yello masai
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 3,662
- 3,715
Mkuu Mungu akubariki sana. Nimeelewa vizuri sana.Kitaalam hapo kwenye kibaraza ilitakiwa pawe chini kwa kozi moja ukilinganisha na level ya msingi wa nyumba ili mtu akiingia hapo mlangoni (sebuleni) apande step moja. Hizo kozi 5 zinazoonekana kwenye kibaraza ilitakiwa ziwe kozi 4 badala ya 5
Upande wa nguzo, nondo zilizotokeza juu kwa ajili ya kuungana na nondo za juu zina urefu mdogo (angalau zingekuwa zimefika urefu wa futi mbili ili zifungwe ringi 4 kwa nafasi ya sentimita 15)
Kingine cha kuwasisitiza mafundi wako waambie wajitahidi kutumia kobilo pande mbili za tofali maana ukiangalia vizuri hizo kuta utaona kuna tofali nyingi zimeinama. Upande mmoja wa tofali ni kwa ajili ya kuliset tofali likae wima, na upande mwingine ni kwa ajili ya kuliset tofali likae mlalo ulionyooka (horizontal)
Unaweza ukanunua hayo material uliyotaja na kuyaweka humo bila shida yoyote lakini je kiusalama hali inaruhusu?, wanaweza wakawa wanakuibia usiku kwa kusombelea na kuhamisha kidogo kidogo mpaka wakamaliza material yote
View attachment 3129227
Kuhusu kozi moja ya kibalaza hapo nifanyeje mkuu. Au niongeze kifusi ndani nipandishe level ya flour ya mpaka mlangoni kwa urefu sawa na kozi moja?
Pia hii ya kutotumia kobilo na tofali kuingia ndani inaweza kuwa na madhara gani huko mbeleni? Hasa kwenye uimara wa jengo.
Natanguliza shukrani mkuu.