Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Haitoshi ndg, mana hata tank la lita 1000 tu kipenyo chake kinazidi futi 4, na pia inabidi kuachwe nafasi kati ya tank na mwisho wa slab inapoishia, tank lisiwe pembeni sana, itafanya uzito wa tank uegemee upande mmoja
Mkuu samahani kwa usumbufu.
Vipi nikitumia hako kaeneo nilikozungushia blue, ndo nimweke zege angalau niweke tank lita 2000.
Hii ni sehemu ya stoo na kibalaza cha nyuma. Ina ukubwa wa 3 × 2 mita.
 
Hilo tank lako lina ukubwa gani (kipenyo chake)?
 
Bei ya mlango mmoja wa mbao pamoja na frem yake ni kati ya 400,000 mpaka 500,000 (mlango 250,000 na kuendelea, frem 150,000 na kuendelea kutokana na ukubwa wa mlango na aina ya mbao zilizotumika)

Kama nyumba yako ina milango 10, maana yake utatumia zaidi ya milion 5 kwenye milango tu

Ili kupunguza gharama, sehemu ambazo hazina ulazima wa kuwekwa mlango, milango usiweke

Mfano, kama kwenye Store ya jiko mtu hawezi kuingia mpaka afungue mlango wa jikoni, basi hakuna ulazima wa kuweka mlango wa kuingilia store

Idadi ya milango inategemea na design ya mpangiliovwa nyumba

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi, usiangalie wengi wanajengaje kwa maana kuna muda huwa inatokea wengi wao ndio wanakuwa wanakosea, na wachache wao ndio wanakuwa wapo sahihi

Mifano ni mingi lakini leo nitatoa mfano mmoja
Katika uwekaji wa slab za makaro ya choo, wengi huwa wanalaza mbao juu ya ukuta halafu ndio wanamwaga zege la slab juu ya mbao

Kitaalam slab za makaro zinatakiwa zilale moja kwa moja kwenye kuta ambapo mbao zinazoishikilia hiyo slab zinatakiwa ziflash na nyuso za juu za kuta na sio kukaa juu ya kuta

Zege ikilala juu ya mbao, baada ya muda (mbao ikianza kuoza), ufa utatokea kutokana na kushuka kwa slab

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Ramani ya vyumba viwili yenye

  • Sebule
  • Jiko
  • Chumba single bedroom 1
  • Chumba self bedroom 1
  • Choo cha jumuiya 1

Ukubwa ni mita 8 kwa mita 10

Kiwanja angalau mita 15 kwa 15

bh.jpg
 
Ramani ya vyumba viwili yenye

  • Sebule
  • Jiko
  • Chumba single bedroom 1
  • Chumba self bedroom 1
  • Choo cha jumuiya 1

Ukubwa ni mita 8 kwa mita 10

Kiwanja angalau mita 15 kwa 15

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasilianeView attachment 3148589
Engineer......nauona msimu wako wa offer amazing za ramani uleeeee Kidesemba fulani hivi ukifika tu tujuze nitakuja faster ka mshale nijipatie kiramani changu kwa bei ya punguzo....dah kukosa pesa kubaya....
 
Mkuu na wakuu
Kwenye jengo la ghorofa moja, kuna ulazima partition za upper floor zifuatishe kuta za chini? Kwamba upper floor siwezi kupitisha ukuta sehemu ambayo chini hakuna kuta?
 
Ni vizuri zaidi kuta za partitions zikafuata kuta za chini, maana ukiweka kuta kwenye slab (ambapo chini yake hakuna mkanda especially kwenye kipande cha moja ya tatu cha kati cha slab, middle strip) unaongeza risk ya slab kubonyea (deflection)

Majengo ya ghorofa huwa yanafanyiwa structural analysis, kwa hivyo kama kuna kuta za partition zinatakiwa zipite kwenye slab (ambapo chini hakuna mkanda), inabidi hizo kuta (wall loads) pia ziwekwe kwenye hiyo slab ili baada ya analysis ikuoneshe kwamba kutokana na mzigo uliouweka, nondo za slab zitatakiwa ziwe na spacing ya sentimita ngapi (kama itafeli kubeba hizo partitions, pia itakuonesha ambapo inaweza kukupa option ya kuongeza depth ya slab au vinginevyo)
 
Engineer......nauona msimu wako wa offer amazing za ramani uleeeee Kidesemba fulani hivi ukifika tu tujuze nitakuja faster ka mshale nijipatie kiramani changu kwa bei ya punguzo....dah kukosa pesa kubaya....
Offer itaanza muda si mrefu kabla ya mwezi december, ili kila mmoja aanze mwaka mpya na ramani yake mkononi, mvua zikikata tu watu waanze kuotesha misingi
 
Ni vizuri zaidi kuta za partitions zikafuata kuta za chini, maana ukiweka kuta kwenye slab (ambapo chini yake hakuna mkanda especially kwenye kipande cha moja ya tatu cha kati cha slab, middle strip) unaongeza risk ya slab kubonyea (deflection)

Majengo ya ghorofa huwa yanafanyiwa structural analysis, kwa hivyo kama kuna kuta za partition zinatakiwa zipite kwenye slab (ambapo chini hakuna mkanda), inabidi hizo kuta (wall loads) pia ziwekwe kwenye hiyo slab ili baada ya analysis ikuoneshe kwamba kutokana na mzigo uliouweka, nondo za slab zitatakiwa ziwe na spacing ya sentimita ngapi (kama itafeli kubeba hizo partitions, pia itakuonesha ambapo inaweza kukupa option ya kuongeza depth ya slab au vinginevyo)
Hata mimi nisiye engineer nimeelewa
 
Hata mimi nisiye engineer nimeelewa
Kwenye kudesign ghorofa, designer anatakiwa ajue kabisa kitu anachokidesign chini (kwenye ground floor), huko juu (first floor) kitakuwa ni kitu gani

Mfano kwenye ground floor, muunganiko wa jiko na store unaweza ukatengeneza chumba ambacho ni self bedroom katika first floor (self room ni chumba na choo, ambapo store kwa upande wa juu inakuwa ni choo, na hilo jiko linakuwa ni chumba)
 
Je kitaalam inawezekana ili kupunguza load ya kuta kwa first floor kukawa na partitionz ambazo sio tofali namaanisha baadhi ya kuta za vyumba zikawa labda za gypsum na material yningine? isiyo ya mchanganyiko wa mchanga na cement
 
Kitaalam inawezaka ili kupunguza load ya kuta kwa first floor kukawa na partitionz ambazo sio tofali namaanisha baadhi ya kuta za vyumba zikawa labda za gypsum na material yningine? isiyo ya mchanganyiko wa mchanga na cement
Mkuu umeandika wazo langu, baada ya Hechy Essy kutoa maelekezo nikawaza hivyo ulivyoandika. Tusubiri majibu. Tunaomba atushauri pia ni material gani tunaweza kutumia
Nina design kule juu ilikuwa 2 rooms sasa nafikiri kuongeza cha tatu kidogo, maana kuna nafasi kubwa tu
 
Sure kiukweli kama kitaalamu inawezekana inaweza ikawa ni option nzuri ya kupunguza gharama maana huu ujenzi ambapo hela unazitaabikia inabidi mtalaam atushauri namna gani ya kupunguza gharama zisizo za lazima
 
Mkuu umeandika wazo langu, baada ya Hechy Essy kutoa maelekezo nikawaza hivyo ulivyoandika. Tusubiri majibu. Tunaomba atushauri pia ni material gani tunaweza kutumia
Nina design kule juu ilikuwa 2 rooms sasa nafikiri kuongeza cha tatu kidogo, maana kuna nafasi kubwa tu
Wataalam wakitumika watasaidia kushauri kitaalam na hii itapelekea kuepusha makosa au kupunguza gharama mfano siku hizi maghorofa ya makazi na hata ya biashara yenye floor 1-3 mengi yanatumia nondo mm 12 kwenye nguzo sasa wengine wanaiiga tu kutumia hizo mm 12 ambapo unakuta hakuna anaysis ya kitaalam imefanyika ili kuona if kweli structural ni sawa.
Kingine nimeona kwenye slab kuna majengo yana kichanja kimoja cha nondo mfano jengo la ilipokuwa branch ya postal bank kariakoo na mengine mengi yanatumia vichanja 2. Sasa fundi maiko ambaye ameona hilo jengo la benk ya posta anaweza conclude kuwa kichanja 1 cha nondo kinatosha!!!
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=toQaa8tgWLc

Nimefuatilia vitu vya watalaamu wa Wazungu. Watalaamu wetu waje na ushauri
 
Je kitaalam inawezekana ili kupunguza load ya kuta kwa first floor kukawa na partitionz ambazo sio tofali namaanisha baadhi ya kuta za vyumba zikawa labda za gypsum na material yningine? isiyo ya mchanganyiko wa mchanga na cement
Partition za gympsum boards au hata zile za PVC boards unaweza ukatumia tu, hazinaga shida kutokana na uzito wake kuwa mdogo kulinganisha na uzito wa kuta za tofali.

Katika designing huwa kuna kiasi flani cha mzigo (dead and live loads) kinawekwa katika slab kwa ajili ya vitu kama kitanda, kabati na vitu vingine vingine vinavyoweza kukaa katika chumba hivyo kwa uzito wa hizo partitions ambazo ni light weight unaweza ukatumia tu bila shida yoyote, japo kuwa partitions za aina hii huwa zinatumika sana kwa matumizi ya muda mfupi maana kudumu kwake ni tofauti na kuta za tofali.

Gympsum boards zinaharibika sana na maji, na ukisema utumie PVC boards bado gharama inakuwa kubwa kuliko gharama ya kujenga kuta za tofali

Option ya mwisho ambayo fundi anaweza kukushauri hapo ni kutumia tofali za nchi 4, na katika kuuweka huo ukuta jitahidi ukuta wako ukae katika kipande cha pembeni cha slab (edge strip, yaani slab unaigawa vipande vitatu vilivyo sawa, then vile vipande vya kati kati unaviruka unatumia vipande vya pembeni) maana kipande cha kati kati (middle strip) ndipo mahali ambapo mbonyeo mkubwa (maximum deflection) unatokea hivyo kupaongezea mzigo ambao haujatambulishwa katika zoezi la structural analysis ni kujiweka katika risk
 
Offer itaanza muda si mrefu kabla ya mwezi december, ili kila mmoja aanze mwaka mpya na ramani yake mkononi, mvua zikikata tu watu waanze kuotesha misingi
Dah fursa hii ya kuanza kighorofa changu, nitakutafuta Engineer unichoree ramani na structural ila ujue kabisaa kwenye nguzo unanichorea structural drawings ya nondo za mm 12 na sio mm 16 kwenye nguzo na usiniwekee nguzo nyingi maana hela zenyewe za mawazo sanaaa 🤣😭😭 japo najua ushasemaga kitaalam NO maana za mm 12 zinanepa ila kibishi nitakutafuta.
 
Back
Top Bottom