Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Attachments

  • IMG_20240813_214936_396.jpg
    IMG_20240813_214936_396.jpg
    52.5 KB · Views: 14
Wakuu naomba ushauri wa kitalaamu kuhusu tofali za msingi wa ghorofa. Upper floor ni 50sqm, ambayo itakuwa na chumba masta na common bed room. Ardhi ni mfinyazi.
Je, tofali za msingi ziwe na ratio ipi standard(mfuko mmoja saruji 42.5N utoe tofali ngapi)?
 
🤣 achan naufup wa nyumba nimeipiga tu maali ila at mimi nilimlaumu mwenye nyumba kwa nini kalaza msingi chini sana badala yakuutoa nje ata kozi 3 au nne
Kutokujua tu na pia fundi huwa wanatakiwa kujiongeza, fundi mzuri asingejenga hivyo
 
Wakuu naomba ushauri wa kitalaamu kuhusu tofali za msingi wa ghorofa. Upper floor ni 50sqm, ambayo itakuwa na chumba masta na common bed room. Ardhi ni mfinyazi.
Je, tofali za msingi ziwe na ratio ipi standard(mfuko mmoja saruji 42.5N utoe tofali ngapi)?
25, muhimu ziwe compressed na mixed vizuri

Kwa nn cement ya 42.5N na sio 42.5R?
Lakini pia kwa nn 42.5 na sio 32.5 au 52.5??

Mafundi wengi na baadhi ya builders sasa hivi wanawakaririsha sana watu, wamefanya hadi cement za 32.5 hazihuziki madukani
 
Kabla ya kumwaga zege la jamvi chini, hakikisha unamwaga mchanga wa kutosha. Usiruhusu zege yako igusane moja kwa moja na udongo maana huwezi jua udongo una madini gani ambayo yanaweza kupambana na cement na kuua au kupunguza nguvu yake

Hata kama utakuwa umeweka mawe, mchanga pia inabidi umwage juu ya mawe ili uende kuziba nafasi iliyopo kati ya jiwe moja na jiwe lingine (wakati mwingine zege inashindwa kupita katika hizi nafasi hivyo usipomwaga mchanga, chini kutabaki matundu mengi)

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuliko kuweka bawaba mbili kwenye mlango (yani juu moja na chini moja), ni vyema ukaongeza bawaba nyingine kati kati, jumla ziwe bawaba tatu ili kuongeza flexibilty ya mlango

Pia jitahidi kila mlango uuwekee door stopper kwa nyuma ili mlango unapofunguka mpaka mwisho usiende kugonga na kuchubua ukuta

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kabla ya kupigilia mbao za dari, angalia kwanza na uhalisia wa vipimo upoje ili ujue ni namna ipi ukielekeza board zako utamaliza ukiwa na wastage (vipande ambavyo haviwezi kutumika tena) chache

Wakati mwingine unaweza ukakutana na chumba ambacho ukipangilia vizuri board zako hubakiwi na kipande chochote, lakini ukigeuza ueleko unajikuta board hizo hizo hazitoshi kumaliza hicho chumba kutokana na wastage

Mkuu kuna slab siku hizi zipo namna hiyo hapo chini naomba nijuze unayofahamu kuhusu slab hizi maana wanadai zinapunguza sana gharama but nina mashaka kuhusu ubora in the long run.
4ff8008d-f88d-4e32-bea7-4ea54c0c93d0.jpeg
e6922b9b-da62-40ca-8d53-ba8d15042070.jpeg
IMG-20211125-WA0002-e1644410347741.jpg
Screenshot (1774).png
 
Back
Top Bottom