Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kipindi cha mvua kubwa, nyumba nyingi utaona zile bomba za kukingia maji ya mvua (gutter) zinan'goka. Kitaalam ni vizuri kila upande wa nyumba ukaweka down pipe moja ya kushusha maji chini lakini pia gutter ukiiweka level, maji yanakuwa yanatuama kwenye bomba bila kutembea.

Inatakiwa wakati wa kufix gutter, fundi atumie pima maji ambapo anatakiwa aweke slope ndogo sana ambayo haiwezi kuenekana kwa macho ili maji yanapokuwa yanaingia kwenye bomba yawe yanaondoka muda huo huo kuelekea mahali unapotaka yaende
 
Je? Nitajuaje kua hii Gauge 28 na sio G30?
Asante
Mfano hii hapa ni simba dumu ya gauge 32
20240202_115541.jpg
 
ikiwa plot iko level tu.... pasi na Mabonde... Inashauriwa Msingi uwe na Kozi ngapi za Matofali? Njia gani rahisi ya kuepuka Gharama za Kujaza Kifusi ndani ya Msingi?
 
Msingi kama msingi kwa nyumba za chini (sio za ghorofa) inashauriwa kina chake kisiwe chini ya futi 3 kutokea chini mpaka juu ya level ya mkanda. Kutokea kwenye usawa wa ardhi yaani ground floor mpaka juu ya mkanda atleast urefu uwe ni futi moja na nusu (kwa hivyo juu ya ardhi zitokee walau kozi mbili ndipo ufunge mkanda, ukiweza weka hata kozi tatu). Na kutokea usawa wa ardhi kwenda chini ya msingi angalau kina kiwe ni futi 2 au zaidi sawa na kozi 3 kama utatumia tofali za nchi 6
 
kuna jamaa anachambua pale youtube nyumba ya room 3 sebule dining jiko stoo public toilet ukiw na 10M unafikisha kupaua .. kuna uhalisia apa kwel?
 
Ndio, uwezekano upo inategemea na namna ya ujenzi lakini na bei pamoja na aina za material yaliyotumika maana boma pekee material cost inarange kwenye 7milion to 8M..mfano wengine mkanda wa chini hawaweki kwa hivyo kuna saving anakuwa amefanya
 
kwa maana hiyo nyumba ya standard room 3 sebule dining n.k 10M inatosha boma kabisa mpaka ela ya fundi
 
kuna jamaa anachambua pale youtube nyumba ya room 3 sebule dining jiko stoo public toilet ukiw na 10M unafikisha kupaua .. kuna uhalisia apa kwel?

Mkuu hawa wanaojiita mamotivesheni sipika ni watu wa hovyo hovyo sana wakati mwingine
 
Mkuu nina tofali za inch 5, je ninaweza tumia kujengea msingi wa nyumba ya vyumba vinne? Au ni lazima nikomae nitumie tofali za nchi 6, maana tatizo bajeti yangu nayo haipo sawa...eneo ni flat na lina nature ya kichanga
 
Tumia bila shaka Mkuu
 
kwa maana hiyo nyumba ya standard room 3 sebule dining n.k 10M inatosha boma kabisa mpaka ela ya fundi
Hapana, hiyo ni material tu..tena hapo ubane bane sana (mfano mkanda wa chini utumie nondo 3 badala ya 4, mawe kwemye msingi uachane nayo n.k)
 
Mkuu nina tofali za inch 5, je ninaweza tumia kujengea msingi wa nyumba ya vyumba vinne? Au ni lazima nikomae nitumie tofali za nchi 6, maana tatizo bajeti yangu nayo haipo sawa...eneo ni flat na lina nature ya kichanga
Tumia tu hizo hizo japo ungetumia za nchi 6 ingekuwa vyema zaidi, kwanza ungejenga kozi chache kulinganisha na tofali za 5 kwa kina kile kile cha msingi
 
uhalisia upoje?
Chukulia mfano tofali ni 3500 (hapo tayari 3.5M), chukua cement za kujengea mifuko 70 (hiyo ni 1,225,000/=), nondo 50 mkanda wa chini na wa juu (hiyo ni 1,300,000/=) mpaka hapo ni almost 6M+...bado kokoto, mchanga na vitu vitu vingine (ukija kwenye kupaua napo kuna shughuli, bati tu kama bati unaacha 2M+, bado mbao n.k
 
Tumia tu hizo hizo japo ungetumia za nchi 6 ingekuwa vyema zaidi, kwanza ungejenga kozi chache kulinganisha na tofali za 5 kwa kina kile kile cha msingi
Ntatumia za nchi 5 tu mkuu,maana nikichek cost yake ndogo, afu kuhusu idadi ya kozi sitegemei kama ntaenda kozi zaid ya sita kwenye msingi
 
Udongo wa kujengea unatakiwa usiwe mlaini, inatakiwa ukichota chepe la huo udongo na kuumwaga chini, udongo usisambae chini bali utengeneze kamlima. Madhara ya kutumia udongo (mortar) mlaini ni kutokea kwa nyufa katika maungio kati ya tofali na mortar baada ya huo udongo kushuka chini (kunywea)
 
4 bedroom house
  • Master 1 yenye kibaraza chake, unaweza ukaingia ama kutokea mlango huo (ramani nzuri sana kwa wadaiwa sugu)
  • Self 1
  • Single 2
  • Jiko
  • Dining
  • Store
  • Library/Pray room
  • Public toilet 2

Chumba cha master kipo mbali sana na vyumba vingine, hata kitanda kikiwa kibovu kunakuwa hakuna shida yoyote
20240208_213647.jpg
 
Back
Top Bottom