Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ulishawahi kuona mahali nyufa zinatokea katika kuta kabla hata ya udongo(mortar) kukauka?

Sasa hiyo hali huwa inasababishwa na udongo kuwa na maji mengi katika uchanganyaji. Udongo ambao unakuwa na maji mengi bado unakuwa na mjongeo (slump) kwa hivyo kadri unavyoendelea na ujenzi na wenyewe unakuwa unashuka chini taratibu taratibu na kufanya huo udongo uachane na tofali.

Udongo wa kujengea unatakiwa uwe mgumu kiasi kwamba hata ukichukua ndoo ukaujaza huo udongo, kisha ukaumwaga mahali, ile shape ya ndoo unakuwa unaiona na sio kutawanyika wote chini (collapse)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika nyumba yako epuka sana kutumia vitu ambavyo vinakuwa na ncha kali kwa sababu ikitokea mfano mtu amejigonga kwa nguvu bahati mbaya, madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa...mtu anaweza hata akapasuka kama amejigonga sehemu yenye mfupa

Vitu hivyo ni vingi, nitavitaja vichache

1. Nguzo za zege (kibarazani). Hizi wakati wa kupiga plaster, usitumie chuma kona ya nyuzi 90 net (hapa utakuwa unajitengenezea kisu mwenyewe), tumia chuma kona ambayo inakuwa na curve kwa ndani ili kusiwepo na hiyo ncha

2. Frem za milango
Ukiangalia frem za milango ya kisasa, utagundua zile ncha zake zina curve badala ya nyuzi 90 iliyozoeleka

3. Maungio ya tiles za kusimama na tiles za kulala.
Hapa huwa inatumika corner strip (hiki ni kama kibati ambacho kinakuwa na curve kwa nje). Mara nyingi utakiona katika ngazi au mahali ambapo kuna step kati ya floor mbili tofauti

4. Mable za jikoni
Hizi ukiziangalia, utaona upande mmoja una curve na upande mwingine una ncha. Upande wenye ncha ndio unatakiwa uwe ukutani, na upande wenye curve uwe huku mbele

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukishinda site kinachofata ni kukukomoa, mahali ambapo panahitajika mifuko mitatu ya cement, wenyewe watachanganya mifuko mitano. Lengo lao hasa ni kukutia hasara zaidi baada ya wewe kuamua kuwabana kupita kiasi
mpaka wanachanganya izo ratio nitakua nazijua kabsaa
 
Namba ya msumeno inawakilisha idadi ya meno katika kila urefu wa nchi moja katika msumeno

Mfano msumeno namba 18 maana yake katika kila urefu wa nchi moja wa msumeno, kuna meno 18 (Huu ndio msumeno ambao unatumika sana site katika zoezi la ukataji wa nondo)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika majengo makubwa kama makanisa, kumbi za mikutano n.k huwa tunatumia chuma (trusses) katika upauaji badala ya mbao ili kupunguza uzito wa paa, lakini pia ni ngumu kupata mbao ya urefu unaohitajika tofauti na ilivyo kwenye chuma

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Hivi inakuaje bati la simba dumu kiwandani apa Arusha wanauza 409,000 kwa bando alafu mtaaani bando ni 390k wengine 380k hii imakaaje asee nimeshindea kuelewa

haya bati la versatile online Alaf wameandika 27,800/m kiwandani nimeambiwa 28,200/m

sasa kuna faida gan ya kusema naenda kiwandani?
 
Hivi inakuaje bati la simba dumu kiwandani apa Arusha wanauza 40,9000 kwa bando alafu mtaaani bando ni 390k wengine 380k hii imakaaje asee nimeshindea kuelewa

haya bati la versatile online Alaf wameandika 27,800/m kiwandani nimeambiwa 28,200/m

sasa kuna faida gan ya kusema naenda kiwandani?
Ukinunua au kuagiza kupitia kwa wakala wao, bei huwa inapungua kidogo. Nafikiri wamefanya hivi makusudi ili kupunguza mrundikano wa wateja kiwandani.

Ingekuwa bei ya mtaani ni kubwa kuliko bei ya kiwandani, hawa wenye maduka wangeshayafunga maduka yao muda mrefu maana watu wangekuwa wanaenda kununua kiwandani moja kwa moja.

Kingine, ukipitia kwa wakala order yako kule kiwandani inafanyiwa kazi haraka tofauti na ukienda mwenyewe kiwandani kuweka order

Mawakala huwa wanauziwa kwa bei yao (jumla) ili na wao wakiuza wapate faida/mgao katika kila mauzo wanayofanya lakini wewe ukienda, wanakuuzia kwa bei ya reja reja ambayo inatakiwa iwe kubwa kuliko bei ya mtaani ili mawakala na wafanyabiashara wasikose wateja
 
Wakati mwingine ni ngumu kupata tofali zinazolingana upana kutokana na hizo tofali kufyatuliwa kwa kutumia machine/watu tofauti tofauti.

Upana halisi wa tofali ni sentimita 23 (sawa na 230mm), lakini wakati mwingine unaweza ukapata tofali ambazo hazitimii huo upana wa 23cm (mfano tofali zinaweza zikawa na upana wa 22.5cm, 22cm n.k) kutokana na kushindiliwa kupita kiasi, lakini pia unaweza ukapata tofali ambazo zinazidi huo upana wa 23cm kutokana na kushikiliwa kidogo au mould ya machine ikawa imezidi kipimo kinachohitajika

Ukienda kununua tofali, kama utakuta kuna machine zaidi ya moja, muambie muuzaji akupatie tofali zilizofyatuliwa na machine moja (asikuchanganyie tofali zilizofyatuliwa na machine tofauti tofauti) ili kuepuka huo utofauti

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
20240713_095448.jpg
 
Usiogope kujenga nyumba ya ndoto yako kwa sababu ya uchumi mdogo

Unachotakiwa kufanya ni kujenga msingi wote kwanza, kisha huku juu unakuwa unainunua boma kidogo kidogo kwa kuacha matoleo ya tofali sehemu zote ambazo zitahitaji kuunganisha kuta baadae.

Ukifanya hivi, utajikuta unakamilisha ujenzi ndani ya muda mfupi (miaka miwili, mitatu n.k) kwa sababu utakuwa unajenga kwa malengo tofauti na kusubiri upate pesa yote mara moja kwa mkupuo ndipo uanze ujenzi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika zoezi la ushindiliaji wa kifusi katika msingi, maji huwa yanatumika kwa lengo la kuondoa hewa (air voids) katika udongo, lakini maji yanapozidi kupita kiasi na kufanya udongo uloane (fully saturated), inasababisha nguvu ya msukumo wa udongo (earth pressure) katika kuta iongezeke zaidi ambapo matokeo yake unaweza ukafika site asubuhi ukakuta kuna nyufa kila mahali katika msingi (kuta).

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Wakati mwingine unaweza ukashindwa kuendelea mbele na ujenzi kwa sababu kuna watu uliwafanyisha kazi, lakini haki zao ukawadhulumu

Lakini pia Mungu anaweza akakuacha ukafanya ujenzi wako hivyo hivyo kwa dhulma dhulma, na baada ya nyumba kukamilika, hiyo nyumba isidumu hata miaka mitano ukaipoteza (kuungua, kukuingiza hasara katika matengenezo kila kukicha na mabalaa mengine) yote ni kwa sababu kuna watu wanalilia haki zao kwako na hutaki kuwalipa.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kama paa lako litakuwa na mlalo (slope) mdogo, utalazimika kuweka vibao (spacer) wakati wa kufunga bomba za mikingio ya maji (gutter) vinginevyo maji ya mvua yatakuwa yanamwagikia nje ya mkingio

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ujenzi wa nyumba huwa unaenda kwa mtiririko maalum. Ukivuruga huo utaratibu, unaweza ukaingia gharama zaidi na pengine hata jengo lako kupata madhara licha ya kufata standards zote za ujenzi

Mfano kati ya ripu (plaster) na sakafu (rough floor), inatakiwa ianze sakafu kisha ripu ndio ifatie (plaster ya kuta isimame juu ya sakafu) vinginevyo nyufa zitajitokeza katika maungio ya sakafu na kuta

Mtalamu kwa mjengo wa ghorofa moja,nini kianze kati ya nguzo na ukuta? Pia kati ya ukuta na slab?
 
Mtalamu kwa mjengo wa ghorofa moja,nini kianze kati ya nguzo na ukuta? Pia kati ya ukuta na slab?
Kuta ndio zinatakiwa zianze kujengwa, ambapo utakuwa unaacha nafasi ya nguzo katika makutano ya kuta. Zikishakamilika kuta, unafunga box zako then unamimina zege.

Ila kwa msingi, unatakiwa umwage kwanza vitako (base) vya nguzo ili zile tofali zinazokaribiana na nguzo zilale juu ya base (wakati huo unakuwa umeshasuka nondo za nguzo na kitako chake, ndipo unamwaga zege kwenye base)

Lakini hii ni kwa majengo ya kawaida sio framed structure (nikisema framed structure namaanisha majengo kama yale maghorofa ya Kariakoo, ambapo huwa wanaanza kutengeneza frame ya jengo (nguzo,mkanda na slab) then kuta zinakuja kujengwa mwishoni au kila baada ya ghorofa moja kukamilika

Kipengele cha pili, kati ya kuta na slab huwa inaanza slab maana kuta huwa zinakaa juu ya slab (mahali ambapo chini ya slab kunakuwa na mkanda)
 
Umesomeks vizuri mkuu.
Kipengele cha pili nilimaanisha kuta za chini ya slab. So, kupitia maelezo yako ya juu nimekuelewa pia. Kwamba kwa kuwa tunaweka kuta then guzo, maana yake slab itawekwa baada ya nguzo na ukuta wake kukamilika
 
。✅
 
Baada ya kuta na nguzo kukamilika, kinachofata ni kuweka mkanda (beam), ambapo wakati unasuka nondo za beam, unakuwa unasuka pia na nondo za slab na pia unakuwa umeshatengeneza box lako la beam na slab (ukimwaga zege, unamwaga pote kwenye slab na beam)
 
Back
Top Bottom