Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Kitaalam hapo kwenye kibaraza ilitakiwa pawe chini kwa kozi moja ukilinganisha na level ya msingi wa nyumba ili mtu akiingia hapo mlangoni (sebuleni) apande step moja. Hizo kozi 5 zinazoonekana kwenye kibaraza ilitakiwa ziwe kozi 4 badala ya 5

Upande wa nguzo, nondo zilizotokeza juu kwa ajili ya kuungana na nondo za juu zina urefu mdogo (angalau zingekuwa zimefika urefu wa futi mbili ili zifungwe ringi 4 kwa nafasi ya sentimita 15)

Kingine cha kuwasisitiza mafundi wako waambie wajitahidi kutumia kobilo pande mbili za tofali maana ukiangalia vizuri hizo kuta utaona kuna tofali nyingi zimeinama. Upande mmoja wa tofali ni kwa ajili ya kuliset tofali likae wima, na upande mwingine ni kwa ajili ya kuliset tofali likae mlalo ulionyooka (horizontal)

Unaweza ukanunua hayo material uliyotaja na kuyaweka humo bila shida yoyote lakini je kiusalama hali inaruhusu?, wanaweza wakawa wanakuibia usiku kwa kusombelea na kuhamisha kidogo kidogo mpaka wakamaliza material yote
View attachment 3129227
Mkuu Mungu akubariki sana. Nimeelewa vizuri sana.
Kuhusu kozi moja ya kibalaza hapo nifanyeje mkuu. Au niongeze kifusi ndani nipandishe level ya flour ya mpaka mlangoni kwa urefu sawa na kozi moja?

Pia hii ya kutotumia kobilo na tofali kuingia ndani inaweza kuwa na madhara gani huko mbeleni? Hasa kwenye uimara wa jengo.

Natanguliza shukrani mkuu.
 
Strength ya tofali zilizosafirishwa
Nimekuwa na plan ya kupiga tofali za msingi wa ghorofa eneo tofauti na ilipo site kwa sababu ya changamoto ya maji. Plan ni tofali za ratio ya 25 kwa mfuko.
Engineer anasema nipigie palepale site kwa sababu za kusafirisha strength inapungua. Safari ni ya kama kilomita 5 tu hivi

Yana ukweli haya?
 
1. Kutengeneza step moja inayolingana na unene wa kozi moja kwa kutumia hiyo rough floor ni gharama sana, cement na kokoto zitamezwa nyingi

Hapo cha kufanya, tindua kidogo zege ya mkanda hapo kwenye kibaraza angalau nchi 2 ili zege la jamvi lije kumwagwa juu ya mkanda (jamvi la kwenye kibaraza liwe level moja na mkanda wa nyumba nzima)

Huko ndani jaza kifusi mpaka level ya mkanda halafu ndio umwage jamvi la nyumba nzima (hata ukiweka zege ya nchi 3 sio mbaya, sio lazima mpaka ifike unene wa kulingana na kozi moja). Kama utaweka mawe, basi mawe yako ndio yalingane level na mkanda.

Ukisema uunge zege ya jamvi pembeni ya mkanda, uwezekano wa kutokea ufa kwenye floor ni mkubwa ndio mana huwa inatakiwa zege mpya ilale juu ya zege ya zamani

2. Ikitokea jengo limeshuka (kusettle), uwezekano wa nyufa kutokea kwenye kuta ni mkubwa kwa sababu tofali zimeungana lakini zimepishana level lakini pia kwenye zoezi la upauaji litamsumbua fundi kupaua kutafuta level kwa kutumia vibao, unakuta sehemu moja fundi anaweka wall plate ubao mmoja lakini sehemu zingine anaweka vibao zaidi ya kimoja ili paa likae sawa lisiiname

Hapo inabidi wakati wa kufunga box la huo mkanda wa juu, waambie watumie PIPE LEVEL ili kufanya jengo lote liwe na level moja, na pia kwenye kozi ya mwisho napo ahakikishe tena
 
Strength ya tofali zilizosafirishwa
Nimekuwa na plan ya kupiga tofali za msingi wa ghorofa eneo tofauti na ilipo site kwa sababu ya changamoto ya maji. Plan ni tofali za ratio ya 25 kwa mfuko.
Engineer anasema nipigie palepale site kwa sababu za kusafirisha strength inapungua. Safari ni ya kama kilomita 5 tu hivi

Yana ukweli haya?
Sidhani kama kuna huo uhusiano wa strength ya tofali na usafirishaji, cha kuzingatia hapo ni ratio tu

Ukifyatulia tofali site, gharama utakayoikwepa ni gharama ya usafirishaji tu ambayo pengine itakuja kutumika tena kwenye zoezi hilo hilo la tofali (no saving).

Hapo itabidi ukodi mashine ya kufyatulia, vibao vya tofali, kuwalipa wafyatuaji tofali na pia maji ya kumwagia hizo tofali mpaka zikomae (huwa inalipa kidogo kama idadi ya tofali ni nyingi, vinginevyo utajikuta unatumia gharama zaidi kuliko ile ya tofali za kusafirisha).

Maghorofa yote unayoyaona huko mitaani kwa asilimia karibu 90, tofali zake ni hizo hizo za kusafirisha kwa hivyo kama kungekuwa na huo uhusiano basi kila site wangekuwa wanafyatua tofali zao huko huko site
 
Madirisha ya wavu huwa yana nyavu mbili, wavu mkubwa na wavu mdogo (wavu wa mbu)

Mafundi wengi huwa wanachanganya madawa, wavu mkubwa wanaupigilia nje na wavu mdogo wanaupigilia ndani

Kitaalam wavu wa mbu ndio unaotakiwa uwe nje, na wavu mkubwa unatakiwa uwe ndani ili hata mtu akitaka kusafisha vumbi kwenye madirisha aende kusafishia nje na sio ndani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kama eneo lako la ujenzi lipo ndani sana (pembezoni mwa mji au mbali na makazi ya watu), usije ukajaribu kununua tank la maji na kuliacha nje ukitegemea kwamba wezi hawatoweza kulibeba

Kwa kesi kama hii, huwa tunachimba shimo na kuliingiza tank kwenye hilo shimo ambapo wezi ili waliibe hilo tank inabidi wachote maji yote na kuyamwaga na kufanya kazi nyingine ya kulifukua

Mkuu ni kama umeikia changamoto yangu. Post yangu ya juu kuhusu tofali kupigia mbali na site ilikuwa ni kwa sababu ya kukosa chombo cha kutunzia maji, tofauti na bomba la mamlaka.

Hapa umenipa akili, kwamba naweza kuchimbia (kwa muda) tenk.
 
Ndio unaweza ukafanya hivyo kwa sababu za kiusalama kwamba lisiibiwe, ila kwa kesi yako ukifanya hivi, zoezi la umwagiliaji tofali litakuwa gumu sana maana itabidi mtu awe anachota na ndoo na kwenda kumwagilia tofali moja moja vinginevyo utaingia gharama ya kutafuta pump ya maji.

Hapo kwa kesi yako itabidi tu tank liwe juu kiasi (unapanga hata tofali kadhaa tu kuzunguka mzunguko wa tank, kati kati unajaza udongo mana ni kwa matumizi ya muda tu), then unatoboa hapo chini unaweka koki kwa ajili ya kuunganisha na mpira wa maji kwa ajili ya kumwagilia hizo tofali.

Kama utafyatua mwenyewe tofali site, inabidi uzingatie na mchanga utakaoutumia. Mchanga unaotumika kufyatulia tofali ni tofauti na huu tunaoutumia kwenye ujenzi. Mchanga wa kufyatulia tofali ni gharama
 
Bawaba nzuri na imara ni zile ambazo zinakuwa na unene (mark) mkubwa lakini pia matundu yake yanakuwa yanapishana (ukiunganisha matundu ya bawaba ya upande mmoja kwa kuchora mstari, unapata mstari ambao ni zigzag)

Hii inasaidia bawaba zako ziwe zimeshikiliwa katika upana wote wa fremu ya mlango hivyo inazuia bawaba kuzunguka kutokana na uzito wa mlango

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ukipachika frem zako za milango kwenye kuta, baada ya muda utaona kuna mwanya unatokea kati ya frem na ukuta. Hii ni kwa sababu mbao na tofali ni vitu viwili tofali (kila kimoja kinatanuka na kusinyaa kwa namna yake pindi kunapotokea mabadiliko ya joto)

Ili huo mwanya usionekane, huwa tunatumia mbao nyembamba (architrave) kupigilia hiyo sehemu ambayo inaficha huo mwanya na kufanya muonekano wa mlango wako uwe mzuri zaidi

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ni muhimu ramani ikawa na grid lines ili kurahisisha zoezi la kuset msingi

Katika ramani, huwa kuna kuta nyingi ambapo hizi kuta huwa tunazipa majina mfano kuta A,B,C au 1,2,3 n.k

Ramani ikiwa na hizi grid lines, inakuwa rahisi hata kuelekezana watu wawili ambao hawapo pamoja kwa njia ya simu

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
PLN 0001 2BR

Ramani ya Vyumba Viwili
  • Living room (Sebule)
  • 1 Master bedroom with a Dressing room (W.I.C)
  • 1 Single bedroom
  • Kitchen (Jiko)
  • Public toilet (Choo cha jumuiya)
Ramani hii ina privacy na ventilation ya hali ya juu sana

Bei: Tsh. 100,000/=

Ramani inakuwa na Makadirio yake ya vifaa vya ujenzi kuanzia hatua ya msingi mpaka finishing ambapo itakusaidia kukuongoza katika manunuzi ya vifaa na kuepuka kulanguliwa na mafundi wenye tamaa ya kukuzidishia hesabu ili wajinufaishe zaidi.
View attachment 2694970
Inaukubwa gani
 
Kabla ya kumwaga kifusi kwenye msingi, hakikisha unaziba matundu ya msingi kwa ndani kwa kutumia wavu mdogo utakaokuwa unazuia udongo usitoke nje ya msingi kupitia hayo matundu lakini pia wadudu kama Nyoka, Nge na wengineo wasiweze kuingia ndani

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Unaweza ukachagua kibaraza kimoja wapo (kati ya kibaraza cha mbele sebleni, au kibaraza cha nyuma jikoni) kuweka zege juu ili usiingie gharama ya kujenga mnara wa tank la maji, lakini kingine utakuwa ume-save eneo kwa ajili ya matumizi mengine.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Unaweza ukachagua kibaraza kimoja wapo (kati ya kibaraza cha mbele sebleni, au kibaraza cha nyuma jikoni) kuweka zege juu ili usiingie gharama ya kujenga mnara wa tank la maji pembeni ya nyumba, lakini kingine utakuwa ume-save eneo kwa ajili ya matumizi mengine.

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Habari mkuu Hechy Essy
Haba nilipozungushia nyekundu ni sehemu ya vyoo. Vipi hizo kuta za nyuma nikiweka nguzo za zege na juu nikamwaga zege kwa ajili ya kiwekea tenk la maji itakuwa sawa kweli?
 
Attachments

  • IMG_20241102_080726.jpg
    IMG_20241102_080726.jpg
    604.1 KB · Views: 15
Habari mkuu Hechy Essy
Haba nilipozungushia nyekundu ni sehemu ya vyoo. Vipi hizo kuta za nyuma nikiweka nguzo za zege na juu nikamwaga zege kwa ajili ya kiwekea tenk la maji itakuwa sawa kweli?
Hapo kwa kupaangalia inaonekana ni padogo sana japo sijajua kipimo chake halisi kikoje, upana wa kibaraza ambacho unakusudia kuweka tank la maji juu angalau uzidi futi 8, maana utakapopaua ile overhang ya bati itapunguza ukubwa wa kibaraza kwa angalau futi 1 (mapana na marefu), hivyo utabakiwa na kama futi 7, kati ya bati na tank unaacha tena nafasi japo futi moja, inabaki futi 6 ambayo inatosha kuweka tank la ukubwa wa wastani
 
Mkuu hiyo sehemu iliyotoka nje ni futi 5 kwa maana hstatosha tank la lita 2000
 
Mkuu hiyo sehemu iliyotoka nje ni futi 5 kwa maana hstatosha tank la lita 2000
Haitoshi ndg, mana hata tank la lita 1000 tu kipenyo chake kinazidi futi 4, na pia inabidi kuachwe nafasi kati ya tank na mwisho wa slab inapoishia, tank lisiwe pembeni sana, itafanya uzito wa tank uegemee upande mmoja
 
Back
Top Bottom