Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kama uchumi hauruhusu kuweka mkanda wa chini, basi ile kozi ya mwisho ya msingi na kwenye kona zote jengea tofali zenye vile vikokoto (huwa inaongezeka sh 100 ktk bei ya tofali za kawaida yaani cement & mchanga bila vikokoto)

Uimara wake hauwezi ukawa sawa na mtu aliyefunga mkanda lakini haiwezi ikawa sawa na mtu aliyejengea tofali za kawaida pote. Tofali zenye vikokoto zina compressive strength kubwa kulinganisha na tofali za kawaida hivyo itaongeza uimara zaidi
 
Katika ujenzi, maji huwa tunayacontrol kwa kuyawekea slope. Unapoweka tiles ktk floor ya kibaraza, jitahidi kuwe na slope (slope ndogo sana ambayo haiwezi kuonekana kwa macho, kumbuka utofauti wa kimo kati ya sehemu moja na sehemu nyingine hata kama ni kwa kiasi cha milimita 2 inatosha kabisa kufanya maji yasituame sehemu hiyo).

Ukiweka slope, ile mvua ya upepo inaponyesha maji yanakuwa hayakai kibarazani (yanaondoka yenyewe kutokana na kamuinuko ulikokaweka), tofauti na hapo utakuwa na kazi ya kuyaondosha kwa mikono kila muda

Ramani, Makadirio, Ushauri kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Hii ramani ,, nyumba yake inaweza cost kama Shilling ngapi?
 
Hii ramani ,, nyumba yake inaweza cost kama Shilling ngapi?
Inategemea na mkoa unapotaka kujenga maana bei za material hazifanani, lakini pia inategemea na aina ya umaliziaji wa nyumba (finishing). Mwingine anaweza akaweka dirisha za mbao na wavu, mwingine akaweka grill na aluminium
Kama ni Dsm, ukiwa na milion 20 mpaka milion 25 unamaliza bila shida
Kiujumla factors ni nyingi, nyumba hiyo hiyo inaweza ikajengwa na watu wawili tofauti, sehemu moja na bado wakapishana gharama
 
Niko n swali hv mtu akishindwa kuweka mkanda kwenye msingi wa fensi si anaweza kuweka lile nailoni turubai. Au ni nailoni special? Je linaitwaje?
Asante
 
Ramani, Makadrio na Ushauri wa kitaalam kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Alishakupa mkuu ama
 
Takataka hii
 
Takataka hii
Sawa ndg, All in all jaribu kuheshimu kitu kinachompatia mtu riziki hata kama kwako hakikufai kwa maana ni Mungu Mwenyezi ndiye aliyempangia apate riziki kupitia kitu hicho. Haijalishi una mali kiasi gani, una cheo gani maisha ni mapito hivyo hakuna sababu yoyote inayoruhusu binadamu kudharauriana. Ramani yangu ni takataka sawa, lakini kuna elimu pia naitoa hapo mbali na kuuza ramani (hata hiyo pia haikufai?)
 
Ramani, Makadrio na Ushauri wa kitaalam kuhusu ujenzi tuwasiliane
 
Jamiiforums ni msaada mkubwa sana kwenye ulimwengu wa leo unaohitaji akili na matumizi sahihi ya pesa,post za mdau Hechy Essy zimenifungua akili kama hivi alivyoandika ningevijua mapema vingenisaidia sana.

Kwenye ujenzi tusiogope kutumia washauri kisa kukimbia gharama mimi sikuwa na akili hii majibu yake nimeshayaona,kwa mnaoanza ujenzi tafadhalini watumieni watu kama hawa watawasaidia sana.
 
Mtaalamu hayo matundu yanasaidia nini?

Yasipowekwa itatokea shida gani ktk msingi au nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…