Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Ramani, Makadirio, Elimu na Ushauri kuhusu Ujenzi

Mkuu Hechy Essy nina kakiwanja kana ukubwa wa 18m × 18m. Nataka niweke nyumba yenye ukubwa wa 14.5m × 11m. Iwe na vyumba 4 vya kulala, Sebule, Dinning, Jiko na stoo ndogo. Mkuu vipi itawezekana hii?
 
Mkuu Hechy Essy nina kakiwanja kana ukubwa wa 18m × 18m. Nataka niweke nyumba yenye ukubwa wa 14.5m × 11m. Iwe na vyumba 4 vya kulala, Sebule, Dinning, Jiko na stoo ndogo. Mkuu vipi itawezekana hii?
Inawezekana japo vyumba havitakuwa na ukubwa wa kutosheleza, hasa hapo kwenye mapana ya mita 11
 
hapo chapa room za 2.5M × 2.5?
Hapana, minimum size ya chumba cha kulala atleast ianzie 2.7m x 2.7m na kuendelea ambayo ni sawa na futi 9 kwa 9

Room ya 9ft kwa 9ft, ukiweka kitanda cha 5ft kwa 6ft unabaki na nafasi ya 4ft ambayo katika hiyo 4ft unaweza ukaweka kabati la upana wa 1ft au 1.5ft na ukabaki na nafasi ya njia kati ya kitanda na kabati (3ft)
 
Hechy Essy kwa jengo la kawaida la makazi la ghorofa moja nondo size gani ndo zinatakiwa kutumika kwenye slab? Nimesoma mahali kuwa inawezekana kutumia mm 12, na 10 kwenye slab kwa ghorofa moja kwa maana ya kichanja cha juu na chini je hii ni sawa
 
Kwenye slab huwa tunatumia nondo za milimita 12, tofauti huwa inakuja kwenye spacing kati ya nondo na nondo pamoja na kina (depth) cha slab.
 
Uwekaji wa fence katika kiwanja ambacho ni kidogo kunaongeza joto zaidi katika nyumba kutokana na mzunguko wa hewa kuwa mdogo hivyo hutakiwi kujenga fence ambayo ni plain, weka louvers au hata ile miguu ya tembo kila baada ya mita 3 kuruhusu hewa kuingia kwenye nyumba
 
Kabla ya zoezi la kupigilia mbao za dari, fundi anatakiwa atumie pipe level kuchorea alama pote ili dari za vyumba vyote ziwe katika usawa mmoja

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Kuna baadhi ya gympsum board huwa zina alama ya spacing kati ya screw moja na screw nyingine. Hizi ni nzuri zaidi kwa sababu hizo alama zinamuongoza fundi asifunge screw sehemu ambapo hakuna mbao, lakini pia inamuongoza fundi kutoacha nafasi kubwa/ndogo kati ya screw moja na screw nyingine

Nafasi ya kuacha kati ya screw moja na screw nyingine katika ufungaji wa gympsum board angalau isizidi sentimita 20 ambapo kila gympsum board moja itatumia wastani wa screw 50

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika kupunguza gharama za ujenzi, mikanda yote ya nje unaweza ukafunga nondo nne nne, na mikanda ya ndani ukafunga nondo tatu tatu. Hapa nazungumzia mikanda ya juu

Hii ni kwa sababu kuta za nje ndio zinakuwa na madirisha, lakini pia sehemu yoyote ambayo opening yake (iwe ni mlango ama dirisha) inazidi upana wa futi 4 ni vizuri mikanda yake ukafunga nondo nne nne

Offer ya punguzo la bei inaanza leo tarehe 2 December, na itaisha tarehe 31 December

Mkuu mimi hukunipa ushirikiano nilipohitaji kufanya kazi na wewe!

Yaani sijui nakosea wapi tu.

Nashangaa sana.
 
Mkuu mimi hukunipa ushirikiano nilipohitaji kufanya kazi na wewe!

Yaani sijui nakosea wapi tu.

Nashangaa sana.
Njia ya mawasiliano unayotumia ni ngumu sana ndg na hata kule inbox nilikuambia. Ukipiga voice call, ili mtu aone kama simu inaita na apokee ni mpaka awepo online, tunakuwa tunapichana muda wa kuwepo online.

Atleast ungekuwa unaacha voice note, ili hata mtu akiingia online asikilize lakini kupiga voice call pekee, ni mtihani ndg.

Wakati wa kudesign, kuna vitu pia nitahitaji kukuuliza na kama haupo online maana yake itabidi nisitize zoezi kwanza mpaka nitakapopata feedback yako ya kuendelea mbele na zoezi, inaweza ikachukua muda mrefu kumaliza hiyo kazi
 
Njia ya mawasiliano unayotumia ni ngumu sana ndg na hata kule inbox nilikuambia. Ukipiga voice call, ili mtu aone kama simu inaita na apokee ni mpaka awepo online, tunakuwa tunapichana muda wa kuwepo online.

Atleast ungekuwa unaacha voice note, ili hata mtu akiingia online asikilize lakini kupiga voice call pekee, ni mtihani ndg.

Wakati wa kudesign, kuna vitu pia nitahitaji kukuuliza na kama haupo online maana yake itabidi nisitize zoezi kwanza mpaka nitakapopata feedback yako ya kuendelea mbele na zoezi, inaweza muda mrefu kumaliza hiyo kazi
Sasa mkuu,kweli hata kusema upate dakika 10 tu tutaongea tukamaliza ilishindikana?

Dah!

Kuongea ni rahisi sana kuliko voice note.

Nadhani Leo tungekuwa tumemaliza,ila kwa ufupi hadi muda huu nimekwama kuendelea,sababu sina ramani,na nilitegemea tufanye kazi.

Basi tu.
 
Voice note na Maandishi ndio njia nzuri zaidi ndg, voice note unaweza ukairudia kuisikiliza na maandishi pia unaweza ukayasoma kwa mara nyingine tofauti na voice call ambayo hata access yake ni ngumu
 
Ukinunua tofali, jitahidi ununue tofali sehemu moja na ukipata sehemu ambapo wana machine moja tu ya kufyatulia tofali itakuwa bora zaidi.
Hii ni kwa sababu tofali zilizotengenezwa na machine mbili tofauti huwa kuna uwezekano mkubwa wa kupishana ukubwa hivyo inakuwa changamoto katika ujenzi wake

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Nyufa nyingi huwa zinatokea chini ya madirisha kwa sababu mbali mbali lakini moja wapo ni mkanda wa sehemu ya dirisha kuelemewa na mzigo mkubwa juu yake

Mzigo kuwa mkubwa juu ya mkanda husababisha mkanda kupinda (deflection) na kupinda kwa mkanda kunafanya pembe za madirisha zikandamizwe na hivyo kusababisha nyufa

Wengine huweka mkanda kati kati kuzunguka nyumba nzima ili kuzuia hizi nyufa lakini njia nzuri na nafuu ni kuongeza nondo katika nondo za chini za mkanda sehemu za madirisha na pia kuweka ringi karibu karibu (angalau nafasi kati ya ringi na ringi isizidi sentimita 20) ili kuimarisha uwezo wa mkanda kubeba mzigo

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Katika ujenzi kuna size mbali mbali za kokoto, lakini size ambayo inatumika zaidi katika member mbali mbali za zege kama vile nguzo, mkanda, slab n.k ni 3/4" yaani three quarter au 20mm

Nafasi inayoachwa kati ya chuma na box kwa kima cha chini ni nchi 1 sawa na 25mm, kwa hivyo ukitumia kokoto zinazozidi au kulingana na 25mm, kokoto zitashindwa kupita kwenye hiyo nafasi ndio maana tunatumia zaidi size ya 3/4" au 1/2"

Kuna member zingine, nafasi ya chuma na box inatakiwa izidi nchi 1 mfano kwenye vitako vya nguzo ambapo nafasi yake kati ya nondo na box inakuwa ni nchi 1½ hivyo kokoto zake zinatakiwa ziwe kubwa hata 1¼"

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Gharama ya bati na mbao utakayoikwepa/kuisave katika ujenzi wa nyumba za paa la kuficha (contemporary) huwa zinahamia katika kununua material mengine

Hii ni kwa sababu, ujenzi wa nyumba ya paa la kuonekana na ujenzi wa nyumba ya paa la kuficha unatofautiana, haufanani

Nyumba ya paa la kuonekana, kawaida boma lake huwa linajengwa na kozi 13 (kozi 10 kati ya mkanda wa chini na mkanda wa juu japo wengine huweka zaidi, na kozi 3 juu ya mkanda wa juu) lakini kwenye nyumba ya paa la kuficha idadi ya kozi kati ya mkanda wa chini na mkanda wa juu ni zaidi ya kozi 12, na juu ya mkanda zinakaa kozi 6 ama zaidi kutegemeana na slope ya paa na upana wa nyumba.

Mpaka hapo utaona, nyumba ya paa la kuficha linatumia tofali nyingi zaidi ukilinganisha na nyumba za paa la kuonekana. Tofali zikizidi, maana yake na cement pia itaongezeka, mchanga n.k

Kuna gharama tena ya kutengeneza mfereji wa maji ambapo utatumia nondo, cement, kokoto n.k

Mbali na hivyo, nyumba za paa la kuficha zinahitaji marekebisho ya mara mara kama vile paa, rangi katika kuta n.k tofauti na nyumba za paa la kuonekana ambapo marekebisho yake unaweza ukakaa hata zaidi ya miaka 10 bila changamoto yoyote

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Back
Top Bottom