Hechy Essy
JF-Expert Member
- Mar 30, 2023
- 640
- 2,413
- Thread starter
-
- #161
Kampuni gani ina bat zuri za hizo versatile/ romantilBinafsi sikushauri utumie huo mfumo wa kuficha paa kwa sababu kwanza inahitaji umakini mkubwa sana katika upauaji, unaweza ukajikuta unaingia kwenye hasara ya kubadilisha huo mfumo ndani ya miezi michache ijayo.
Hiyo milion 10 mpaka 12 mbona ni nyingi sana? Au unatumia bati za versatile / romantile?
Ni huyo huyo ALAF, mpinzani wake (no. 2) nadhani ni kampuni ya SunshineKampuni gani ina bat zuri za hizo versatile/ romantil
Swali je kuchanganya nchi 6 Kwa nje na ndani 5 muingiliano unakubali kwenye jointKama mfuko unaruhusu, kuta zote zinazozunguka nyumba kwa nje tumia tofali za nchi 6...hii itakupa nafasi ya kutosha kuweka madirisha ya grill na aluminium katika muonekano mzuri zaidi lakini pia kwenye milango ya nje ambayo inakuwa na mlango wa mbao na geti la grill. Ukuta wa nchi 6 ukipigwa plaster ndani na nje unene wake utakaribia/kufikia nchi 7
Leo tuangalie upande ambao SEBULE na VYOO vinapotakiwa vikaeKabla hujaanza ujenzi, ni vizuri ukajua upande ambao jua huwa linachomoza (mashariki)...Mada ni ndefu, kwa leo nitaelezea upande ambao jiko (kitchen room) linatakiwa likae
Jiko linatakiwa likae upande wa Kusini Mashariki ambapo mida ya asubuhi jua linakuwa ni la wastani (jua la vitamin D, hapa mpishi atapata muda wa kuandaa breakfast akiwa comfortable kabisa), baada ya hapo jua litakuwa linaendelea kuhama taratibu ambapo mpaka kufikia mida ya saa tano tano kuelekea saa sita, jua litakuwa lipo juu ya nyumba linapiga bati kwa juu (hapa pia mpishi atakuwa katika mazingira rafiki kuandaa chakula cha mchana bila kusumbuliwa na joto la jua)
Ramani, Makadirio, Ushauri tuwasiliane
Ndio mkuu, tofali zote zinakuwa zinasimamishwa (utofauti utakuwepo kwenye unene wa tofali, ambao wenyewe hauna shida kwa sababu haziunganishwi parallel)Swali je kuchanganya nchi 6 Kwa nje na ndani 5 muingiliano unakubali kwenye joint
Nipe namba yakoPLN 0001 2BR
Ramani ya Vyumba Viwili
- Living room (Sebule)
- 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
- 1 Single bedroom
- Kitchen (Jiko)
- Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana
Bei: Tsh. 100,000/=
Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
+255(0)624068809Nipe namba yako
Ubarikiwe mkuu kwa kutoa hints mbali mbali kuhusu umeme lakini sio busara kutangaza biashara yako kwenye uzi wa mtu mwingine ambaye nae pia yupo kibiashara. Chochote kitakachotokea baina yako na mteja, mimi pia naweza nikahusishwa, mtu anaweza akakupigia wewe akajua anaongea na mimi kwa sababu namba ameikuta kwenye uzi niliouanzisha mimi.UFUNDI UMEME
(1) Hata kama unampa ela ya vifaa fundi basi ni vizuri kuakikisha alichokiandika ni sahihi maana mafundi uwa tuna tamaa baada ya ela kuwa mikononi.unakuta fundi kakuandikia waya(kampuni ya euro)ila unashangaa analeta site waya usiojulikana.hii ni hatari sana kwa usalama wako na vifaa vyako.
(2) Kabla ya kufanya wiring ni vizuri wewe muhusika kumwambia fundi maitaji yako yote ya vitu ambavyo utakuja kutumia baadae ili isije ikatokea changamoto ya kufanya upanuzi wa maitaji mengine ya umeme.mfano kwenye stage ya kwanza(kuchimbia bomba) ni vizuri kuweka point nyingi ili hata ikitokea unaitaji kuongeza kibu basi kusiwe na changamoto.
(3) hakikisha umeme wowote unaopita chini ya ardhi basi ununue waya maalum kwa ajili ya chini ya ardhi.sio kila waya una uwezo wa kupita chini ya ardhi.hii baadae itakuja kukuletea shida wakati huo utashindwa kufanya kitu kwa sababu gharama ya marekebisho itakuwa kubwa.
(4)Hakikisha unanunua vifaa vya umeme ambayo kwa ndani vimetengenezwa kwa copper na sio chuma kilicholambishwa copper.kampuni yenye vifaa vilivyotengenezwa kwa pure copper kwa hapa nchini ni( Tronic,ABB,Africab,havels)
(5)Hakikisha fundi anatumia bomba kwenye kufanya wiring na pia anafunga na mifuniko kwenye sehemu zenye juction box ili kuzuia wadudu kufika kwenye switch au main switch.
(6) Hakikisha fundi anaorodhesha matumizi yako yote kwenye kuomba mita tanesco ili usije ukapewa mita ndogo ukashangaa umeme unaenda mwingi kumbe mita inazidiwa.hakikisha taarifa za matumizi alizoweka kwenye mchoro ni sahihi.
Kwa ushauri na kazi nicheki 0652868486
Futa hii post mkuuUbarikiwe mkuu kwa kutoa hints mbali mbali kuhusu umeme lakini sio busara kutangaza biashara yako kwenye uzi wa mtu mwingine ambaye nae pia yupo kibiashara. Chochote kitakachotokea baina yako na mteja, mimi pia naweza nikahusishwa, mtu anaweza akakupigia wewe akajua anaongea na mimi kwa sababu namba ameikuta kwenye uzi niliouanzisha mimi.
Kuanzisha uzi ni bure, hakuna malipo yoyote...kwanini na wewe usiwe na uzi wako ukajibrand wewe kama wewe?!!
Mtu kutangaza biashara yake ndani ya uzi wa mtu mwingine inafanya wateja wasikuamini kwa sababu ni rahisi kufuta comment kuliko kufuta uzi hasa pale kunapotokea tatizo baina ya mteja na mtoa huduma