo utakuwa unaacha nafasi ya nguzo katika makutano ya kuta. Zikishakamilika kuta, unafunga box zako then unamimina zege.Mtalamu kwa mjengo wa ghorofa moja,nini kianze kati ya nguzo na ukuta? Pia kati ya ukuta na slab?
Umesomeks vizuri mkuu.Kuta ndio zinatakiwa zianze kujengwa, ambapo utakuwa unaacha nafasi ya nguzo katika makutano ya kuta. Zikishakamilika kuta, unafunga box zako then unamimina zege.
Ila kwa msingi, unatakiwa umwage kwanza vitako (base) vya nguzo ili zile tofali zinazokaribiana na nguzo zilale juu ya base (wakati huo unakuwa umeshasuka nondo za nguzo na kitako chake, ndipo unamwaga zege kwenye base)
Lakini hii ni kwa majengo ya kawaida sio framed structure (nikisema framed structure namaanisha majengo kama yale maghorofa ya Kariakoo, ambapo huwa wanaanza kutengeneza frame ya jengo (nguzo,mkanda na slab) then kuta zinakuja kujengwa mwishoni au kila baada ya ghorofa moja kukamilika
Kipengele cha pili, kati ya kuta na slab huwa inaanza slab maana kuta huwa zinakaa juu ya slab (mahali ambapo chini ya slab kunakuwa na mkanda)
。✅Umesomeks vizuri mkuu.
Kipengele cha pili nilimaanisha kuta za chini ya slab. So, kupitia maelezo yako ya juu nimekuelewa pia. Kwamba kwa kuwa tunaweka kuta then guzo, maana yake slab itawekwa baada ya nguzo na ukuta wake kukamilika
Baada ya kuta na nguzo kukamilika, kinachofata ni kuweka mkanda (beam), ambapo wakati unasuka nondo za beam, unakuwa unasuka pia na nondo za slab na pia unakuwa umeshatengeneza box lako la beam na slab (ukimwaga zege, unamwaga pote kwenye slab na beam)Umesomeks vizuri mkuu.
Kipengele cha pili nilimaanisha kuta za chini ya slab. So, kupitia maelezo yako ya juu nimekuelewa pia. Kwamba kwa kuwa tunaweka kuta then guzo, maana yake slab itawekwa baada ya nguzo na ukuta wake kukamilika